Serikali imechukua hatua hiyo baada ya kupata malalamiko mengi kwa kile kilichokuwa kinarushwa na Kituo cha Televisheni cha TBC1 cha shirika hilo linaloendeshwa kwa ruzuku kutoka Serikalini.
Agizo hilo limetolewa jana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ambaye alibainisha kuwa amepokea simu za watu wengi waliokuwa wanahoji juu ya kipindi hicho, hivyo kulazimika kuchukua hatua mara moja za kutaka maelezo kutoka kwa watendaji wa shirika hilo.
Miongoni mwa programu za burudani na masuala ya kijamii, kituo cha TBC1 kinacho kipindi cha Chereko ambacho hurushwa kila Jumapili kwa matukio ambayo yamerekodiwa, lakini hali ilikuwa tofauti juzi usiku baada ya sherehe za harusi hiyo kurushwa moja kwa moja.
Kwa urefu wa muda uliotumika kurusha sherehe hizo, watazamaji wengi walishikwa na butwaa hivyo kuzua mijadala kwenye mitandao ya kijamii wakihoji inawezekanaje kwa TBC1 kutoa muda mrefu kwa mtu mmoja kwa ajili ya shughuli yake binafsi.
“Mtu hawezi kuitumia Televisheni ya Taifa kwa matakwa yake. Hii ni mali ya umma. kama kila mwenye pesa atakuwa na uwezo wa kulipia muda wa matangazo, si muda wote tutakuwa tunawaona watu wenye hela tu badala ya vipindi muhimu?” alihoji mwananchi mmoja katika mtandao wa kijamii.
Alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Clement Mshana alisema kwa kifupi kuwa kipindi hicho ni sehemu ya vipindi vya kituo hicho cha televisheni.
“Kile ni kipindi cha Chereko ambacho tunacho kwenye programu zetu,” alisema Mshana.
Alipoulizwa ilikuwaje ratiba ya kipindi hicho ikabadilishwa kutoka Jumapili mpaka Jumamosi, alisema: “Kile ni kipindi cha wikiendi na kama mtu sherehe yake inafanyika siku hiyo, inakuwa haina shida yoyote.”
TBC ni shirika linalomilikiwa na Serikali likiwa na televisheni na redio.
Wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu, kituo hicho kilikuwa kikilalamikiwa kwa kuendesha kwa upendeleo kipindi cha Jambo Tanzania ambacho hupitia na kusoma magazeti makubwa ya kila siku. Katika moja ya vipindi hivyo, habari zilizokuwa zikihusu wagombea wa upinzani zilikuwa hazisomwi licha ya kuwamo kwenye magazeti yaliyokuwa yakichambuliwa.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene amewahi kukaririwa akisema kuwa ameshaliandikia barua za onyo shirika hilo juu ya kukiuka kanuni za utangazaji ambazo hazitaki upendeleo wa aina yoyote
Nafasi za Kazi
Bonyeza >>www.Ajirayako.com
TBC WABAGUZI WALA SIIANGALII IMEKUWA NI TV YA CHAMA KIMOJA TU KAMA KWA KULE ZANZIBAR UTAKUTANA NA ZBC NAO WABAGUZI KUPITA KIASI WALA HAWAJIFICHI HOTUBA WANAZOEKA NI ZA RAIS WA 1995 ALIEULETA UBAGUZI WA UUNGUJA NA UPEMBA PAMOJA NA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA ZANZIBAR.
ReplyDeleteWewe umesema huangalii, hayo ya hotuba za 1995 umejuaje??
ReplyDeleteHebu wacha unafiki, kama huangalii ungekaa kimya.
Toka alipo ondoka TIDO TBC imepoteza dira
ReplyDeleteHaa haaa.. Majanga...akae kmya eeeh...BT all n all.. TBC haiko kimisingi ya utaifa...na tido mhando silaha pekee ingewapeleka mbali.
ReplyDeleteHaa haaa akae kimya sio...ukimya sio njia ya mabadiliko na demokrasia anasema uwazi kuondoka kwa tido mhando kumefanya tbc ipoteze misingi ya utaifa na kuwa ya watu wachache..wanapotea na watakwama hakuna ubabaishaji karne hii
ReplyDelete