Serikali imetoa tamko kwa vyombo vyote vya habari nchini kuanzia january mosi mwakani kutotumia miziki ya aina yeyote ,wa ndani au nje bila kibali kutoka Cosota.
Wakitoa tamko hilo kwa pamoja waziri wa habari michezo na utamaduni Nape Nnauye na waziri wa viwanda na biashara Charles Mwijage wamewataka wamiliki wa vyombo vya habari kutoa ushirikiano.
Nape amesema atalisimamia zoezi hilo na kutoa tahadhari kwa chombo chochote cha habari kitachokiuka tamko hilo hatakionea haya kukifungia leseni.
Naye waziri wa viwanda na biashara amesema kuna kampuni ya wazawa ya CMEA ambayo imeanza kazi ya kusimika mitambo yake kila mkoa itakayofanya kazi ya kunakili kila kinachofanyika kwenye kila chombo cha habari.
Kwa upande wa wasanii msanii Nick wa pili amependekeza muziki wa wasanii wa nje ya tanzania uchajiwe gharama kubwa ili muziki wa Tanzania upate nafasi kubwa.
Nape Aonya Vyombo vya Habari Kutumia Miziki ya Wasanii bila Idhini ya COSOTA
3
December 17, 2015
Tags
Asante kaka nape
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeletehaya sasa wasani Mungu awape nini tena
ReplyDeletempige kazi tuu kilichobaki
kazi tuu!