Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amewaagiza watumishi wa wizara hiyo katika kitengo cha huduma kwa wateja, kufanya kazi hadi usiku ili kuhakikisha wanawahudumia kwa muda wananchi wengi wanaofika katika kitengo hicho na kuondoka bila kupata huduma stahiki.
Waziri Lukuvi alitoa maagizo hayo jana alipofanya ziara katika kitengo hicho na kubaini kuwepo urasimu mkubwa unaopelekea wananchi kushindwa kupata huduma kwa wakati.
Baada ya kuzungumza na baadhi ya wananchi waliofika katika kitengo hicho, alibaini kuwepo wananchi ambao wamekuwa wakifuatilia hati zao kwa takribani miezi mitatu bila mafanikio lakini alipoagiza wapewe hati hizo zilipatikana mara moja.
“Watu wasirudi bila kuhudumiwa. Na kama ni wafanyakazi watabaki mpaka usiku, tutafanya utaratibu wa hao wafanyakazi wanaobaki mpaka usiku. Wafanyakazi wabaki muda zaidi lakini kila anayekuja katika kituo kile lazima ahudumiwe,”alisema Lukuvi.
Pia, Lukuvi aliagiza kufungwa kwa mitambo itakayosaidia kutoa huduma za kieletroniki. Alisema kuwa uanzishwe mfumo wa kuwasiliana na wananchi wanaohitaji huduma katika kitengo hicho kwa njia ya barua pepe, whatsap, simu na kadhalika.
Naye Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo ambaye pia ni kamishna Mkuu wa ardhi, Dk Moses Kusiluka alisema kuwa katika utoaji wa huduma hukutana na changamoto inayotokana na baadhi ya watu wanaotaka kujipatia hati kwa njia za udanganyifu bila kuwa na nyaraka za kisheria husasan wanapokuja kuwawakilisha watu wengine.
Wazo ni zuri ika anzisha taratibu watu hawa wafanye kazi kwa shift
ReplyDeleteKwani sheria za kazi duniani kote ni masaa 8
Huduma ziwepo masaa 24
Ardhi ndio kulioza kabisaaaaa.Kila siku tunatangaziwa viwanja,tunafata sheria za mwanzo lakini mwisho wa siku hatuitwi kupewa viwanja,na hata ikitokea ukaitwa basi ujue unaambiwa ulipie mamilion kitu ambacho ni kichekesho ukizingatia wafanyakazi wengi mishahara yetu bado haitoshelezi hata huduma zetu nyingine,Na ndio maana wengi tunaishia kununua kwa wanavijiji kienyeji.Liangaliwe na hilo maana kila mtanzania ana haki ya kumiliki ardhi.Mungu ibariki Tanzania.
ReplyDeleteARDHI WIZARANI BALAA,MATATIZO.WATEJA MNARUHUSIWA KUINGIA PALE SAA TATU ASB MWISHO SAA SABA MCHANA,GETI KUU LINAFUNGWA NA ASKARI HAWARUHUSU MTEJA YEYOTE KUINGIA KUPATA HUDUMA,HII NI AMRI TOKA KWA KATIBU MKUU.PILI SIKU ZA HUDUMA KWA WATEJA NI JUMATATU HADI ALHAMISI TUU.IJUMAA MWIKO HII NI AMRI TOKA KWA KATIBU MKUU.TATU USAJILI WA HATI TOKA WIZARA INAPOPOKEA RASIMU KUTOKA MANISPAA NA HALMASHAURI NI MIEZI MITATU,WAKATI USAJII HUO HUCHUKUA WIKI MBILI TUU-UTAUKUTA USHAHIDI HUO KWENYE MIHURI YAO,NI AIBU.NNE WATUMISHI WANATOKA BILA KUELEZWA WALIKOKWENDA NA WAKATI MWINGINE HAWAREJEI MAOFISINI KABISA.TANO,USHAURI:UANDALIWE MKATABA WA KIUTENDAJI -MKATABA KWA MTEJA- VIKITAJWA WAZI MUDA MAALUMU WA KUSHUGHULIKIA BARUA,NYARAKA,NA HATI ILI KUWALINDA WANANCHI NA PIA KUTUMIKA KAMA KIBANO KWA WATUMISHI WAVIVU NA WAZEMBE AMBAO WIZARA YA ARDHI WAPO ASILIMIA THEMANINI-80%-.MHESHIMIWA WAZIRI HAPO ARDHI ITAKUBIDI UPAMBANE KWELI-KWELI.
ReplyDelete