Jakaya Kikwete Aibukia 'Sauzi' Magufuli Akitumbua Majipu Magogoni Aliyomwachia....

Wakati Rais John Magufuli akitimiza siku 31 akiwa amejifungia Ikulu kutatua kero za nchi bila kusafiri nje ya nchi, Rais mstaafu Jakaya Kikwete (pichani) ameendelea kujumuika katika hafla za kimataifa baada ya kuonekana nchini Afrika Kusini juzi akiwa mwalikwa wa Mkutano wa China na Afrika.

Tangu aingie madarakani Novemba 5, Rais Magufuli amepiga marufuku safari za nje kwa watendaji wa serikali bila ya kibali maalumu cha Ikulu.
Alifikia uamuzi huo baada ya kubainisha katika hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge la 11 mwezi uliopita kuwa safari za kimataifa zinatafuna mabilioni ya fedha za walipa kodi.

Rais Magufuli hajasafiri kwenda nje ya nchi mbali na kwenda Dodoma kwa ajili ya kumwapisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na kuzindua Bunge.
Picha zilizotumwa na Ofisi ya Makamu wa Rais jana, zilimwonyesha JK akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, aliyemwakilisha Rais Magufuli kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China, uliomalizika jana jijini Johannesburg.

JK ameonekana katika picha hizo akitembelea mabanda ya maonyesho ya mkutano huo ulioandaliwa na China ili kujadili mikakati ya ushirikiano baina yake na Afrika. 

Ni mara ya pili kwa Kikwete kwenda nje ya nchi tangu Rais Magufuli aingie madarakani. Novemba alionekana katika Jiji la Addis Ababa Ethiopia.

Kwenye utawala wake wa miaka 10, Rais mstaafu huyo alilaumiwa kusafiri mara nyingi nje ya nchi akiwa na msururu wa viongozi na wasaidizi wake hivyo kutumia gharama kubwa, lakini alijitetea kuwa huenda nje kutafuta fedha za maendeleo.

Wakati akihutubia Bunge mjini Dodoma mwezi uliopita Rais Magufuli alisema safari za nje ziliigharamu nchi Sh. bilioni 356 kuanzia mwaka 2013 hadi 2015.

Alisema kati ya kiasi hicho karibu Shilingi bilioni 200 zilitumiwa kwa tiketi za ndege, kadhalika bilioni 68 zilitumiwa kwa mafunzo ya nje wakati bilioni 104 ziliishia kwenye mifuko ya vigogo na maofisa kwa ajili ya posho.

Rais Magufuli alisema mabilioni hayo ya safari yangejenga kilometa 400 za barabara kwa kiwango cha lami akitaja ile inayotoka Urambo Tabora hadi Kigoma mjini.

Katika kutimiza azma ya kupinga safari za nje , Rais Magufuli alikacha kwenda kwenye mkutano wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Madola, uliofanyika visiwa vya Malta wiki mbili zilizopita.

Aliagiza Balozi wa Tanzania jijini London Uingereza na maofisa wengine wanne kuiwakilisha nchi kwenye mkutano huo hatua iliyookoa karibu Shilingi milioni 700 ambazo zingegharamia safari hiyo.

Nafasi za Kazi 

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu mzee WA msoga anapenda anasa Sana apigwe pini

    ReplyDelete
  2. KWA MIAKA KUMI YA UTAWALA WAKE KIKWETE PEKE YAKE ALITUMIA TRILLION 4 KWA GHARAMA ZA SAFARI ZAKE NJE.HAPA BADO PAKA HAJAFUNGWA KENGELE,TUMEIBIWA SANA.

    ReplyDelete
  3. He stil the president of Tanzania
    Oops don't believe
    Only country in the world have to capital cities
    Dar es salaam and Dodoma
    And have two president s
    Wow

    ReplyDelete
  4. Mh. JPM tunakuaminia, na pia tunaamini kwa kasi uliyonayo unamaanisha na utatunasua huku tulikozamishwa na Serikali ya CCM ya JK. Tanzania inahitaji mchapakazi kama WEWE na wengine wa AINA YAKO ili tusongembele kwa maendeleo ya Taifa letu na watu wake. MWENYEZI MUNGU AKULINDE NA KUKUEPUSHA NA HILA ZOZOTE MBAYA ZA WASIOPENDA UTENDAJI WAKO NA WALE WOTE WANAOHOFIA KUFICHULIWA UCHAFU WALIOUFANYA WAKATI WA SERIKALI ZILIZOPITA. Amen. SISI WAPENDA MAENDELEO NA AMBAO TULIYATAMANI KWA MUDA MREFU TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad