Mlinzi wa Mfalme wa Qatar Atiwa Mbaroni Moshi Kwa Tuhuma za Kusafirisha Fuvu la Twiga

Kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Jeshi la Polisi kupambana na ujangili, kimemtia mbaroni mlinzi wa mfalme wa Qatar, kwa tuhuma za kusafirisha fuvu la twiga kwenda Uarabuni.

Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Fulgence Ngonyani jana alithibitisha kukamatwa kwa mlinzi huyo wa mfalme na kwamba utaratibu wa kumfikisha mahakamani ulikuwa ukifanyika.

“Ni kweli tuna mtu kama huyo tulimkamata pale (Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro) Kia, akapelekwa Arusha lakini amerudishwa Moshi na mchakato wa kumfikisha mahakamani hapa Moshi unaendelea,” alisema Ngonyani.

Habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi, Idara ya Uhamiaji na Idara ya Wanyamapori zimemtaja mlinzi huyo kuwa ni Jasim Mbarakke Alhkubaisi (43).

Mlinzi huyo amekamatwa wakati mtuhumiwa muhimu aliyepatikana na hatia ya kusafirisha wanyama hao wakiwamo twiga wanne kwenda jijini Doha, Qatar, Kamran Ahmed akiwa hajapatikana licha ya kushtakiwa na kuhukumiwa kifungo baada ya kupatikana na hatia.

Mlinzi huyo alikamatwa Kia, ambako Novemba 26, 2010 walipitishwa wanyamapori 152, wakiwamo twiga.

Taarifa zilizopatikana jana mjini Arusha na Kia, zilidokeza kuwa mlinzi huyo wa Mfalme wa Qatar alikamatwa na kikosi kazi hicho Desemba 18.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, mtuhumiwa huyo alikutwa akiwa na fuvu la twiga, ambalo anatuhumiwa kuwa alitaka kulisafirisha kwenda Qatar kwa kutumia ndege ya Qatar Airways ya nchi hiyo.

“Hii issue (suala) ni nyeti. Kuna maofisa wa ubalozi wa Qatar walikuja hapa Arusha juzi na jana wakijaribu kufanya kila njia asishitakiwe lakini imeshindikana,” alidokeza afisa mmoja wa Uhamiaji.

Taarifa nyingine za uhakika zilisema kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa amelazwa katika hospitali moja jijini Arusha na polisi inaangalia uwezekano wa kulipeleka shtaka lake mahakamani ili asomewe shauri lake akiwa hospitalini.

Kukamatwa kwa mlinzi huyo, kumekuja wiki moja tangu Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, limtie mbaroni raia wa Vietnam, Hoang Nghia Trung (49), akiwa na kucha 261 na meno 60 ya simba.

Kamanda Ngonyani, alikaririwa akisema raia huyo wa Vietnam alikamatwa Desemba 14 saa 10 alasiri kwenye uwanja huo wa Kia.

Kwa mujibu wa Kamanda Ngonyani, mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya polisi wa uwanjani hapo kumtilia shaka na alipopekuliwa alikutwa na nyara hizo za Serikali.

Taarifa hizo zinadai kuwa wakati akikamatwa, kulitokea ubishani baada ya mlinzi huyo kujitetea kuwa alilichukua fuvu hilo kwa ajili ya utafiti, lakini akashindwa kufafanua ni utafiti gani.

Kwa mujibu wa vyanzo, mlinzi huyo alikuwa na hati mbili za kusafiria, moja ikiwa na hadhi ya kidiplomasia na nyingine ya kawaida lakini katika safari hiyo alitumia pasi ya kawaida.

Desemba 5, 2014, Kamran ambaye ni raia wa Pakistan, alihukumiwa kifungo cha miaka 60 jela baada ya kupatikana na makosa manne ya kusafirisha wanyamapori hao kwenda Arabuni bila kibali.

Mbali na kuhukumiwa kifungo hicho, pia Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa, Simon Kobero aliamuru kutaifishwa kwa mali zote za mtuhumiwa huyo zilizopo Tanzania.

Hata hivyo, hukumu hiyo ilitolewa bila ya mtuhumiwa kuwapo mahakamani kwa kuwa alitoroka nchini Februari 2014.

Twiga hao na wanyama wengine walitoroshwa kwenda Arabuni Novemba 26, 2010 kupitia Kia kwa kutumia ndege kubwa ya Jeshi la Qatar.

Wanyama waliotoroshwa kwenda Doha wenye thamani ya Dola 113,715 za Marekani (Sh170.5 milioni), walisafirishwa kwa kutumia maboksi marefu.  

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mpaka wanasafirishwa nyie wa tanzania mulikua wapi

    ReplyDelete
  2. huyu mpuuzi hana la kufanya hapa nchini bali kutaifisha nyara za serikali? maluuni mkubwa

    ReplyDelete
  3. Ni uhusiano wa Kikwete kwa watu hawa.alipokuwa Raisi amemuwa na uhusiano na watu hawa kama ndugu.akitoa vibali vya kuwindia,na kuingiza vitu binafsi toka huko uarabu.msiwashike dagaa tupu. Mfikisheni naye mahakamani kwa uhuumu mkubwa na ufisadi.Ni hawa wamepewa mikataba, ardhi Bagamyo kwa mjomba wao na Ki ukoni.

    ReplyDelete
  4. twiga alishasafirishwa kwa ndege,,, haya sasa fuvu,,,, bado mavi yake...

    ReplyDelete
  5. Mmmh hivi Tanzania hii ndani ya miaka 10 iliyopita ilikuwa n hata balozi wa nyumba kumi kwelia!! kwani mambo yaliyokuwa yanafanyika ni kama nchi hii haikuwa na kiongozi yoyote yule nchi ilikuwa inajipeleka. Hapana ni AIBU tena kubwa sana kutamka eti we we ni rais mstaafu wa Tanzania kwa matukio kama hiyo hapo juu. Wanyamapori 152!! Tena wanapitishwa kwenye viwanja vyetu vya ndege n mijitu inakula mishahara tu. Eti mnamuhukumu Mtu aliyetoroka anatorokaje kwa mfano?? Mbona nchi zao Mtanzania akikamatwa n madawa ya kulevya wanamnyonga?? Kwetu huku wanatoroka hiyo ni akili jamani? M bona makwao sheria ni Kali sehemu ya siri ni yako umepewa n Mungu lakini wakikukuta unazini wanakupiga mawe mpk ufe kwa nn cc sheria zetu zinawalea sana hawa watu? Magufuli okoa nchi hii jamani warudishe wanyamapori wetu. Niliangalia tamthilia ya The stray cat kuna sehem wanaonyesha wanyamapori twiga n wengine nikajiuliza hawa watu Twiga wamepata wapi kwani wale wanyama wamefugwa c kama huku kwetu walivyo kwenye hifadhi zetu no wamefugwa jamani ndo wanyama wetu. Hii nchi ilikuwa imeozaa kwa mijipu mikubwa yenye funza tena kwenye sehemu nyeti ndo mijipu ilipo. Masikini rais wetu ni sehem mbaya mijipu ilipo ila usichoke tunakuombea sana zidi kuitumbua.

    ReplyDelete
  6. Asipofungwa huyu
    Magufuli zirooooooooooo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad