Je..Fedha Zilizopigwa Stanbic Bank Ziligharimia Kampeni UKAWA?


Kinara Bashir Awale
UCHUNGUZI unaoendelea wa serikali kuhusu ufisadi wa takribani shilingi bilioni 13 katika mkopo uliochukuliwa kupitia Benki ya Stanbic unaonyesha kuwagusa watu ambao walikuwa mstari wa mbele kwenye kampeni za vyama vilivyo kwenye Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), imefahamika.

Ingawa kiwango halisi cha mkopo ambao serikali ilichukua kupitia benki hiyo ni dola milioni 600 (shilingi trilioni 1.3), ufisadi unaonekana katika kiwango cha dola milioni sita (shilingi bilioni 13) ambazo sasa imethibitika zilitumika kuwahonga viongozi wa serikali ili wauruhusu.

Kinara Bashir Awale
Huyu ndiye aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Stanbic wakati wa kutafuta na hatimaye kupatikana kwa fedha hizo. Kwa mujibu wa taarifa za kimahakama kutoka Uingereza, huyu ndiye alikuwa mtengenezaji wa mpango wote wa kupatikana kwa rushwa hiyo.

Mara baada ya kuondoka kutoka Stanbic mwaka 2013, kutokana na kukataa kutoa ushirikiano wakati wa uchunguzi wa sakata hilo, mara nyingi Awale alionekana akiwa na aliyekuwa mgombea urais wa Ukawa, Edward Lowassa.

Ndani ya kambi ya Lowassa haikuwa siri kwamba endapo angeshinda urais, Awale angeweza kupewa nafasi ya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Yeye ni mmoja wa watu waliokuwa wakitajwa kama wasaka fedha wakuu wa Ukawa na Lowassa. Akiwa na uzoefu wa muda mrefu katika eneo la benki na fedha, Awale alikuwa miongoni mwa wana Ukawa walioweza kujigamba kwamba wako karibu na Lowassa.

Kwa sasa, Awale amefukuzwa nchini kwa madai ya kutokuwa raia wa Tanzania lakini ukaribu wake na Lowassa unaonekana katika baadhi ya picha zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha akiwa katika mojawapo ya mikutano ya kisiasa ya Chadema, akiwa amekaa karibu na mtoto mkubwa wa Lowassa, Fred.

Uchunguzi wa vyombo vya usalama vya Uingereza unaonyesha kwamba wakati wa fedha hizo kulipwa kutoka Stanbic kwenda kwa kampuni ya EGMA, fedha zilikuwa zikitolewa kwenye akaunti na kwenda kwanza kugawiwa kwenye ofisi yake kabla ya kutoka nje ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.

Kinara Shose Sinare
Taarifa za kikachero kutoka Taasisi ya Uchunguzi wa Makosa ya Kijinai ya Uingereza (SFO), zinamtaja mfanyakazi huyu wa zamani wa Stanbic kama SS, na aliwahi kuwa Miss Tanzania mwaka 1996.

Katika ufisadi huu, Shose anatajwa kama msaidizi wa karibu wa Awale na mtu ambaye ukiondoa bosi wake huyo, alifanya kazi kubwa kuhakikisha mpango huo unafanikiwa. Hakuna ushahidi wa moja kwa moja wa kumhusisha Shose na Ukawa zaidi ya hatua ya mama yake, Dk. Eve Sinare, aliyekuwa mwanachama wa muda mrefu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutangaza kuhama chama hicho katika siku za mwisho za kampeni za Uchaguzi Mkuu.

Wakati Dk. Sinare akitangaza kuhama CCM, watu wengi walishangazwa na uamuzi wake huo kwa vile yeye si mmoja wa wanachama maarufu wa chama hicho na hatua yake hiyo haikuonekana kumsaidia yeyote. Mara baada ya kuibuka kwa kashfa hii ya Stanbic, maswali yameanza kuibuka kuhusu mwenendo wao katika wakati huo wa kuelekea Uchaguzi Mkuu. Inadaiwa kuwa kwa kawaida Dk. Sinare na Shose ni watu walio karibu sana.

Harry Kitilya
Huyu alipata kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Ushiriki wake katika kashfa hii umewashangaza wengi kwani kwenye jamii alijenga picha ya kiongozi msafi. Kitilya alikuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni ya EGMA ambayo ndiyo ilipewa kiasi hicho cha shilingi bilioni 13 kwa ajili ya ?kulainisha viongozi wa serikali? kukubali kuchukua mkopo huo kutoka Stanbic.

Wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, jina la Kitilya lilikuwa likitajwa kama mmoja wa watu waliokuwa wakichangisha fedha za kusaidia Lowassa ashinde uchaguzi.

Tofauti na watu kama Awale waliokuwa wakimuunga mkono Lowassa hadharani, Kitilya hakuwahi kutamka hadharani kumuunga mkono mwanasiasa huyo wala kuonekana kwenye mikutano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Kitilya, kwa nafasi aliyokuwa nayo TRA, ni mmoja wa watu waliokuwa wakiombwa ushauri na serikali iwapo ichukue mkopo au isichukue. Kwa maana hiyo, Kitilya alilipwa fedha hizo ili pia naye ?alainike? na ?kuishauri? serikali ichukue mkopo huo hata kama masharti yake hayakuwa muafaka.

Kwa mfano, wakati riba ya kawaida ya mikopo ilikuwa ni asilimia 1.4, mkopo huo ulichukuliwa kwa riba ya asilimia 2.4. Ongezeko hilo la asilimia moja ndilo lililoleta kiwango hicho cha shilingi bilioni 13. Ili kuhakikisha EGMA inapata fedha nyingi kupitia asilimia hiyo moja, badala ya serikali kukopa dola milioni 550 ilizotaka kukopa awali, ikakopa dola milioni 600. Kama ingekopa dola milioni 550, EGMA ingepata dola milioni 5.5 tu.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa SFO, ingawa Kitilya ndiye alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya EGMA, hakuwahi kwenda kuchukua fedha hizo Stanbic na badala yake kazi hiyo ilifanywa na wabia wenzake, Dk. Fratern Mboya na Peter Nyabuti.

Peter Nyabuti
Uchunguzi wa SFO unamtaja Nyabuti kama raia wa Kenya na hakuna taarifa nyingi zinazomhusu. Hata hivyo, katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, Nyabuti alikuwa mmoja wa wateja maarufu katika baa ya Kruz In iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Kwa kipindi kirefu, baa hiyo imefahamika kama kambi rasmi ya ?Marafiki wa Lowassa? ambapo ni kawaida kwa watu waliokuwa kwenye kambi yake; tangu akiwa CCM, kujumuika na kubadilishana mawazo katika eneo hilo. Kwa sababu hiyo, Nyabuti aliyekuwa akichanganyika na watu kama Awale na Fred Lowassa, alikuwa akifahamika kama mmoja wa wapanga mipango na mikakati wa Ukawa.

Ingawa Chadema na vyama vilivyo kwenye Ukawa vimekuwa vikifahamika kwa kupinga ufisadi, hadi sasa hakuna kiongozi yeyote wa kambi hiyo aliyetoa kauli ya karipio dhidi ya ufisadi huo wa Stanbic.

Kwa sasa serikali inafanya uchunguzi kuhusu suala hilo na tayari imeahidiwa kwamba itarejeshewa shilingi hizo bilioni 13 zilizotolewa kama hongo.

Kwa hisani ya RaiaMwema
by MsemajiUkweli/JF



Nafasi za Kazi
Tags

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Na za CCM
    Ndo makonteina, Meno ya tembo
    CCM mnamaneno sana
    Nilifikiri kazi tu kumbe umbea
    Fyuuuuu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Inachoooooma kama pasi!!
      Ndio sababu wakati wa kampeni ukawa hamkuzungumzia kuhusu kupinga ufisadi,mnajijua kwamba nyinyi ni WANAFIKI, na mnaempigia kampeni ndiye FISADI NYANGUMI.....na bado, mtaumbuka sana mwaka huu

      Delete
    2. Koma wewe ushoga na usenge Kama Makonda
      Ufisadi Upo kwenu CCM hata kwenye vyeo angalia wakuu WA wilaya na mikoa oops aibu aibu
      Makapi ya CCM
      Wizi WA kura mbona ya Zanzibar mmeufyata fyuuuuu
      Uchaguzi haurudiwi ngo
      Na ughaibuni mabasha zenu hawatoi missada ngo
      Aibu uchumi wote tulionao bado unategemea missada
      Aibu watoto wanakaa chini tena Dar Es salaam

      Delete
    3. hahahahahah!!! PPIIIIPPPPOOOOZZZZ PWAAAAAAAAA

      Delete
    4. nonymousDecember 15, 2015 at 4:25 PM huoni aibu kutukana mitusi yote hiyo tatizo mijitu ya ukawa haiwezi kubishana kwa hoja ao ni matusi tuu na ndoo maana tunawachapaga kuku nyie
      kuliko kumpa nchi lowasa na ukawa ni mara mia tungeishi bila rais
      sio hao wahuni kuwapa nchii
      PIPOZZZZZZZZZZZZZZZZZZZ
      WEAKNESSSSSSSSSSSSSSSS
      HAKUNA PAWA TENA
      FYUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU

      Delete
    5. michadema ikiongea hadi mipovu inawatoka na mishipa ya shingi pumbavu zenu

      Delete
  2. AHSANTE SANA MUNGU KWA KUTUEPUSHA NA HILI....................
    Bado najiuliza, hivi angeshinda Lowasa hii nchi ingekuwa vipi??? Maana walishajipanga 'wapiga dili'.....sipati picha, watanzania maji tungeyaita 'mmah'! TUNAKUSHUKURU MUNGU KWA USHINDI WA JPJM, TUNAKUOMBA UZIDI KUMTIA NGUVU NA UMLINDE NA MAADUI...AMEN

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mtakalia hivyo hivyo kuwa wapiga debe wenzenu wanakulanchi fala nyie

      Delete
  3. Hiyo pesa ndio ilotumika kununulia chadema, pamoja na 'kuwanyamazisha' akina Tundu Lissu, Msigwa, Mnyika na wale wote walojifanya kupinga ufisadi, ni Dr.Slaa pekee ndio mwenye msimamo wa kweli, wengine wote ndio wale wale'wakubadilisha gia angani'.....hahahaha YAMEWAFIKA HAPAHH!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Senge wewe nini

      Delete
    2. Msenge nini wewe
      Ya CCM mbona husemi
      Mabaliions
      Na mkawapa ubunge tena shame you CCM

      Delete
  4. Wapo kama hawapo, KIMYAA, wangekuwa wenzao, ungeona mapovu yanavyowatoka, wangeshaita na press conference, wameumbukaje! wadogo kama nukta....

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad