Hizi Ndio Dalili za Serikali ya Magufuli Kushindwa? Au Tuendelee Kuwapa Muda?

Nimeamka asubuhi natoka kuelekea kazini. Nimefika kituoni nikakuta daladala imesimama inapakia abiria huku ikiwa tayari imejaa, nikaitwa nipande nikakumbuka AMRI ya serikali kwamba ni marufuku kusimamisha abiria.

Sikupanda nikasubiria nyingine nikazunguka nayo ndani ya daladala abiria tumejaa watu wamesimama hakuna ata pa kuweka mguu. Tunapita barabarani askari awa barabarani wanatutazama tofauti na nilivyohofu kwamba nikikutwa nimesimama nitapigwa faini na wala sioni anayejali.

Nafika ofisini nakuta magazeti tayari yameshafika naona vichwa vya habari waganga wa tiba asili wameigomea serikali na wanamkanya Waziri wa serikali aache kutaka sifa so hawapo tayari kutekeleza amri ya serikali, nikapekua habari iliyoandikwa ukurasa wa juu ya gazeti la mwananchi inaonyesha namna awa waganga wanavyotapeli wananchi..

Kwa habari hiyo ya uchunguzi inaonyesha kifaa ambacho kinatiliwa shaka kinauwezo wa kuchunguza mwili wa binadamu bila kuchukua damu wala kitu chochote mwilini na kutoa majibu ndani ya dakika tatu. Mwandishi kama sehemu ya uchunguzi anaonekana ana tatizo la ugumba ilihali ana watoto tayari alikuwa anawajaribu.

Nilishikwa na ganzi baada ya kusoma hiyo habari nikabaki najiuliza huu ujasiri wa kuigomea serikali wanautoa wapi? Na wanafanya utapeli kama huu bila woga?

Muda wa kazi ukafika tukaanza kufanya kazi ghafla nikakumbuka AMRI ya Waziri wa kazi kwa wafanyakazi wanaofanya bila vibali baada ya kumuona mfanyakazi mwenzangu kutoka Kenya akiendelea na kazi bila wasiwasi wowote na ukweli ni kwamba anafanya kazi bila ya vibali kuangalia around ofisi yote nakuta wale wakenya waliokuwa wanafanya kazi bila vibali bado wapo na hawana uoga wowote na boss wala hashtuki kuwatafutia vibali wapo zaidi ya ishirini(kumbuka deadline ya serikali imeshapita) .

Ndipo nikaanza kupatwa na hofu inamaana awa mawaziri wanapotoa matamko na maelekezo mbona yanapuuzwa? Wasiposikilizwa leo ni lini watasikilizwa? Tatizo ni maagizo hayatekelezeki au watanzania hawapo tayari kwa changes? Au mawaziri hawakujipanga kusimamia utekelezaji? Au Magufuli yupo ahead of time ambapo watanzania awako tayari kufika kwa sasa bado wanataka kufurahia comfort zone?

Sina mashaka kabisa na Magufuli katika kusimamia mambo yake sababu ana historia hiyo ila nimeanza kupata mashaka na mawaziri kama haya mambo ya kusimamia taratibu wataweza au wanajilazimisha ila hawawezi.

Ni hayo tu, kazi njema!
Judi wa Kishua

Nafasi za Kazi
Bonyeza>>www.ajirayako.com

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. acha gvt ifanye kazi tusitafute story za vjiwe

    ReplyDelete
  2. Ukitaka kubomoa nyumba unaanzia juu
    Sasa kuta na msingi wa nyumba vishapata mtikiso
    Then unakuja kuta Na msingi wote wakati huo mvua inayesha ni rahisi kuuchimba na kuuwa na bomoa nyumba yote tupeni muda it's only few days but u have seen it
    Wengine walikaa miaka 10 walilea uupuzi na uuzo huu
    Tushirikiane tutaweza
    Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  3. Ndugu yangu mwandishi,
    1.Nakushauri urudi shule.
    2.Serikali sio Magufuli na mawaziri tu,bali mimi na wewe pia.
    kama umeona kuna mambo yanakwenda ndivyo sivyo unatakiwa
    kutoa taarifa mahali husika.
    3.Nina wasiwasi wewe ni mmoja wanaothubutu hata kuficha wahalifu
    kisa tu unaona kama huhusiki,kumbe kuitengezeza Tanzania
    tunatakiwa wote tuwajibike kwa namna yoyote,na utoaji
    taarifa ni kuwajibika pia.
    4.Wewe ni mmoja wa WaTZ ambao hawako tayari kwa changes.




    ReplyDelete
  4. nimewapenda. muhimu ni kushirikiana kuondoa ubovu. hiyo inainyesha, huyu Judi akimkuta mtoto wa mwenzie katumbukia KISIMANI hawezi mwopoa! manake atasema mamake ni mzembe. kaacha mtoto mpaka kutumbua kwenye kisima chenye kina kirefu!

    ReplyDelete
  5. Mi naona watz wote tuna wajibu kumuunga mkono ndg magufuri kwa vitendo wajibika kwa nafasi yako

    ReplyDelete
  6. Judi wa kishua,unakumbuka hotuba ya Rais Magufuli bungeni?yaani kama una imani na magufuli katika utendaji basi ondoa wasiwasi juu ya mawaziri wake,kwa kuwa kabla ya kukubali kuwa mawaziri wanajua kasi wanayotakiwa kwenda nayo.Tuwaombee uzima katika utendaji wao.

    ReplyDelete
  7. Nina wacwac n mwandishi naona umeandika hili kwa kejeli sana kweli kama ww ni Mtanzania kweli pia inabidi kuwa mzalendo kwa nchi yko. Inabidi tumshukuru Mungu kwa kutupa rais mwenye uchungu n nchi yetu. Ni ngumu sana kila kitu kikae sawa kwa kipind hiki kifupi tulichomchagua tuwape mda kwani tanzania yetu ilikuwa imefikia pabaya sana tena sana. Kwahiyo mpaka hapa kwa kile wanachokifanya tuwatie moyo c kuwakejeli tusizidiwe na Uganda wanakubali kazi ya Rais MAGUFULI mpaka wametunga nyimbo kumpongeza MAGUFULI kwa kazi nzuri anayofanya a lafu cc wa tanzania tunakejeli kazi wanazofanya ni AIBU kwetu. Naungana n nyote hapo juu tuwape viongozi wetu ushirikiano. Ukihamia kwenye nyumba ukakuta mpangaji aliyetoka alikuwa ni mchafu hasafishi choo itakuchukua mda kusafisha hiyo choo ili ing'ae kama utakavyo wewe. Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki JPJMAGUFULI.

    ReplyDelete
  8. Enter your subili kazi wewe

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad