Hatimaye mzee Samwel Sitta atangaza kustaafu rasmi siasa, hajasema kama atarudi kijijini kulima kama ilivyo kwa wanasisa wengi ambao Mara nyingi wanapostaafu hutangaza kurudi kijijini na kuwa wakulima, lakini pia kilimo kwanza ilikuwa ndiyo Sera ya chama chake katika Serikali ya awamu iliyopita.
Source: Magazeti ya leo
Hatimaye Samwel Sitta Akubali Yaishe Aamua Kustaafu Rasmi Siasa
1
December 23, 2015
Tags
Wakati umefika sasa kwa wanasiasa pamoja na viongozi wote wazee kustaafu. Kihistoria, makundi hayo niliyoyataja yalipata elimu toka kwa mkoloni. Ushahidi unaonesha kuwa elimu waliyopewa na mkoloni haikuwa na lengo la kumuendeleza mu-afrika. Lengo kuu lilikuwa kuandaa tabaka la viongozi ambao wataendelea kulinda maslahi ya wakoloni, hata kama nchi za Afrika zitakuwa zimepata "uhuru".
ReplyDeleteKazi hiyo ndio waliyoifanya, na Waafrika kwa ujumla wamekuwa ni masikini kuliko watu wa mabara mengine kutokana na uwepo wa tabaka hili la viongozi; matatizo ya rushwa na ufisadi kwa asilimia kubwa yanasababishwa na ubinafsi walionao viongozi wa ki-afrika ambao wengi wao wanawakilisha maslahi yao binafsi pamoja na wakubwa zao, yaani nchi "zilizoendelea". Hivyo kwa pamoja, kizazi kipya cha Waafrika kifanye jitihada za dhati za kuwaondoa viongozi hawa katika nydhifa muhimu za maamuzi mmoja baada ya mwingine. Hapo ndipo tutaanza kupanga na kufanyia kazi maendeleo ya kweli ya Muafrika.