Madee Amdiss Afande Sele, ni Baada ya Kuwaponda Wanaoshoot Video South

Kauli ya Afande Sele kuwa wasanii wanaoenda kushoot video zao Afrika Kusini wanafanya biashara za siri, haijamuingia vyema hasimu wake wa muda mrefu, Madee.

Bongo5 iliongea na msanii huyo mkongwe wiki hii na kudai kuwa haoni sababu ya maana wasanii wa Tanzania kwenda kufanya video zao nje ya nchi.

Kwenye kushoot video nje ni ulimbukeni,” alisema.

Tanzania tuna kila kitu kuliko hata huko wanakoenda. Mimi hii naitafsiri ni usaliti wa nchi, sisi tunakosa nini hapa nyumbani? Tuna milima, mbuga, maporomoko mazuri, yaani tuna kila kitu. Unajua wasanii wengi walikuwa wanatumia mwanya wa kwenda kushoot video nje ili kufanya biashara zao za siri. Wengi wameutumia sana huu mwanya, sasa Magufuli alivyoingia atawanyoosha tu,” alisisitiza Afande.

Kupitia Twitter, Madee aliandika: Kadri unavozidi kuzeeka na akili nazo zinarudi utotoni na kuambatanisha screeshot ya kichwa cha habari cha habari ya Afande.


Hata hivyo Madee amefafanua zaidi kupitia website ya Millard Ayo ambapo amemtaka Afande aombe radhi kwa kauli hiyo:

Unajua yale ni matusi kwenye muziki kwenye Bongo Fleva halafu watu kama Afande Sele ndio waanzilishi wa huu muziki sasa muziki unapoelekea sasa ni kwenye level ya kimataifa muziki unakua kwahyo vitu alivyokuwa anafanya yeye mwanzo..kwasasa anaviona vipya anaona kama maajabu watu kumiliki hela nyingi…astaajabu na kuhisi labda wasanii wanafanya ishu nyingi.

Anazungumzia suala la wasanii kushoot nje ya nchi Labda tuchukulie mfano John Legend alipotoka kwao Marekani ambapo kuna vitu vingi na kuja Zanzibar kushoot video yake Je alikuja kufanya vitu vya siri eeeh! Hii ni katika harakati za kutanua wigo wa muziki, watu wanataka kufanya vile vitu ambavyo hatukuwahi kufanya ili twende sawa na soko la kimataifa.

Sasa wewe Baba au Babu yetu ambaye unastaajabu kuona watu wanatoka kwenda kushoot sehemu nyingine wewe unasema wanaenda kufanya vitu vya ajabu unakuwa unatukatisha tamaa sisi ambao tumeachiwa hii nafasi kwahiyo nikiwa kama msanii namuomba Afande Sele awaombe radhi wasanii wote kwa ujumla kutokana na kauli yake aliyoizungumza sio nzuri.

Afande na Madee wamewahi kuwa na beef.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hata wafanye akhera video hatuhusu sisi siku hizi mambo yote studio kuna Kila kitu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad