Meneja wa operesheni wa kampuni ya huduma za simu za mkononi ya Zantel, Gabriel Rafael ameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi.
Tukio hilo limetokea jana saa 4:45 asubuhi eneo la ofisi za kampuni ya Nabaki Afrika, iliyopo Mwenge, mita chache karibu na kampuni ya Coca-Cola.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura alisema haikujulikana mapema meneja huyo alikuwa akitokea wapi na gari lake aina ya Toyota Double Cabin.
Alisema baada ya kupata taarifa za mtu kuuawa kwa kupigwa risasi, polisi walifika eneo la tukio na kubaini kuwa meneja huyo alikuwa amepigwa risasi kwenye kwapa la mkono wa kulia.
Kamanda Wambura alisema ndani ya gari la mfanyakazi huyo walikuta simu, laptop na fedha taslimu Sh1 milioni.
“Mwili wake umepeleka kuhifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala na polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo pamoja na kuwasaka waliofanya mauaji hayo,” alisema Wambura.
Taarifa za mauaji ya meneja huyo zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii jana mchana zikieleza kuwa, alikuwa akitokea benki kuchukua fedha.
Katika hatua nyingine, Wambura alitoa rai kwa wakazi wote kutumia njia za kiteknolojia kuchukua na kuhifadhi fedha badala ya kutembea nazo mfukoni.
Wafanyakazi wenzie idara moja , waliopiga simu the same day, mkewe
ReplyDeleteWote peleka segerea it's simple kupata ukweli
Haiwezekani Mtu auawe zikutwe 1 million na laptop kwenye gari lake
Waliopo juu ndo wahusika
poleni ndugu, marafiki na jamaa. Mwenyezi Mungu wapunguzie maumivu makali mliyoyata.
ReplyDeletekama ni wezi si wangechukua pesa?
ReplyDeletePoleni sana
ReplyDeleteGabriel umetutoka lakini mimi kama mdogo wako na pia nilifanya kazi na wewe zantel hakika tumepoteza mtu muhimu sana katika tasnia ya telecom ni mtu mwenye uwezo usiekubali kushindwa mchapakazi mpiganaji na ni rafiki wa kweli bila kujali rika hakika inauma na inasikitisha sanaa mimi umeniachia jambo moja kubwa sana ambalo ni utendaji wa kazi kwa vitendo pia kujiongeza pale unapofanya jambo na hata kama boss basi usisubiri kuletewa jambo pia kuwa mbunifu katika kipind chote nilichokaa na ww tukiwa zantel nimejifunza mambo mengi kutojka kwako rai yangu kwa jeshi la polisi kuahkikisha watu wote waliofanya unyama huu wanakamatwa kama kweli alikuwa na pesa na alitoka benk uchunguzi uanzie bank ni nan alimkabdhi pesa na mawasiliano yafuatiliwe asante sana

ReplyDelete