Mkemia mkuu Tanzania: DNA Yabaini 49% Watoto Sio wa Baba Halali

Asilimia 49 kati ya asilimia 100 ya matokeo ya uchunguzi wa makosa ya vinasaba (DNA) yanayowasilishwa katika ofisi ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa mwaka yanaonyesha kuwa baba si mzazi halali wa mtoto katika kesi hizo.

Hayo yamesemwa na Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa wadau wa wakala wa afya ya mazingira leo jijini Dar es Salaam.

Kesi zinazopokelewa katika maabara yetu zinazohusu sampuli ya Vinasaba kwa mwaka zinaonyesha kuwa asilimia 49% kati ya asilimia 100% ya matokeo hayo huonyesha mzazi mmoja ambaye ni baba kuwa si mzazi halali wa mtoto huyo?.

Vinasaba ni utambulisho wa kipekee wa kila kiumbe ambao unabeba taarifa muhimu na inayorithisha tabia au umbile fulani la mhusika. Vinasaba ni kama vile kitabu cha kumbukumbu kinachohusu maisha binafsi?, aliongeza Prof. Manyele.

Profesa Manyele aliongeza kuwa mikoa ya kanda ya Ziwa, Arusha, Dar es Salaam na Mbeya ndio inayoongoza kwa matokeo ya uchanguzi huo wa makosa ya Vinasaba nchini.

Akizungumza kuhusu lengo la mkutano huo, Profesa Manyele amesema kuwa ni kuimarisha uhusiano uliopo kati ya wadau wa kemikali na wadau wa afya ya mazingira kutoka katika halmashauri tofauti nchini pamoja na ofisi ya Mazingira.

Aidha Profesa alibainisha baadhi ya majukumu yanayofanywa na wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali kuwa ni kufanya uchunguzi ili kuhakiki ubora na usalama wa vyakula, dawa, maji, maji machafu, bidhaa za viwanda na mashambani, sampuli za mazingira na sampuli zinazohusiana na makosa ya jinai.

Matokeo ya uchunguzi wa makosa ya jinai na vinasaba (DNA) huviwezesha vyombo husika kufikia maamuzi stahili na kusaidia kutendeka kwa haki katika tuhuma za kesi za jinai ikiwemo ulevi, mauaji, ubakaji, wizi wa

watoto, uhalali wa mtoto kwa mzazi, kwa kupitia vyombo husika? alifafanua Profesa.

Mbali na hayo, alisema wakala kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inatarajia kuwasilisha mapendekezo ya kutunga sheria ya kuunda maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na Sheria ya kusimamia taaluma ya Wakemia, kuimarisha upatikanaji wa mitambo na vifaa vya maabara kila teknologia inapobadilika pamoja na kuimarisha zaidi taratibu za uchunguzi ziwe za kisasa ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknologia.

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Makubwa haya
    Lakini la Zari watu wamelivalia njuga
    Kapimeni kwanza kabla hamjanyooshea Zari kidole
    Team wema
    Hallo

    ReplyDelete
  2. hapo sasa...... teheteheteheteheeee ni shida!! ina maana hao akina baba wanaochapiwa hawana mbegu za uzazi au ni mahanisi.. mi sijaelewa somo.

    ReplyDelete
  3. ndugu mkemia mkuu asante sana kuliweka wazi hili jambo maana kwa miaka ya hivi karibuni vijana wengi hawana mbegu na pampu zao ni ndogo zisizo na nguvu inasadikiwa kwa ajili ya vyakula na vinywaji vya kileo..pia kule wilayani rombo wanaume wengi wameharibika kwa ulevi wa gongo kwa hiyo wanawake wanavuka kwenda nchi iliyo jirani ili wapate wanaume wenye mbegu bora ndo matokeo yake hayo sasa.

    ReplyDelete
  4. haya Dai upooooo!

    ReplyDelete
  5. Hayo matokeo sio kwamba vijana hawana nguvu za kutoa mimba isipokuwa wasichana wengi wanatembea na zaidi ya wavulana 5 katika mwezi mmoja hivyo akijisikia ujauzito anachagua yule anamuona anamshiko mkubwa sasa mvulana ukataana kuseme twende kwenye DNA mimi nitalipia kila kitu matokeo mtoto si wake hivyo hayo ni kwa wasichana wadoga sio wanawake wala wanaume thx

    ReplyDelete
    Replies
    1. kamwambie lyobo wa anti ezekiel naye apime DNA, si umedai kwa mwezi alitembea na wavulana watano

      Delete
  6. michepuko imezidi

    ReplyDelete
  7. APELEKWE TIFA WA ZARI.AMPOZE MAMA DIAMOND ROHO.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad