Ni kama wahusika wametishwa na hatua ya wakinga-kifua wa Mhandisi Mussa Natty. Pamoja na kurejea Dar es Salaam, kutokea babati, kwa ajili ya uchunguzi dhidi yake kwa tuhuma zinazomkabili, hadi sasa Mamlaka husika zimeshindwa kuanza uchunguzi huo.
Mhandisi Mussa Natty alikuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kabla ya kuwa Mkurugenzi wa Mji wa Babati huko mkoani Manyara alikosimamishwa kazi kupisha uchunguzi. Anakabiliwa na tuhuma mbalimbali za ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka ikiwemo ile maarufu ya kuuzwa kwa fukwe ya Coco.
Taarifa za uhakika zinaonesha kuwa Mhandisi Natty, pamoja na kuwa na nyaraka za kutosha zinazomsafisha, anaondolewa matatizoni na Wakurugenzi wawili waliomtangulia katika Manispaa ya Kinondoni ambao ndiyo hasa waliokuwepo wakati mambo anayotuhumiwa nayo Mhandisi Natty yakitendeka.
Kutokana na kuachwa kando kama washukiwa, Wakurugenzi hao wa zamani na waliomtangulia Mhandisi Natty wameonesha utayari wao 'kumtetea' Mhandisi Natty popote. Pia, Mbunge wa Ubungo na Diwani wa Kata ya Ubungo, Kubenea na Jacob, wameapa kuanika ukweli mambo yakianza kunoga.
Mamlaka zimetishika. Zimepunguza kasi. Zinajiuliza mara mbilimbili. Zinatafakari uwezekano wa kuanza upya kwa kuhusisha watu wapya!
By Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam/JF
Ndo serikali ya Kikwete hiyo.
ReplyDeleteKwa JPJMAGUFULI kila mtu atavuna alichopanda. Jipangeni sana majipu kurudisha mlichopora kwa wananchi.
ReplyDeleteNdio Serikali ya Kikwete imewalea sana mbwa hawa kiasi cha cha kufikia kuwadhalilisha mamilioni ya Watanzania maskini wasiokuwa na mahali pa kukimbilia dah kwa kweli ilikuwa shida......sasa wamfuate Ridhiwan aliyekuwa mshauri mkuu wa Baba yake aende akawateteee
ReplyDelete