KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana Amemjibu Lowassa Baada ya Kudai Kazi Nzuri Anayofanya Magufuli ni Sera za Upinzani

KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amemjibu aliyekuwa mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa, aliyedai kuwa kazi nzuri anazofanya Rais John Magufuli, ni utekelezaji wa sera za vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni za mgombea ubunge wa Arusha, Philemon Mollel (Monaban), uliofanyika katika kata ya Daraja Mbili jana, Kinana alisema sera ya kupambana na ufisadi ilizungumzwa katika kampeni na Dk Magufuli peke yake na si Lowassa wala kiongozi yeyote wa Ukawa.

Kinana alisema anamshangaa kiongozi huyo kwa kuwa mbali na kushindwa kuzungumza wakati wa kampeni za urais, pia hakuwa na hotuba yoyote ambayo ingeweza kukaririwa na Dk Magufuli.

Alisema Lowassa hakuweza kuzungumzia masuala yoyote ya kupambana na ufisadi kwa kuwa yeye ni mtuhumiwa na vyama vina vyounda umoja huo ndiyo vimekumbatia ufisadi kwa sasa.

Kwa mujibu wa Kinana, Lowassa alinadi sana mabadiliko kama angeweza kuingia madarakani, lakini hakufafanua ni mabadiliko yapi ambayo angeweza kuyaleta, wakati anatoka katika mfumo ule ule aliokulia kwa zaidi ya miaka 40 akiwa ndani ya CCM na Serikali yake.

“Jamani Lowassa alisema mabadiliko lakini hao wanaotaka mabadiliko wana umri wa ujana sawa na jua linalochomoza la saa mbili asubuhi, wakati yeye anayedai kuleta mabadiliko ana umri wa uzee sawa na jua linalozama la saa 12.30 jioni, si vichekesho hivyo?” Alihoji Kinana.

Alisema kutokana na ukweli huo, ndiyo maana Watanzania walipima na kuamua kumpa ushindi wa kishindo Dk Magufuli, kutokana na uadilifu wake pamoja na uwezo wake wa kuchapa kazi na kuamua kumnyima Lowassa na ndiyo maana kwa sasa anajifariji kwa kusema sera zinazotekelezwa ni za Ukawa.

Akizungumzia kazi alizoanza kuzifanya Rais Magufuli, Kinana alisema zimewakuna Watanzania wengi na kusema kuwa hiyo ndiyo kazi aliyoahidi kwao kuifanya na kwamba anaamini ataifanya kwa dhati katika kuwapigania wananchi wanyonge.

Mfumo wa CCM 
Akizungumzia madai kuwa hakuna kiongozi yeyote atakayetokana na CCM anayeweza kupambana na machafu ndani ya Serikali, kwa kuwa hilo ni suala la mfumo, Kinana alipinga na kusema si kweli.

Akifafanua alisema mfumo unaweza kubadilishwa hata na mtu mmoja kama anavyofanya Dk Magufuli, Makamu wake, Mama Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Alisema moja ya mambo aliyoyaondoa Magufuli katika mfumo huo, ni pamoja na kufuta safari za nje kwa viongozi akiwemo yeye binafsi, kuondoa semina, warsha, makongamano, sherehe na maadhimisho mbalimbali pamoja na posho mbalimbali na kuagiza fedha hizo kwenda katika mahitaji mengine ikiwemo hospitalini.

Akizungumzia uchaguzi wa ubunge unaotarajiwa kufanyika Desemba 13 mwaka huu, Kinana aliwataka wananchi wa Jimbo la Arusha Mjini, kuachana na ushabiki wa vyama na badala yake wachague kiongozi kutokana na sifa zake na kuangalia maslahi yao na siyo ya chama wala kiongozi husika.

Alisema kwa sasa wananchi wa jimbo hilo wanapaswa kuangalia maslahi yao katika kumchagua mbunge, yakiwemo maslahi ya shule, afya, miundombinu, amani pamoja na mambo mengine mengi, badala ya kubaki kuimbiwa kuwa wanafundishwa kuiwajibisha Serikali huku wakibaki katika lindi la umasikini, ukosefu wa amani na maandamano kila kukicha.

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyo Lowasa hana jipya, kwanza tumemshtukia yeye bado ni CCM damu, kazi alotumwa na CCM nadhani bado kidogo ataimalizia, asepe zake.....HATUDANGANYIKI

    ReplyDelete
  2. Hivi ukawa wana sera gani?? Labda ile alilolifanya jukwaani pale Chato ndio sera yao .......'kujinyea'

    ReplyDelete
  3. Meno ya tembo Zurich

    ReplyDelete
  4. LOWASA ANATAPATAPA KMA MTU ANAYE TAKA KUFA BAHARINI NI MJINGA TU

    ReplyDelete
  5. Fanyeni kazi msilete ngonjera hapa.

    ReplyDelete
  6. huyu katibu mkundu wa ficiem mbona yeye apewi uwaziri mwanzie nape kapewa au yeye kazi yake ni kupigia debe chama chenu?

    ReplyDelete
  7. jamani ndugu zangu watanzania naomba tuwe subira ya kupambanua mambo kama Magufuli na serikali yake wanafanya kazi na kazi ya kwanza ambayo wanafanya nchi nzima ni kubomoa nyumba za watu maskini je hyo ni kuongeza umaskini au kuondoa kama wanavyojinadi ok zimejengwa kinyume na sharia wanapowabomelea hawa watu wanaenda wapi? mbona hata mvua au kipunga au moto ulikileta madhara ya uharibifu watu walioathirika wanahifadhiwa je hawa amabo nyumba zao zinabomolewa wanapelekwa wapi? kama Magufuli ni muumini wa wa uadilifu na ufuatiliaji wa sharia basi nafikiri huu ni muda muufaka wa kurudisha nyumba zetu za serikali ambazo ziliuzwa kwa bei ya maandazi! amabzo yeye alikuwa kinara wa uuzaji na alijimilikisha moja wapo ya hzo nyumba! badala ya kuvunja hzi za maskini ambazo nyingi zao zimechangiwa na umaskini wetu ni imani yangu kuwa waliojenga holela wengi sana ni maskini!. Jamani Rais wa nchi na hamasa au sifa ni vitu viwili tofauti! hawa wanaobomolewa nyumba zao na kulala nje ni watu wa rais kama watoto wake ni unafiki kunadi uadilifu usiokuwepo nisameheni jamani naitumia demokrasia yangu kueleza kilicho rohoni mwangu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umechanganyikiwa wewe, kama mpaka sasa hujajua dunia inasimamiwa na sharia kanuni na taratibu. Kuwa mnyonge ama tajiri sio kinga ya kuishi hovyo hovyo bila kufuata utaratibu; sheria lazima ikupitie, usilaumu anayetekeleza sharia. Jisikie aibu kidogo, hata haya anayotekeleza Magufuli leo unayabeza; umechanganyikiwa na kipigo cha uchaguzi nini?

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad