Lowassa Atoa Ujumbe Mzito Kwa CCM baada Ya Kupewa Tuzo ya Amani na Taasisi 1200 Duniani

Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na kuungwa mkono na Ukawa, Edward Lowassa amesema anashangaa kuona anaambiwa mleta vurugu wakati dunia inamkubali kuwa ni mlinzi wa amani.

Kauli ya Lowassa imekuja ikiwa ni siku moja baada ya taasisi za kidini 1,200 duniani kupitisha jina lake kwa ajili ya kumpatia Tuzo ya Amani.

Nimepokea kwa unyenyekevu  na furaha tuzo ya amani duniani ninayotarajiwa kupewa na taasisi za kidini 1200 duniani,” alisema Lowassa akinukuliwa na msemaji wake, Aboubakar Liongo.

Lowassa alisema tuzo hiyo ni kithibitisho cha uongo wa CCM na Serikali yake kuwa wapinzani ni watu wa vurugu.

Taasisi hizo katika kikao chake huko Bukavu DR Congo, zilitangaza kumpa tuzo hiyo Edward Lowassa kutokana na utulivu aliyouonyesha kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.

Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu Kwa jamii,  Mchungaji William Mwamalanga ilisema kiasi wajumbe 1,400 wa mkutano huo kutoka kote duniani walikubaliana kumpa tuzo hiyo Lowassa kati ya wanasiasa 1,000 waliyoshindanishwa ili kumpata kiongozi bora wa Amani mwaka 2015, ambaye anajali na kuangalia maslahi ya jamii badala ya madaraka.

Alisema yeye ni muungwana na ana hofu ya Mungu na hata siku moja hatoweka mbele maslahi binafsi, na ndiyo maana aliwatuliza wananchi waliyokuwa wakimtaka kutoa tamko baada ya matokeo kutangazwa.

Siko tayari kuingia Ikulu huku mikono yangu ikibubujika damu. Nashukuru taasisi hizo za kidini duniani, zimeliona hilo,” alisisitiza Lowassa.

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hapo sio dunia inamkubali Lowasa isipokuwa ni wale wafadhili wake ndio wanajikosha mikono kwa kumpaka chura mafuta kwa mgogo wa chupa!

    ReplyDelete
  2. Tumekuchoka Lowassa endelea Na ishu zako!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Fisi wewe umemchoka kwa kipi

      Delete
    2. nenda leba we uliechoka

      Delete
  3. Viva viva Liwasssaaaaaaaaaaaaaa
    Mkuranga tupo nawe

    ReplyDelete
  4. ni kweli kabisa lowasa ni muungwana na mtu asiye na makelele ni muumini mzuri wa dini yake,,, hana muda wa kujibizana na wakorofi. kweli amedumisha amani mpeni tuzo yake. inammsitahili. acha walala sebeleni waendelee na kelele za chuki kwani mtaji wa mjinga ni majungu.

    ReplyDelete
  5. wafadhili wake wameamua kumpa tuzo kumpoza sio
    huna jipya lowasa unatafuta kiki

    ReplyDelete
    Replies
    1. Koma wewe
      Mbona kikwete Na PhD feki hasemi CCM
      Wasenge kweli nyinyi lakini ya Zanzibar yatawatokea puani

      Delete
    2. ni sifa nzuri kwa taifa hili.

      Delete
  6. Yatamtokea mama ako kwenye mkunduuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  7. ALIYEANDIKIWA KUPEWA HAINA PINGAMIZI NA ANA HAKI YA KUPONGEZWA LOWASA ANAJITAHIDI KWA AMANI NA UTULIVU NA ANAJALI HAKI, ANGALIA MFANO MMOJA WA CCM KWA ZANZIBAR WANAUCHU WA MADARAKA KULIKO KUWAJALI WANANCHI KWA CHAGUO LAO. ALLAH MKUBWA FIRAUNI ALITAKABAR MWISHO ALIJUA KAMA YEYE SIO MUNGU WAKTI UMEPITA.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad