Kasi ya Magufuli Yamkuna Mbunge wa Chadema Sugu, Awataka Madiwani wa Chadema Jimboni Mwake Kushindana na Kasi ya John Magufuli

Sugu Akiteta Jambo
Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu amewataka madiwani wa jimbo hilo waliochaguliwa kwa tiketi ya Chadema kuhakikisha wanafanya kazi kubwa kushindana na kazi ya rais John Magufuli.

Sugu alitoa kauli hiyo hivi karibuni katika kikao cha kumchagua diwani atakayewania nafasi ya Umeya kwa tiketi ya chama hicho.

Aliwataka madiwani hao kuchapa kazi na kuwafanya wananchi kujivunia kasi ya maendeleo inayoletwa na Mbunge na Meya wa jiji hilo ili wasitamani jimbo hilo lingeongozwa na wapinzani wao wa CCM.

“Hata CCM wenyewe wamebadilika, Magufuli anakwenda jalamba. Hakutakuwa na vitu kama ambavyo mnaviwaza, tunaenda kufanya kazi za wananchi ili wananchi wasitamani kwamba afadhali na hapa pangekuwa CCM. Waseme hata kama Magufuli anaenda spidi na sisi Mbeya yetu Meya na Mbunge wanakwenda spidi.”


Nafasi za Ajira

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Bravo mdogo wangu

    ReplyDelete
  2. Sugu wakati unaishi America kuna mtu alikukopeshaga dollar 500 je uliwahi kumrudishia huyo mtu?

    ReplyDelete
  3. WEWE SUGU NI FASIDI TU HUNA LOLOTE KUWADANGANYA WATANZANIA

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad