Akizungumzia hatua zinazofanywa hivi sasa na serikali kuhusu ada elekezi kwa shule binafsi, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Sifuni Mchome, alisema timu mbili hivi sasa zinafanya kazi ya uchambuzi wa michanganuo ya ada kwenye shule hizo, na baada ya muda mfupi uamuzi utatolewa.
“Hili sasa tumeliundia timu mbili za kufanya uchambuzi wa masuala ya ada katika shule za msingi na sekondari binafsi, ili kuwa na ada ekelezi kwenye utozaji wa ada kuanzia Januari mwakani,” alisema Profesa Mchome.
Aidha, alisisitiza kuwa katika mchakato huo, na kwa muda uliopo hivi sasa hadi Januari ni kipindi kifupi, hivyo inawezekana ada elekezi zikaanza kutumika kwa baadhi ya shule za msingi binafsi, kama eneo la majaribio.
Aliongeza kuwa Tanzania ina shule za msingi 17,000, zikiwamo za binafsi karibu 1,000 na zile za serikali 16,000 na kwamba iwapo wataanza na ada elekezi kwa shule hizo binafsi, wanaweza kuona utekelezaji wake.
Kwa upande wa shule za sekondari, Profesa Mchome alisema ziko zaidi ya shule 4,700 na kati ya hizo shule binafsi ni karibu 1,400 huku za serikali zikiwa 3,300 na kwamba mchakato wa ada elekezi kwa shule hizo binafsi unaendelea pia.
“Timu yetu inaendelea kufanya kazi kwenye mchakato katika shule za sekondari binafsi, zina wadau wengi kwa vile ni nyingi pia, hivyo hatuwezi kutoa maekelezo ya harakaharaka bila kuangalia utekelezaji wake kwa kina,” alifafanua Katibu Mkuu.
Alisisitiza kuwa kwa kuanzia, serikali ilifuta michango yote kwa shule zote nchini na kwamba hatua hiyo inazihusu pia shule binafsi na kuzitaka kutotumia ujanja wa kuingiza michango hiyo kwenye ada kwa madai ya kupandisha ada kwa mwaka ujao wa masomo.
Nafasi za Ajira
Bonyeza www.ajirayako.com
Asante Mungu kutuletea mkombozi,mwenye kusikia kilio cha watanzania
ReplyDeletemaana tumelia siku nyingi juu ya swala hili.Mungu ibariki kazi ya mikono yake pamoja na tume inayoendelea na mchakato huu,Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
hakika. mungu mbariki Rais Magufuri.Nimependa
DeleteMishahara kwa hizo shule binafsi italipwa Na nani? Embu nifumbueni macho...
ReplyDeletendo mashangingi ya wabunge wanaplun na hao wamakontena wakilipa kodi zetu na mafisadi wa TRA wanataifishwa na ela nyingi tu zipo mikononi mwa majizi ya jk, mtalipwa mishahara na posho. pia tinga tinga haitaji mawaziri mzigo.
DeleteKutoa elimu ni huduma, haipaswi kuwa gharama kubwa kiasi hicho! bado mzazi analipa ada 2,000,0000 na anadaiwa michango mengine na bado vitabu mpaka rim paper wananunua wazazi. Shule imekua ni sehemu ya kujipatia utajili na si kutoa huduma. Lazima haya mambo yaangaliwe
ReplyDelete