UFALME umeanguka! Unaweza kusema hivyo! Hatimaye Miss Tanzania 2006, aliye pia staa wa filamu za Bongo, Wema Isaac Sepetu amedaiwa kutimuliwa kwenye nyumba ambayo alipanga kwa mbwembwe na kualika waandishi wa habari ili watoe ‘nyuzi’ hewani, akidai ni yake kwa kuinunua kwa shilingi milioni 280, fuatana na Ijumaa Wikienda.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Wema amekumbwa na kadhia hiyo ya kuhamishwa kwenye nyumba hiyo iliyopo Makumbusho jijini Dar, usiku wa Desemba 18, mwaka huu.
SIKIA CHANZO
“Jamani mmesikia kilichomtokea Wema Sepetu? Yaani huyu dada anaishi kwa maigizo hadi basi. Lile sakata lake la kudaiwa kutumia umeme na maji kimagumashi limemtokea puani, maana kwenye umeme pekee yake nasikia anadaiwa zaidi ya shilingi milioni nane (8,000,000) fedha ambazo imekuwa shida kulipa.”
Mizigo ikiwa kwenye gari.
BABA MWENYE NYUMBA AINGIA KATI
“Sasa baba mwenye nyumba ameingilia kati. Ameamua kulipa yeye deni hilo lakini akamtaka Wema ahame haraka kwenye nyumba yake,” kilisema chanzo.
SIKU YA TUKIO
Paparazi wetu alizidi kupenyezewa ‘ubuyu’ kuwa, muda huo tayari kuna lori aina ya Toyota Canter linahamisha vitu nyumbani kwa Wema na kwamba, kuna kila dalili anahama baada ya baba mwenye nyumba wake kumtimua.
PAPARAZI NYUMBANI KWA WEMA
Ilibidi paparazi wetu akimbie kwa pikipiki iendayo kasi mpaka nyumbani hapo na kukuta kweli lori likibeba vitu mbalimbali huku wabebaji wakitokwa jasho chapachapa.
Gari hilo lilisimama kwenye lango kuu la kuingilia ndani ya nyumba hiyo huku likiwa na shehena ya mafurushi ya mizigo.
Muonekano wa mjengo huo.
Wakati paparazi wetu akiwa kwenye hali ya mshangao, aliendelea kuona mizigo mbalimbali ikitoka ndani ya mjengo huo huku vyombo anuai vya ndani, kama kabati na baadhi ya makochi yakiwa nje ya nyumba hiyo yakisubiri kupakiwa tayari kwa safari ya kumuondoa Wema kwenye mjengo huo.
WEMA HAYUPO
Swali la kwanza kwa wabebaji hao kutoka kwa paparazi wetu ni wapi alipo Wema.
“Unamtaka Wema wa nini wakati unajua hayupo hapa, kwanza wewe nani?” alikuja juu mpakiaji mmoja.
Vitu vikiwa nje.
PAPARAZI ANUSURIKA KIPIGO
Katika hatua nyingine isiyokuwa ya kawaida, wapakiaji wengine walitaka kumshushia kipigo paparazi wetu baada ya kuona mwanga wa kamera wakati akichukua picha kadhaa kwa ajili ya ushahidi.
WALIKOHAMIA
Uchunguzi wa awali, Wema amehamia Mbezi Beach, Dar. Hata hivyo, tangu sakata la wizi wa maji na umeme, Wema hajawahi kulala na kuamka ndani ya nyumba hiyo huku habari zikisema amekuwa akiishi mahotelini kama ‘digidigi’.
KWA NINI WEMA ALISEMA NYUMBA NI YAKE?
“Kuna watu wengi walikuwa hawatambui kwa nini Wema awali alisema hii nyumba ni yake. Mwanzo wakati anahamia, pia alikuwa ana mazungumzo na baba mwenye nyumba kwamba ainunue lakini watoto wakagoma hivyo Wema akawa analipa kodi kila mwaka.
WEMA, PETIT MAN
Juzi, Wema hakupatikana hewani ili kujibu madai hayo, lakini mmoja wa watu wake wa karibu, Petit Man alikumbana na paparazi wetu katika klabu moja jijini Dar, alipoulizwa kuhusu mambo hayo alikiri Wema kuhama kwenye nyumba hiyo.
“Tena sasa tunahamia kwenye nyumba aliyonunua Wema mwenyewe. Bonge la nyumba, mtaipata habari yake. Iko Mbezi Beach,” alisema Petit.
Source:Global Publishers
Nafasi za Kazi
Bonyeza>>www.ajirayako.com
Source:Global Publishers
Nafasi za Kazi
Bonyeza>>www.ajirayako.com
Oops makubwa haya
ReplyDeleteUbishoo unataka pesa jamani
Magufuli kafunga mianya yote ya mabuzi
Karibu manzese au Mbagala shoga
huyu binti kama agekuwa anakatika kiungo kimoja kimoja kila akisemwa da tusigekuwa naye
ReplyDeleteNdio faida ya kujikweza kipumbavu, acheni wizi.
ReplyDeleteMimi sio team ushuzi yoyote ila huyo Petit Man na Boss wake wote pyschos
ReplyDeletekwa taarifa yenu kajenga na kahamia kwake. acheni ujinga ndo maana kakaa kimya.
ReplyDeleteMbezi beach kwake
DeleteFyuuuuuuuuu
Jamani!! Haya ni maisha.. Hebu mwachieni huyu mdada afanye mambo YAKE. Her privacy to be respected beside being given
ReplyDeleteWema jipange achana na matumizi yasio ya lazima asaivi ungekua na mjengo wa nguvu unatumia pesa vibaya hile range rover uliyonunua haina maana zaidi ya nyumba
ReplyDeleteno shida... kawaida sana, wengine wanafukuzwa kazi, wengine wanafukuzwa kwenye nyumba walizopanga, wengine wanabomolewa nyumba zao kila uchao,..wengine wanafukuzwa kwenye vyama vyao ni sehemu ya maisha ya binadamu. mimi ni mmojawapo aliyefukuzwa kazi. maisha yanaendelea.
ReplyDeleteBut s vyema kujitapa kuwa vitu vya uongo! Mi mbona naishi kwenye banda langu la mbavu za mbwa c naish jamani;go east go west home is the best;; teh teh teh!!
ReplyDeleteKahamia nyumba yake lakini aache kuiba umeme na maji pambavu zake,yeye hajui hapa kazi tu!!ooops mama ongea na mwanao.hahaha!
ReplyDeletebefore ununue gary la dola elfu 90, ungenunua nyumba kwanza or kujeng. hat kaa is 180 millis, hiyo ingekuwa nyumba nzuri kuliko hatahiyo ulikuwa unakuaa.
ReplyDeletekwani akinunua gari akiacha nyumba wewe kinakuuma nn?
ReplyDeletekapige magoti ubinuke kimgongomgongo madale kwa mjomba dai....kwe kwe kwe!
ReplyDeleteMmmh kumbe Ile nyumba ilikuwa c yakwake kulikuwa na ulazima gani kudanganya umma kuwa nyumba ni yake!! Tena kwa mbwembwe n wahandishi wa habar! Wema acha maisha ya mshumaa unajiteketeza mwenyewe n. umri wako ndo huoo hakuna maana ya kujulikana dunia nzima wakati unahishi maisha ya plastiki.uko ulipohamia piga kimya kimya usitake sifa mwenye nyumba atakufukuza tu. Dah mama uko wapi ongea n mwanao na mkumbushe WEMA SEPETU kuwa duniani kote huwa hakuna Baba/mama mwenye gari hata kama ni range uwa kuna Baba/mama mwenye NYUMBA hata kama ni ya maboksi.
ReplyDeleteEnter your comment... huyo anapenda sifa sana sasa kaumbuka
ReplyDeleteAsione aibu!
ReplyDeleteSuala la kupanga ni jambo la kawaida na iwapo hachagui nyumba na mahali pa kuishi basi niko tayari kumpa nyumba eneo la CHANIKA - Kinyamwezi