Mwanasheria Albeto Msando Afunguka Kuhusu Dr Mwaka....Adai Walikuwa Wapi Siku Zote?

Kuna watu watasema ni wivu! Kuna wengine watasema Mwaka ni tapeli! Kuna ambao watakuwa upande wa Kigwangwala na kuna ambao watakuwa kwa Mwaka. Ila je kwa nini mpaka leo hii tiba inahojiwa? Siku zote mamlaka husika zilikuwa wapi? Hao waliotibiwa wakapona wako wapi? 
Ambao hawajapona ni kina nani? Mkurugenzi wa Baraza la Tiba Asili mpaka anafika hapo kwenye 'kliniki' alikuwa hajui kama Mwaka ana vyeti au la? Hakuwa na taarifa zozote za ziada? Je Babu wa loliondo ilikuwaje? Wanaotibu mapenzi na kupata kazi vipi? Wale madaktari wa kusafisha nyota? Au hao kuku weusi wanaokula sio dhuluma? Nadhani Naibu Waziri ameanza kushtukiza ila AENDE NA KWENYE VITUO VYA AFYA NA ZAHANATI PIA. Kuna hao madaktari waliosomea na wao ni bure kabisa huko!! Hili la Mwaka kilichomponza ni kupitiliza!! Wote huwa inatukuta tukinogewa!! Sasa ndio atajua kama bado WATAMPENDA
By Alberto Msando-Instagram

Nafasi za Kazi

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndo maana tunasema majipu yanahitaji kutumbuliwa kwani zamani TRA walikua wapi kukusanya kodi ila leo zinzkusanywa TZ ilikua ya kifisadi ndo mnaana hata leo wakienda kukagua vifaa vya hospitali binafsi unaeza kuta vingine ni vya serikali ila kwa uozo uliokuwepo hakuna aliyekuwa anafatilia

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad