Mwanasheria Mkuu Awakana Wakuu Wa Mikoa Wanaositisha Likizo Za Watumishi

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju amezungumzia suala la wakuu wa mikoa kutoa matamko ya kusitisha likizo za watumishi wa umma kwa kuwataka wafanye kazi tu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalum na kituo cha runinga cha Azam, Masaju amesema amekuwa akisikia kupitia vyombo vya habari kuhusu taarifa za kuwepo matamko hayo kutoka kwa baadhi ya wakuu wa mikoa.

Amesema kuwa hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria na kwamba sheria na katiba ya nchi lazima ifuatwe na watu wote nchini bila kujali cheo cha mtu aliyetoa matamko hayo.

Masaju amesema  kuwa hajawahi kupokea malalamiko yoyote ofisini kwake kutokana na matamko hayo ambayo amekuwa akiyasikia kwenye vyombo vya habari pekee .

Katika mahojiano hayo,Masaju alikataa kueleza moja kwa moja kama uamuzi huo unaochukuliwa na baadhi ya wakuu wa mkoa ni kosa kisheria.

“Mimi sio Jaji wa kusema kuwa waliosema hivyo wamevunja sheria, lakini nataka kusema kuwa sisi sote tunaongozwa na sheria na katiba ambavyo lazima vifuatwe.” Alisema Masaju.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla wametangaza kusitisha likizo kwa watumishi katika mikoa hiyo kwa sababu za kuwataka wafanye kazi tu!

Nafasi za Kazi 

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hawa ma RC wanataka kujipendeka tuuu
    Kimwatumu, makala RC Dodoma Acheni sifa magufuli si kikwete
    Pimeni mmefanya ni tangu mlipoteuliwa
    Magufuli si kipofu wala kiziwi
    Likizo ni haki ya Mtu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad