Mbunge wa Ubungo Atiwa Mbaroni kwa Amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda

MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema) amekamatwa na polisi eneo la viwanda (EPZA) Mabibo kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.

Tukio hilo limetokea kukiwa na mgomo wa wafanyakazi zaidi ya 1800 wa kiwanda cha nguo cha TZ TOOKU ambao walimpigia mbunge wao aende kutatua mgogoro huo.

Kubenea alifika katika eneo hilo saa 6 mchana, akakutana na wafanyakazi kusikiliza kero zao za muda mrefu.

Kisha aliamua kuondoka na viongozi wa wafanyakazi hao na kufanya kikao na menejimenti ya kiwanda hicho kuanzia saa 7 hadi saa 9.

Ilipofika saa 10:30 Makonda alikuja na kupata taarifa kwa muafaka uliofikiwa kati ya Kubenea, menejimenti na viongozi wa wafanyakazi.

Alitoa amri wafanyakazi wakusanyike, akaawaambia kesho atafika huko na Waziri wa Viwanda na Biashara, Waziri wa Kazi na Ajira, na Waziri wa Afya Wanawake, Jinsia na Watoto.

Baada ya kutoa maagizo hayo, Makonda alimzuia Mbunge asihutubie kuaga wananchi aliokuwa nao tangu mchana, kutokana na hali hiyo Kubenea alisema ni vema aseme neno, ndipo mvutano ulipoanza.

Makonda alimuru mkutano ufungwe lakini wafanyakazi hawakutawanyika eneo hilo, alipoona hivyo aliamrisha Polisi wamkamate Kubenea, kwa madai alimwita yeye Kibaka.

Katika tukio hilo, Mwandishi wa habari wa Star Tv aliyekuwa anarekodi tukio hilo alinyang’anywa kamera na Polisi aliyejulikana kwa jina moja tu la Denis.

Mwandishi wa habari Mwanahalisi alijaribu kumsaidia mwenzake ili arejeshewe kamera lakini Polisi wa kituo cha Magomeni walimtisha, na kumtaka kuondoka haraka huku wakiondoka na aliyenyang’anywa kamera.

Bado Kubenea anaendelea kuhojiwa na polisi katika kituo cha Magomeni akiwa na mwanasheria wake, Fred Kihwelo.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Makonda unalewa sifa ulimpiga Warioba serikali ya CCM ikafurahia hiyo hali shukrani yao kwako ukapewa ukuu wa wilaya pasipo elimu stahiki, subiri uone kama utaendelea na hicho cheo ambacho ni dhamana, magufuli anataka CV ya kila mkuu wa wilaya na mkoa hivyo vyenu mlivyopewa na hawara yenu kikwete vitawatokea puani nyoko wewe

    ReplyDelete
  2. huyu makonda naona angevuliwa huu ukuu wa wilaya imekuwa balaa kabisa hana busara

    ReplyDelete
  3. Shoga hili
    Fyuuuuuu
    Chakula cha bwana mwanaume mzima ovyo
    Watu wakuheshimu wasikuogope
    Poleni mapolisi kinondoni kufanya kazi na hili senge

    ReplyDelete
  4. Ni aibu Mungu atusaidie viongozi wetu ,kuwa na hekima,ni muhimu zaidi ,wananchi tunatarajia viongozi wakae pamoja wa tatue matatizo yetu,badala yake wanaaibishana ni aibu kwa nchi,inaonekana kuna shida katka madaraka ya viongozi wetu,pia polisi wajue sheria za kuwashika watu,ni sawa kupokea order ila wajue madhara ya maagizo,vyuo vya polisi wafundishwe sheria kidogo zitawasaidia katika majukumu yao ya kila siku,bila hivyo tutaonekana kichwa cha wendawazimu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad