KIMENUKA Somalia...Serikali Yapiga Marufuku Sikukuu za Christmass Nchini Humo

Serikali ya Somalia imepiga marufuku sherehe za kuadhimisha Sikukuu ya Krismasi katika mji mkuu wa Mogadishu.

Mkurugenzi mkuu katika wizara ya masuala ya dini, Sheikh Mohamed Khayrow, ameonya kuwa maadhimisho kama hayo yasiyofungamana na dini ya Kiislamu yanaweza kusababisha mashambulizi kutoka kundi la wanamgambo wa Al Shabab.

Maofisa wote wa kulinda usalama wanapaswa kusimamisha ama kuvunja mikutano ya aina yoyote yenye nia ya kuadhimisha sikukuu hiyo isiyofungamana na dini ya Kiislamu.” alisema Sheikh Mohamed

Mwaka uliopita wapiganaji wa Al shabab walishambulia kambi ya majeshi ya muungano wa Afrika (AU) iliyopo Mogadishu wakati wanajeshi hao walikuwa wakisherehekea sikukuu ya Krismasi.
Wanajeshi 5 waliuawa katika shambulizi hilo la kuvizia.
Asilimia kubwa ya raia wa Somalia ni wasilamu.

Credit: BBC
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. jaribu kuzuia waislamu waishio nchi za kikristo kusherehekea sikukuu za eid uone watavyochoma majumba na makazi ya watu...ila wao...

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad