Gwajima Amkana Edward Lowassa...Adai Yeye Hakuwahi Kumuunga Mkono Wakati Wa Kampeni

Mchungaji wa kanisa la ufufuo na uzima,Josephat Gwajima amejitokeza hadharani  na kukana kwamba hakuwahi kumuunga mkono Edward Lowassa wakati wa kampeni za Urais.

Akiongea katika mahojiano maalumu na kituo cha Azam Tv, Gwajima amesema yeye hakuwahi kuwa mshirika wa Lowassa wala chama chochote, bali aliitwa jijini Arusha na Jangwan Dar es Salaam  kwa ajili ya maombi tu na sivinginevyo....

Amesema kitendo cha kukubali wito huo wa maombi kimewafanya watanzania wahisi kwamba yeye alikuwa team Lowassa, kitu ambacho sio kweli.

Amedai yeye alikuwa mfuasi wa mabadiliko ya nchi, alikuwa akiunga mabadiliko ya nchi na SIO  personality ya mtu au chama cha mtu.

Wakati Gwajima akikana kumuunga mkono Lowasaa, kumbukumbu zinaonyesha kuwa mchungaji huyo alikuwa ni team Lowassa na  alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha mheshimiwa Lowassa anashinda kiti cha Urais.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa Gwajima alitumia nguvu kubwa sana wakati wa kampeni kupambana na Dr Slaa ambaye wakati huo alikuwa akishusha makombora mazito kuhakikisha Lowassa hashindi huku akimtuhumu Gwajima kuwa mshenga wa Lowassa aliyemfuata kumpigia debe wampokee Chadema

Tazama Video hii Kumsikiliza Gwajima

Baada ya Mchangaji Gwajima Kumkana Lowassa, nimelezimika  kuitafuta Video ya Maombi ya Gwajima tarehe 29.08.2015 Jangwani, Dar es Salaam wakati UKAWA Walipokuwa wakizindua kampeni zao.

Miongoni mwa maneno aliyoyasema Gwajima siku hiyo ni kuwa Anayemlaani Lowassa  na Haji Duni, Laana iwarudie wenyewe kwa kuwa huu ni wakati wa Lowassa na hakuna wa kumzuia. Je, ni Kweli Gwajima hakuwa mshirika wa Lowassa kama alivyomkana leo?

Tazama video hapo chini

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. na bado
    fake pastor

    ReplyDelete
  2. Mbona ninyi waandishi wa habari ni wa wachokozi? Kampeni ziliisha tangu tarehe 24/10/2015 leo unakumbusha ili iweje. Unajua wakati huo kila mtu alikuwa na kitu au wazo analoona linafaa kwa wakati huo, lakini sasa ni wakati wa kujenga nchi sio nani alifanya nn kwa nani. mimi nilikuwa mabadiliko lakini sasa na kazi tu inafanya kazi. kama mshabiki wa simba au yanga sio dhambi. huo ni utashi wa mtu na huwezi kuzuia. Naomba tukutane tena 2020 october. anayeshinda apewe nafasi ya kuongoza ss wote ni watanzania kuwa upizani sio dhambi ni maisha tu. sawa na watu wengine wapo katika ajira za serikali na wengine binafsi lakini wote hawa ni watanzania na wote wanachangia kwenye pato la Taifa kwa njia moja au nyingine. Kwa hiyo basi wote tuheshimu utashi wa mtu bila kuathiri sheria za nchi ikiwa wewe ni ccm act au chadema hakuna mwenye kosa kuwa miongoni mwa wanachama kati ya vyama hivyo.

    ReplyDelete
  3. Huyu mchungaji feki kweli. Mchungaji anayekataa maneno yake mwenyewe ni lijipu kwa Taifa. Mh rais tumbua n majipu ya wachungaji feki. Mungu mlinde MAGUFULI wetu.

    ReplyDelete
  4. Du! HUYU GWANYOKO NI ZAIDI YA MNAFIKI.

    ReplyDelete
  5. laana za kujifanya askofu, kumbe muuza unga, sasa anabadilisha maneno hata haya haoni.

    ReplyDelete
  6. kakosa mamillio ya Lowasa, kageuka hahaaaa. ni kigeugeu+ Mnafiki

    ReplyDelete
  7. Mungu amfichi mnafiki lol. hata haya haoni

    ReplyDelete
  8. Amefulia huyo achana nae!

    ReplyDelete
  9. GWAJIMA NI MALAYA,MWIZI NA MDANGANYIFU ANAE TUMIA BIBLIA NA KULITANGAZA JINA LA MWENYEZI MUNGU KUWHADAA WAUMINI KWA MANUFAA YAKE BINAFSI NA KUJITAFUTIA UTAJIRI.. NAWASHANGAA WALE WANAO MUAMINI.. ANAFAA KWENDA JELA,,

    ReplyDelete
  10. hahahah kweli hizi ni nyakati za mwisho... Wtz tumefunuliwa lakini hatutaki kuona nani ni Nabii wa KWELI na nani ni MUONGO.

    ReplyDelete
  11. huyu ngwajima ndo ainifanya nisimpe lawasa kura yangu
    huyuu mshenz ngwajima sijui waumini wake kawafanya nini manake ni kama mandondocha vile

    ReplyDelete
  12. Enter your comment...halo oyoooooooooooooo HALLOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO SIASA ZA NCHI MASKINI UTAZIPENDA LOL LOL

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad