Lowassa Afunguka....Magufuli Anatekeleza Hoja Zangu na Chadema

Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa amesema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Magufuli imeanza kuzifanyia kazi hoja zake alizozieleza wakati wa uchaguzi.

Lowassa aliyasema hayo jana jijini Arusha alipokuwa akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema katika uwanja wa shule ya msingi Sinoni.

Lowassa aliishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kumuachia huru Sheikh Issa Ponda na kuiomba kuliangalia pia suala la mwanamuziki, Nguza Vicky (Babu Saye) na mwanae.

“Haya mambo ndiyo tuliyoyaema wakati wa kampeni, sasa namuona Magufuli ameanza kuyatekeleza. Sasa nawaomba angalau wawe wanasema hizo ni sera za Lowassa na Chadema na wanapozitumia basi wawe wanatushukuru,” alisema Lowassa.

Kauli hiyo ya Lowassa iliungwa mkono na waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye ambaye aliwataka pia wananchi wa jimbo hilo kumchagua Lema ili aende bungeni akatumbue majipu ambayo yanapeleka damu kwenye mishipa ya moyo, majipu ambayo alidai CCM haiwezi kuyatumbua.

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kweli Kabisa liwassa wetu

    ReplyDelete
  2. Wameishiwa hoja

    ReplyDelete
  3. polee mzeee
    pole sanaaaaaaaa
    huna sera mzeeeee

    ReplyDelete
  4. inabidi usome tuu afu huache vipite
    magufuli anatimiza ilani ya ukawa as if lowasa ulikemea ufisadi wakati wa kampeni
    zaidi ya kutoa ahadi za matumaini eti nyumba ndani ya siku mia
    duh pole mzee unaitaji maombi
    mwache magufuli awatumikie watanzania sio wew ungewatumikia maswahiba zako wachaga

    ReplyDelete
  5. hoja sio sera za nani sisi tunahitaji maendeleo tu

    ReplyDelete
  6. Mwacheni Magufuli afanye kazi aliyotumwa na Mungu kwa Watanzania.
    Nakumbuka hata Magufuli alipokuja na M4C kwa kunogesha Magufuli for change mlipiga kelele weeeeeee,jembe likaziba masikio kana kwamba hawasikii,sasa mmeanza tena kwamba sera zenu ndio anatumia Kuipika upya TZ mweeh!hamchoki?au ndio maana ya upunzani kwa ukawa?

    ReplyDelete
  7. Namba inasomeka sasa

    ReplyDelete
  8. mtachonga sana vijiba rohoo
    magufuli ndo huyo mbele kwa mbelee hana habari

    ReplyDelete
  9. WEWE LOWASA NI SAWASAWA NA MBWA ALIYE FUNGWA MNYORORO SIKU YAKO ITAFIKA KWA UFASIDI

    WAKO NDIO WATANZANIA WATAELEWA NA HIZO HOJA ZAKO JPM HAZIFATI KAMA UNAVYOSEMA WEWE

    UNATAKIWA UKACHUNGE NGOMBE

    ReplyDelete
  10. Edo we subiri ile mahakama ya mafisadi ianze kazi, itaanza na wewe FISADI NYANGUMI.........

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad