Kikwete Ajibu Tuhuma Za Kulea Ufisadi Bandarini.......Aitetea Familia Yake, Awapiga Kijembe UKAWA

RAIS mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete amesema katika uongozi wake wa miaka 10, hakuwahi kuagiza mtu asamehewe kontena lake lisilipe kodi na angefanya hivyo, mapato ya Serikali yasingeongezeka kutoka Sh bilioni 177 kwa mwezi mpaka Sh bilioni 900.

Akizungumza baada ya kuwashitukiza wananchi wa Chalinze katika soko kuu la eneo hilo kwa kuungana nao kufanya usafi kuitikia agizo la Rais John Magufuli jana asubuhi, Kikwete alisema katika uongozi wake hakuwahi kuagiza mtu anayestahili kulipa kodi asilipe kodi.

Alisema wakati huu ambao amepumzika baada ya kustaafu, amepata nafasi ya kusoma mitandao na magazeti mbalimbali na kukuta baadhi ya watu, wakimshutumu na kumtukana yeye na familia yake wakimhusisha na ukwepaji kodi.

“Ni afadhali wanishambulie mimi ila wamuache Rais Magufuli (John Pombe) afanye kazi, ni maneno ya walioshindwa wasinilaumu, aliyewashinda ni Magufuli sasa hawana la kusema. Ni sawa na siasa za maji taka, lakini watakuwa wanapoteza muda wao na kufanya kazi bure, kwa kuwa mimi sigombei kitu chochote tena.

“Wanahusisha mpaka na familia yangu, kama mimi mwenyewe sijawahi kuruhusu mtu hata mmoja atoe kontena bila kulipia kodi, siamini kama mke wangu (Mama Salma) au mwanangu Ridhiwani (Mbunge wa Chalinze), wangeweza kufanya hivyo tu na watu wakawasikiliza.

“Wanachonga tu, wengine wamesema Kikwete hachomoki, kwani nimechomeka nini?” Alihoji na kusababisha watu walioshirikiana naye kufanya usafi katika soko hilo kucheka na kuanza kushangilia.

Alisema nafasi ya urais aliyoaminiwa na Watanzania kwa miaka 10, ilikuwa yake na haikuwa na ubia na mkewe wala mtu mwingine yeyote.

Kikwete aliwataka Watanzania wamuunge mkono Rais Magufuli katika jitihada anazofanya za kukabiliana na wakwepa kodi, huku akitoa mfano akisema wakwepa kodi kwa Serikali ni kama inzi na kidonda, hawaondoki bila kufukuzwa na ukiacha kuwafukuza wanarudi.

“Serikali ina wajibu kwa wananchi, wanataka barabara, shule, hospitali ziwe na dawa na mengine mengi, lakini haya yote yanahitaji fedha na Serikali inapata fedha kutoka katika vyanzo vya kodi,” alisema.

Alisema pia yapo mapato mengine ikiwemo ushuru mbalimbali kama katika kulipia leseni, hati za kusafiria na nyingine, lakini pia Serikali inaweza kuchukua mikopo na misaada.

Kikwete alisisitiza kuwa wakati wa uongozi wake, kazi hiyo ya kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuziba mianya ya upotevu wa mapato ilifanyika, ndio maana alifanikiwa kuongeza makusanyo ya kodi kutoka Sh bilioni 177 kwa mwezi mpaka Sh bilioni 900.

Pamoja na mafanikio hayo ya uongozi wake, Kikwete alisema bado mahitaji ya Serikali kwa watu wake, yameendelea kuwa makubwa kuliko upatikanaji wa mapato.

“Tunapaswa kuendelea kuboresha mifumo ya kodi, taasisi za mapato na kupata watendaji waadilifu, kwa kuwa kama mifumo na taasisi vikiwa imara, lakini watendaji si waaminifu haisaidii.

Alisema kazi hiyo anayofanya Dk Magufuli ni kubwa kwa kuwa inahusisha kunyang’anya tonge watu na kusisistiza namna bora ya kumuunga mkono ni kulipa kodi na wakusanyaji wa mapato ya Serikali wawe waaminifu.

Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, alisema hata katika kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho walichokaa juzi, waliamua kumuunga mkono Rais Magufuli na kuwataka wanachama wote wa chama hicho kufanya hivyo.

“Ni pale tu mapato yatakapoongezeka, ndipo wajibu wa Serikali katika kuhudumia wananchi utawezekana, tukimuunga mkono Rais wetu mzuri ataweza na mapato yakiongezeka, maji yatapatikana, mapato yakiongezeka, zahanati na hospitali zetu zitapata dawa za kutosha, mapato yakiongezeka barabara za lami zitajengwa,” alisisitiza.

Alisema katika Serikali Kuu, makusanyo yako nyuma ya asilimia 10 ya lengo, lakini kwa juhudi za Rais Magufuli, hali inavyokwenda lengo hilo litapitwa na Serikali itaanza kuzungumzia makusanyo ya matrilioni kwa mwezi.

Hata hivyo, alisema juhudi hizo za Serikali Kuu hazionekani katika halmashauri ambako ni kama hakuna kazi inayofanyika na hata pale kunapokuwa na juhudi za kukusanya mapato, wakati mwingine yanaishia mikononi mwa wajanja.

Kikwete ambaye alifanya usafi katika soko ikiwemo kufagia, kukusanya na kuzoa taka akiwa na mkewe, huku akikataa kuvaa vifaa vya kuzuia vumbi, aliwataka wananchi kujenga utamaduni wa kufanya usafi.

Alisema uamuzi wa Rais Magufuli wa kutumia maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru, kuwataka wananchi wote wafanye usafi, ni wa busara na si wa kukurupuka kwa kuwa mwaka huu taifa lilikabiliwa na ugonjwa wa kipindupindu.

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hahahaha unajua kosa lako ila kukubali ndo ngumu mheshimiwa

    ReplyDelete
  2. NINGEKUWA MIMI NDO WEWE NINGEFUNGA BAKULI LANGU MANAKE UOZO ANAOUFICHUA MAGUFULI NI TUSI KWAKO! ACHANA WA VIJEMBE MALIZIA UZEE WAKO SALAMA, JAPO SI SALAMA! UKITAKA TUONGEE KUHUSU HAO UNAOWAKINGIA KIFUA UTANUKA KULIKO UNAVYONUKA SASA. ZIPO ISSUE NYINGI TUACHE YALOPITA YAPITE, UNAPOHESHIMIWA JARIBU KUJIHESHIMU.

    ReplyDelete
  3. Wakuwache our ex- Presidaa mtu wa watu ujipumzikie umefanya mengi tu watu hawataki kuona

    ReplyDelete
  4. Hata ningekuwa mimi nisingekubali. Anausika sana tu fisadi mkubwa

    ReplyDelete
  5. Mwachie unyekiti basi wa CCM
    Kwani unao ili kumdhibiti
    Huachi
    Kwani mwana si muuza unga
    Na supermarket kulikoni kufungwa ghafla

    ReplyDelete
  6. tatizo jk urafiki ulikuponza mzee uliwaamini watu ukawaachia ofisi na hao ndo wamefanya madudu sasa lawama zinakuangukia wew ila ndo we learn from our mistakes naamin magufuli amejifunza mengi kupitia wew na tutapata tanzania nzuri chini ya magufuli
    tuzidi kumwombea

    ReplyDelete
  7. upuuzi mtupu aende zake akapumzike asitukumbushe machungu hapa,kazi yake ilikuwa ni kusafiri tu na kuacha nchi inatafunwa,aache wanaume wafanye kazi.

    ReplyDelete
  8. Unajua Mheshimiwa Kikwete unapoongea hususani kuzijibu tuhuma unapaswa uwe mkweli na muwazi.usiongee uongo,usikwepe majibu yanayotakiwa kutolewa,usikwepeshe hoja kwa kujaribu kufanya uchokozi wa jambo au mambo yasiyohusika na tuhuma zinazokuandama.nirudi kwenye majibu yako mepesi.unasema kwenye utawala wako wa miaka 10[2005-2015] mapato ya bandari yalipanda toka billion 177 kwa mwaka hadi billion 900.jee mheshimiwa ports operations za mwaka 2005 kwa maana ya ongezeko la wapitisha mizigo [makampuni,taasisi na watu binafsi] zingekwenda hesabu ya the same graph na ports operations kwa 2015[miaka 10 baadaye?]kichwani mwako unawazia nini Kikwete?Matumizi ya Bandari zetu Yameongezeka mno,Biashara imekua mno,NEW ENTRANTS WAMEINGIA KWA MAELLFU NA MAELFU.HIZO NI PESA MPYA.Kwa Uongozi na Utawala bora Makusanyo ya bandari zetu leo hii 2015 yalipaswa yawe angalau TRILLION 2 KWA MWAKA.hiyo billion 900 YA KWAKO NI MATOKEO YA WIZI MKUBWA,UKWEPAJI KODI,HUJUMA NA MAELEKEZO MABAYA YA KIOFISI.kwa kua sasa umeanza kufunguka tuzungumzie uhusiano wa kibiashara baina yako wewe na wamiliki wa HOME SHOPPING CENTRE Kwa sababu hii siyo siri hususani sisi wakazi wa dar-es-salaam. ili tuone walikwepa kodi trillion ngapi na kwa sasa zinachukuliwa hatua zipi kuwaleta mikononi mwa dola kwa maana ya TRA.

    ReplyDelete
  9. Kwa nini ujitetee mwenyewe wakati wengine hawajapewa kujitetea wenyewe. Unavunja sheria za nchi. Ilibidi tuhuma zipelekwe mahakamani na ndugu, familia na rafiki uliowarudisha kukulindia maslahi pia wsjitetee kortini. Wote wapewe haki kama wrngine waliotiwa ndani. Wewr unapotosha tena nchi. Magufuli kama ndio hivi sinamatumaini nawe hata. Naomba Watanzania wahakimishe sheria za nchi zinafuatwa. Raisi aliyepita asiendeleze mao u ambayo Taifaimeanguka. Wote wafunguliwr mashtaka. Mwakyembe ameshindwa kusimamia jazi akiwa waziri atapewaje tena cheo bila kukamatwa na jufungwa, junyang"nganywa mali na mucungwa kama watu wa chini yake ikiwa yeye ndiye aliyekuwa kiongoxi?.Mtoeni madRakani na msiwasanifu watanzania kama chombo chenu.

    ReplyDelete
  10. Ni hovi anawafocha mafisadi na kujimosha. Bado anaendelea kuwabeba na kujibebesha. Akona zmuhongo, Membe , ndio na familia.anawakata watanzania.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad