Mtandao Umekufa Rasmi, Kazi Sasa ni Kusafisha Matokeo yake....

Kwa wafuatiliaji wa kisiasa mtakumbuka jinsi mtandao ulioundwa na Kikwete na Lowasa ulivyotikisa siasa za Tanzania toka miaka ya 1990's.
Hatimaye mtandao huu ulifanikiwa kuingia madarakani mwaka 2005 na wakuu wa mtandao huo wakagawana vyeo kama ile waingereza wanaita "spoils of war" , yaani matunda ya kugawana madaraka yaliyotekwa.

Wakati zkikwete aliwasogeza ndugu jamaa na marafiki zake madarakani, Lowasa kwa gia kubwa aliingiza kina Ole wengi kwenye utawala wa mikoa na mashirika ya umma.

Lakini utawala wa tamaa tu na si kutumikia wananchi ulianza kuleta matokeo yasiyo tarajiwa.
Chama CCM kikakosa malengo baada ya vichwa kama Mangula kutimuliwa au kuondoka.
Mawaziri wakawa wengi na walikuwa wanabadilishwa kama circus.
Na kwa vile tamaa haikuishia kutawala tu kwa wana mtandao, tofauti kubwa, na zinazotokana na tamaa ziliibuka kati ya waasisi wa mtandao, yaani Kikwete na Lowassa.

Tofauti hizo na hatimaye ugomvi uliokuwa ukiendeshwa kama gemu la chess, uliishia kuwamaliza wote wawili katika kimsimamo wa kuuendeleza mtandao.

Watanzania lazima tumshukuru Mungu, kwamba ni tamaa ya madaraka na mali ndio imewamaliza wana mtandao.

Magufuli amefanya vema kwa kuanza kuibua madudu ya kutisha ya uongozi ambao ulikuwa hautawali bali unajinufaisha na utendaji wa serikali.

Ni vema utafiti wa kina ujafanywa na wataalam wa sayansi ya jamii , na katika kipindi kifupi, ili madhara mahsusi yatambuliwe, na hatua za kurekebisha zichukuliwe.

Kitu kinachoonekana dhahiri ni kuubinafsisha ukusanyaji wa kodi, na kodi hizo kuingia mifukoni mwa watu binafsi badala ya serikali ili kutumikia wananchi.

Source:JF

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. well said
    apa kazi tuu
    mtandao huamie ukawa
    sasa chama cha wachaga na mbowe
    ccm imerudi mikononi mwa watanzania sasa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad