Kama jambo hili ni kweli limefanyika: Kigogo wa BoT azuiwa Airport kutokana na kukosa vibali vya kusafiri nje ya nchi
Haiwezekani mtu ambaye yuko huru, tena yuko likizo, ameamua kwenda kujipumzikia zake nchi za wenzetu, azuiliwe!.
Nafahamu kuna wafanyakazi wa serikali, na baadhi ya idara nyeti, au hata madakitari, jeshi, polisi na zimamoto, hata wakiwa likizo, wanawajibika kumtaarifu mwajiri wao, likizo yake atakuwa wapi, ili in case of anything, aweze kuwa reached out!, lakini kitendo cha maofisa uhamiaji, kumzuia mtu mwingine yoyote wa serikali, asisafiri nje ya nchi, huu ni ukiukwaji wa haki za msingi za binaadamu!.
Pamoja na nia nzuri, na nia njema ya Rais wetu, Dr. John Pombe Magufuli, kudhibiti safari za nje ya nchi zisizo na tija kwa taifa, utekelezaji wa kauli hiyo, lazima uzingatie taratibu, sheria na kanuni, na sio kutekelezwa tuu kama zimamoto, na kukiuka haki za msingi za binadamu!.
Ila pia niliwahi kushauri humu, kama baadhi ya sheria, zinaweza kuwa ni kikwazo kwa rais wetu, kututengeneza Tanzania tunayoitaka, rais anayo mamlaka ya kisheria, kuandika waraka, 'decree' kuiweka kando katiba , hivyo kuitawala Tanzania kwa kutumia decree hivyo kuwa huru kufanya jambo lolote atakavyoona inafaa!.
Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria Ongoza Kwa Kutumia Decree tuu!
Viongozi wote wanakula kiapo cha utii wa katiba!, kama katiba inatoa uhuru fulani!, haiwezekana, akaibuka mtu mwingine, kwa mamlaka aliyopewa na katiba hiyo, akauondoa uhuru fulani na haku tunamtazama tuu, au tunamshangilia!. Hili haliwezekani!.
Japo wengi wetu, tunaishi katika lindi la umasikini, uliotopea, na sio tuu hatuna hata hiyo likizo, lakini umasikini wetu, usutufanye tuwachukie, wenzetu waliobahatika kuwa wenye heri, wenye uwezo wa kwenda kujipumzikia zao ulaya wakati wa likizo zao!.
Nashauri serikali itoe waraka wa ufafanuzi wa hili katazo la safari za nje, unless itamkwe wazi, watumizi wote wa umma, hata safari zao binafsi kujipumzikia, au kuwatembelea wapendwa wao, wapenzi wao au hata vimada wao, sasa lazima waombe kibali kwa KMK!, na jee kama hivi ndivyo katiba ilivyotamka?!, kama sio kwa mujibu wa katiba, then rais atoe waraka, Tanzania tujijue tuko kama China au Urusi, enzi zile, kuingia Beijing au Moscow, mtu hujiingilii hivi hivi!.
Jee kumkumbusha rais wetu kuhakikisha watendaji wake wanazingatia katiba aliyoapa kuilinda, ni kumuingilia katika utendaji wake?!.
Pasco/Jamii Forums
Je, Huu Sio Uvunjaji wa Haki Za Msingi za Binaadamu Unaofanywa na Serikali ya Magufuli?
13
December 17, 2015
Tags
Fisadi mkubwa. Ebu muache rais wetu afanye kazi yake.unajifanya kuwa mshahuri nenda kamshauri baba yko kijijini apunguze wanawake.subiri jipu lako linakaribia kuiva. Wabaki hapa nchini wanakimbilia wapi c walijifanya nchi ni ya kwao. Asante Magufuli Mungu akulinde.
ReplyDeleteHUYO BWANA MSAFIRI KWA DHATI YEYE HANA UWEZO WA KUSAFIRI, NA FAMILIA NZIMA MKE NA WATOTO WANNE, KWA MSHAHARA GANI WA MTANZANIA KWENDAKULA BATA LONDON YA X MAS YEYE ANAPATA MSHAHARA GANI? BWANA MAGUFULI WEWE KAZA BUTI TU MPAKA KIELEWEKE TANZANIA IKIKUSANYA ZA KUTOSHA BASI KILA MTU ATASAFIRI
ReplyDeleteHakuna ufisadi Kama hamna uwezo WA kusafiri nje ya nchi hatuhusu
ReplyDeleteMbona tukichangia misaada ya Tanzania hamtuulizi tumepata wapi pesa achani wivu
Watanzania na kama kibano kiwabane hata marais watastaafu
Msoga naye ataruka na pekee bila walinzi Nani analipa
ReplyDeleteChonde Chonde Msoga akiruka tutakusaliti
Utakuwa mnafiki magufuli
Sheria haaingaliiiiiiiii Nani
Mtu aliyekaa kwake watu wakaja kumtembelea
ReplyDeleteMsoga fyuuuuuuuuu
Eti kaalikwa kwa kitu gani au kwa paper kaandika duniani
ReplyDeleteUghaibuni hakuna amjuwaye labda ofisi za ubalozini aliko jaza vilaza waliojuwa hata lugha za nchi wala sheria, utaliiiiiiiii , nini wafanye kazi kuleta ndugu zao na kuzamia ulaya
GO! GO! GO! Rais wetu mpendwa wetu Magufuli, wanyonge woootee tupo nyuma yako. tuliteseka wengi kwa manufaa ya wachache kwani haki za binadamu wakati huo hazikuwepo? sasa hivi watateseka wachache kwa manufaa ya wengi. malipo ni hapa hapa!! Magufuli HUREEEEEE...... mtaisoma namba na bado! bado kabisa ndo kwanza kunakucha.
ReplyDeleteHuyo kibaraka wa mafsad ...umetumwa nn?
ReplyDeleteKwiiii ulihakiki anaenda binafsi? Mtupishee
ReplyDeletekwa sasa nchi imempata kiopngozi ambaye ana image tuu ya ccm na aikili na roho ya ukawa,hiki kitu kinapelekea kuzuka kwa hofu miongoni mwa wana ccm walio kua na fikra za kutumia kivuli cha utawala wa ccm madarakani kuficha na kutetea uchafu wao, kweli wamefanikiwa kubakia madarakani lakini mtu walie mpa ridhaa wanaona kama anawageuka. inazua tafrani na wanabaki na sintofahamu katika fikra zao walikwisha zoeshwa usinipite mwokozi ya serikali ya jakaya.
ReplyDeletethe worst thing that destruct the world is the humanitarian affairs especially human rights.every single human being claim anything he or she want relay on the human right at the end.no one who is above the law, and the maxim that used is dark days of rex non potest pecare has got no room but only in tanzania jus know that.
Kwa jinsi nilivyofahamu mimi hakuna mtumishi wa umma aliekatazwa kusafiri nje ya nchi isipokuwa taratibu zifuatwe. Kusafiri kinyemela kwa kisingizio cha kwenda kula Xmas nje ya nchi ni vichekesho. Nnaishi nje kwa muda sasa na tunapozungumzia Xmas ni wakati mgumu wa kusafiri ni busy angani, busy on the road watu wanarudi makwao kwenda kusherekea Xmas. Kwa mfano kama unaishi Ny city basi wakati huu utaona baadhi ya ndugu zetu weusi wapo safarini kuelekea South Carolina North Carolina,Alabama, Georgia nk wanarudi nyumbani . Sasa kwa kweli inashangaza kuona mtu anakwenda ugenini kwenda kusherekea Xmas? Labda huyo mtumishi ni mgeni si mtanzania tungependa kufahamu. Kwanza Xmas ya ughaibuni haina ladha wala huoni masham masham ya aina yeyote zaidi ya kuikodolea macho tv. Ni siku ya kwenda church na kukutana na wanafamilia. Yaani siku ya Xmas kwa huku nje miji kama hakuna watu ni tuli kabisa tofauti sana na Xmas ya nyumbani jinsi tunavyoisherekea yaani unaweza kusema hakuna furaha ya Xmas huku nje kama ile ya Tanzania licha ya umasikini wa watu wake.
ReplyDeleteKweli ulivyoandika ndugu yangu uishie USA mimi nnaishi hapa Ujerumani sytem or the situation during X-mas time hapa ni sawasawa yaani ni very very boring siku ya X-mas nje humuoni mtu wote ndani tofauti na jinsi X-mas inavyosheherekewa huko nyumbani Tanzania
ReplyDeleteNajua wezi hamkosi la kusema hususani mnapoona kuna mtetezi fulani katokea, Mwacheni raisi wetu atende kazi kadri Mwenyezi Mungu anavyo na atakavyomuongoza. Kama unajua kutetea haki za binadamu, nenda Burundi kazuie watu wasiuawe.
ReplyDelete