Kiama Cha Waliosafiri Nje Bila Ruhusa ya Rais Chaja....

Adhabu inawanyemelea watumishi wa serikali waliokaidi agizo la kutosafiri nje ya nchi bila kibali cha Rais John Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.

Habari zilizopatikana kutoka baadhi ya wizara  zilieleza jana kuwa tayari baadhi ya Makatibu Wakuu wa Wizara wameshapewa orodha ya majina ya watumishi waliosafiri nje ya nchi kinyemela.

Chanzo kimoja cha habari kiliiambia Nipashe kuwa tayari majina hayo yamepatikana na kinachofanyika sasa ni kupitia taratibu, sheria na kanuni kabla ya kuwachukulia hatua.

Watumishi wanne wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wamesimamishwa kazi kwa kwenda nje ya nchi licha ya maombi yao ya kusafiri kukataliwa na mamlaka.

Jana Nipashe ilifanya mahojiano na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto, Dk. Donald Mmbando ili kufahamu ni watumishi wangapi kwenye wizara yake ambao wamesafiri nje ya nchi  bila kibali cha Rais.

Katika mazungumzo na gazeti hili Dk. Mmbando alikiri kukabidhiwa taarifa kuhusu watumishi waliosafiri nje ya nchi bila kibali cha Ikulu na kwamba kwa sasa kuna taratibu ambazo zinafanyiwa kazi na ngazi husika kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi.

“Ni kweli niliagiza nipatiwe taarifa ya watumishi hao na nimeshapewa ila kuna tataribu ambazo zinafanyiwa kazi na zitakapokamilika itatolewa taarifa ya wale wote waliosafiri na wamefanywa nini,” alisema Dk. Mmbando.

“Kwa sasa siwezi kulizungumzia ila likikamilika tutawajulisha.” Hivi karibuni Dk. Mmbando alitoa taarifa kwa wakuu wa Idara wizarani kwake akiwataka ifikapo Desemba 21 awe amepata taarifa ya wale wote waliokiuka agizo la Rais la kutosafiri nje ya nchi.

Dk. Mmbando aliandika dokezo kwenda kwa wakuu wa idara hiyo ambayo iliwataka kuwataja watumishi walio chini yao ambao walisafiri nje ya nchi baada ya katazo la Rais Dk. Magufuli.

Katika dokezo hilo walitakiwa kueleza watumishi hao wamesafiri kuelekea nchi gani, tarehe ya safari, madhumuni ya safari hizo, safari hizo zimegharamiwa na nani pamoja na kiasi cha fedha kilichotumika.

Waliosimamishwa kazi Takukuru ni Msemaji Doreen Kapwani, Mary Mosha, Ekwabi Mujungu na Rukia Nikitas. Awali, Ofisi ya Rais ilisambaza mwongozo kwa taasisi na mashirika ya umma unaoweka masharti ya ambayo watumishi wa umma wanaotaka kusafiri nje ya nchi watatakiwa kuyatimiza ili wapewe kibali cha kusafiri.

Masharti hayo ni kuomba kibali kwa Katibu Mkuu Kiongozi Sefue na maombi hayo yawasilishwe kwa Msajili wa Hazina kabla ya kwenda kwa Sefue ili mwombaji aweze kujenga hoja kwa kuzingatia umuhimu wa safari hiyo na tija itakayopatikana kutokana na safari hiyo.

Masharti hayo yanamtaka Mtendaji Mkuu wa Shirika ama taasisi apime aone kama safari hiyo ni muhimu  kuombewa kibali kwa Katibu Mkuu Kiongozi kabla ya kuwasilishwa Hazina.

Sharti lingine ni umuhimu wa safari hiyo na isipofanyika itaathiri vipi taifa na mwombaji  aeleze manufaa ya safari hiyo kwa taasisi na taifa kama imewahi kufanyika huko nyuma.

Ofisi za Umma zilipokea barua kutoka kwa Msajili wa Hazina Novemba 12 mwaka huu ikieleza kuwa Rais Magufuli ametoa zuio la jumla kwa safari za nje ya nchi katika utumishi wote wa umma na mihimili yake. Barua hiyo ya Hazina ilisema zuio hilo litadumu hadi pale itakavyoelekezwa vinginevyo.

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. uonevu tuu na ukiukwaji wa demokrasia hata huyo sefue siku zote alikua wapi na wakati na yeye alikua kwenye utawala wa anasa uliopita, nae pia ni jipu

    ReplyDelete
  2. Kumbe kina Vasco da Gama wako wengi. Wanafuata nyayo sasa. Au ndio kuficha "vijisenti",liwalo na liwe?

    ReplyDelete
  3. Ww Anony 4:18 kapimwe akili yko vizur, tena jipeleke mwenyewe milembe. Cjui we we ni Toto la lijipu kubwa tena lenye funza ndani!! Unateteaje mijipu inayotumia pesa za wanyonge kwa kwenda tu kushangaa maghorofa ulaya! Eti democracia hunafahamu unachoongea au umetumwa n jipu lenye funza? Kama we we ni mtoto wa mama Kula,kujisaidia, kulala kaa kimya. Cm yenyewe unayotumia kuandika ujinga wako umenunuliwa n hawara yko jipu. Pita kimya acha mijipu itumbuliwe subiri majipu ya wazazi wako yaive ndo utajua kuwa hapa ni kazi tu. Hii mitoto ya mijipu cjui huwa ina akili gani!! Mungu mlinde Rais wetu mpendwa JPJMAGUFULI.

    ReplyDelete
  4. ujinga na utoto umetawala safari hii, unakuta ni mikutano ya kimataifa tena professionals ila tz hatupeleki, ipo siku tutafutwa katika ramani kisa majipu.

    ReplyDelete
  5. Fyuuuuuuuu
    Wewe sefue usilete sifa na kumkanda aliyekuweka hapo
    Mbona kasi hukuanayo
    Magufuli hili nalo jipu
    Anauma na kuvuvia anayarudisha yote Msoga
    Fukuza wote hao
    I understand wanakupa ushauri lakini hawaendani na kasi
    Makontena naye yumo kwa vimo vyake
    Najuwa zigo lote katwishwa kikwete
    Kikwete ulifanya makosa kuwaonea huruma watu sasa wamekugeuka wanakukanda

    ReplyDelete
  6. Anzeni na Msoga na mkapa
    Wakija ughaibuni tutapiga picha na kuzitoa mtaandaoni
    Tujuwe hii ni amri ya Watanzania au amri ya walala hoi

    ReplyDelete
  7. Wakija ughaibuni wanauza sura tangu marais hakuna hata inzi anawatizama fyuuuuuuuu
    Mipicha tutaoa mkome CCM na unafiki

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad