Baada ya kuwa kimya tangu ashinde Ubunge, Mbunge wa Kibamba kwa tiketi ya Chadema, John Mnyika ameibukia kwenye sakata la ubadhirifu kwenye Mamlaka ya Bandari nchini na kuitaka serikali kuweka wazi ripoti za Dk. Harrison Mwakyembe na Samwel Sitta.
Mnyika ameyasema hayo jana alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo amedai kuwa ripoti za Sitta na Dk. Mwakyembe zimebeba ukweli zaidi kuhusu kinachoendelea bandarini hivyo kuziweka wazi kutasaidia kutibu tatizo lililopo zaidi ya kuwasimamisha watendaji waliotajwa.
Akiyafananisha matatizo ya bandari na majipu anayoyatumbua rais John Magufuli, alisema kuwa dawa yake ni kuyapasua ili kuondoa kiini badala ya kuyatumbua tu.
“Dawa ya jipu sio kulitumbua bali ni kulipasua ili kiini cha ndani kitoke, ukikiacha jipu linaazna upya tena linakuwa hatari zaidi,” alisema Mnyika.
“Kama kweli serikali ya awamu ya tano ina lengo la kufichua ufisadi, basi inapaswa kuweka wazi ripoti mbalimbali za uchunguzi ziwe dira ya kujua kiini cha matatizo kujitokeza katika Mamlaka ya Bandari,” aliongeza.
Mnyika Aibukia Sakata la Bandari, Asema Dawa ya Jipu Sio Kulitumbua
7
December 09, 2015
Tags
tumewachoka na nyie ukawa mmezoea kubeza kila kitu hata kiwe kizuri, badala yake hata nyie hamna jipya mnalofanya kwa wananchi zaidi ya kusubiri matukio ili mtengeneze headline. mmekwama HAPA KAZI TU
ReplyDeleteHuo ni upuuzi kabisa anao ongelea Myika wala hajui anacho kizungumza. Utalipasua vipi jipu kabla hujalitumbua kwanza? Mueshimiwa magufuli sio mwanasiasa si mtu wa blah blah ni mtendaji asiekuwa na majungu ni kazi tu. Hao akina sita na mwakyembe walikabidhiwa wizara hiyo wakichokifanya ni kuyapaka mafuta majipu na kuyatengezea ripoti sasa wakati wa kuyawekea vikao ripoti umekwisha ila sasa ni kazi tu.
ReplyDeleteMhe, Mnyika wewe siyo mwanaharati bali ni mwanasiasa, acha uwana harakati siyo muda na level uliyokuwa nayo. Wee ukiwa mbunge jimbo la Ubungo amabalo umelikimbia kwa kushauriwa na wana ukanda wako, uliambiwa uende UBT uanagalie nini kinachofanyika hapo halafu utoe taarifa ngazi husika hasa kuhusu ufisadi unaofanyika hapo, ulileta jibu? tulichokiona ni wewe kubadilika na kunona hadi leo hii.Naamini wewe ni mchaga na kiswahili ukifahamu vizuri kukamua, kutumbua na kupasua ni sawa, au kuna tofauti kati ya maneno,ok,yes , yaah na alright? basi inategemea ni wapi unataka kulitumia na kitu chenyewe.Kulitumbua jibu kunapotumiwa na mhe, rais hakuna maana nyingine ni kutumbua tuu, kwani kupasua kuna ustaarabu kidogo lakini kutumbua kunahitaji roho ngumu bila kumhurumia anayetumbuliwa jibu hilo na hasa likiwa kwenye makalio na kwapani.Wee uanachokitaka unataka rais apsue jibu maana yake ni pamaoja na kutumia kila utaratibu wa kitabibu. hakuna kitu kama hicho na najuwa kuwa kati yao waliotumbuliwa walikuwa financiers wenu ndiyo maana unatoa tafsiri tata. Mhe, acha uwana harakati. ALUTA CONTINUA.
ReplyDeleteUkawa acheni kudandia treni..rudini kwenye majimbo yenu..rais magufuli
ReplyDeleteukawa rudini kwenye majimbo yenu mkafanye kazi
ReplyDeletewatanzania wa sasa wanataka mabadiliko ya kweli na sio ya mdomoni
na uzuri magufuli haangali uchama yeye anataka watu wachapakazi na wazalendo wa kweli
NI UKWELI USIOPINGIKA KUWA MAJIPU YANAYOTUMBULIWA SASA YA VIINI AMBAVYO KAMA VISIPOSHUGHULIKIWA VITAIBUA MAJIPU MENGINE MAKUBWA MNO YA KUJITOA MUHANGA. TASFSIRI YAKE NI KUWA HAKUNA WIZI UNAOFANYA BANDARINI KUPITIA WATEULIWA BILA KUWA NA BARAKA ZA WALIOWATEUA. NA HAO NDIO VIINI VYENYEWE.ITS VERY BAD FOR OUR COUNTRY KWAMBA WALIOTEULIWA NAO WAMETOKA MFUMO ULE ULE SO HAWAKO TAYARI KUSEMA UKWELI ILI KUSAIDIA UCHUNGUZI WA JPM NA JESHI LAKE. KWA UFUPI NDANI YA HAKUNA WA KUMFUNGA KENGELE SHINGONI. NI MUUJIZA KWAMBA NDANI YA MFUMO HUO HUO AMETOKEA MPAKWA MAFUTA AMBAYE YUKO TAYARI KUINGIA GHARAMA KUINUSURU TANZANIA YETU. NA HIZI NI JUHUDI ZAKE BINAFSI SIO ZA CHAMA WALA ILANI YA CHAMA. CCM NA VYAMA VYOTE VYA UPINZANI TUMUUNGE MKONO RAISI WETU KWANI TAYARI AMEAMUA KUONYESHA KUWA ANAYAHESHIMU MAWAZO YENU NA VILIO VYENU VYA MUDA MREFU JUU YA UFISADI NA UHUJUMU UCHUMI KATIKA NCHI HII. ANACHOKISEMA MNYIKA SIO KUMPINGA MH.RAISI BALI NI KUMKUMBUSHA KUWA MAJIPU YALIYOKO NCHINI KWETU YANAHITAJI ZAIDI YA KUTUMBULIWA, YAANI KUPASULIWA NA KUONDOA VIINI KUEPUKA UOTO WA MAJIPU MAPYA NA HATARI ZAIDI YA YALIYOPO SASA.
ReplyDeleteHuyo Mnyika na kundi lake 'wafunge' mabakuli yao, walishasema hawamtambui JPJM kama Rais na hawako tayari kufanya nae kazi, hivyo WAMWACHE AFANYE ATAKALO...........HAPA KAZI TU
Delete