MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri za jiji la Dar es Salaam, kuwaondoa ombaomba wote walioko katika barabara za jiji, kwani wanachangia uchafu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini jana, Sadiki alisema utekelezaji wa kauli ya Rais John Magufuli ya kutumia siku ya Desemba 9 mwaka huu kufanya usafi, utakwenda sambamba na kuwaondoa ombaomba hao, ambao wanachangia kuongeza uchafu.
“Siwezi kusema wao ni uchafu lakini mazingira yanayowazunguka katika maeneo wanayofanyia shughuli zao wanayachafua, wanajisaidia kwenye mifuko na kutupa ovyo,” alisema.
Alisema viongozi ambao wako katika maeneo ambayo ombaomba hao wanarudi, wahakikishe hawarudi mjini kwa sababu imekuwa ni tabia ya omba omba hao wanaporudishwa baada ya muda kurudi tena jijini.
Aidha, aliiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kushirikiana na Jeshi la Polisi kuwaondoa wapigadebe katika vituo vya daladala kwani wamekuwa kero kwa abiria.
Nafasi za Kazi
Bonyeza www.ajirayako.com
Nafasi za Kazi
Bonyeza www.ajirayako.com
Tutasikia makubwa mwaka huu
ReplyDeleteMlikuwa wapi siku zote
HUYU NAE AFUKUZWE KAZI, ALIKUWA WAPI MIAKA YOTE HIYO YA UCHAFU JIJJNI, LEO ANASINGIZIA OMBA OMBA. UMASKINI WA OMBAOMBA ULISABABASHWA NA WAO KUIIBIA SERIKALI BILA AIBU
ReplyDelete