Pamoja Kuwa na Kashfa ya Escrow Huyu Ndio Waziri Anayefanya Kazi Kuliko Mawaziri Wote wa John Pombe Magufuli....

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto mbele) akimsikiliza Mhandisi wa kituo cha kufua umeme wa dharura cha Kibeta- Bukoba mjini, Mhandisi Filbert Mlaki wakati wa ziara yake kituoni hapo leo (27 Desemba, 2015). Kituo hicho chenye mitambo minne kinao uwezo wa kuzalisha megawati 2.1 ambacho hutumiwa pale umeme wa kutoka Uganda unapokatika.

Serikali imesema ifikapo mwaka 2018 Mfumo wa umeme katika Mkoa wa Kagera utakua umeingizwa kwenye Gridi ya Taifa.
Hayo yalisemwa jana tarehe 27 Desemba na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alipofanya ziara mjini Bukoba, Mkoani Kagera ili kukagua miundombinu ya umeme.
Ilielezwa kwamba Mkoa huo kwa sasa unapata umeme kutoka nchini Uganda ambao umekuwa ukikatika mara kwa mara na hivyo kulilazimu Shirika la TANESCO kutumia mitambo yake inayotumia mafuta ambayo hata hivyo haikidhi mahitaji ya umeme ya Mkoa.
Profesa Muhongo aliliagiza shirika hilo kuhakikisha linaharakisha taratibu za kuunganisha mkoa wa Kagera kwenye umeme wa Gridi ya Taifa.
"TANESCO ni lazima muharakishe mipango ya kuunganisha mkoa huu kwenye gridi ya taifa ili kuwapatia wananchi huduma ya umeme wa uhakika," aliagiza.

Aidha, Profesa Muhongo aliiagiza TANESCO kuhakikisha mafuta kwa ajili ya kuendeshea mitambo hiyo yanakuwepo yakutosha kwa muda wote.
Alisema ifikapo mwaka 2025, Tanzania itaingia kwenye uchumi wa kati ambao utatokana na uwekezaji mkubwa kwenye viwanda ambavyo vitahitaji umeme wa kutosha na uhakika.

Mbali na hilo, Profesa Muhongo aliliagiza Shirika la Tanesco mara baada ya mkataba uliopo wa kuuziana umeme kati ya Tanzania na Uganda kuisha, wahakikishe wanaingia mkataba wa muda mfupi mfupi lengo likiwa ni kuepusha kuwa ndani ya mkataba wakati tayari mkoa huo utakua kwenye gridi ya taifa.
Akielezea hali ya umeme mkoani humo, Meneja wa Tanesco Kanda ya Ziwa, Mhandisi Amos Maganga alisema kwa sasa Tanzania inanunua umeme kwa gharama ya senti za Marekani 8.4 kwa kila unit.

Alisema Tanzania inao mkataba wa kununua umeme kutoka Uganda kiasi cha megawati 10 ambao unahudumia wilaya za Bukoba Mjini na Vijijini, Karagwe, Muleba na Misenyi.(P.T)

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kushoto) akimsikiliza Mhandisi Filbert Mlaki.

Waziri wa nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akikagua moja ya mtambo wa kuzalisha umeme wa Kituo cha Kibeta

Moja ya mtambo wa kuzalisha umeme katika kituo cha kufua umeme wa dharura cha Kibeta- Bukoba Mjini.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongella kabla ya kuanza ziara ya kukagua miundombinu ya umeme mkoani humo.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwa kazi gani kupunguza bei ya umeme
    Fyuuuuuuu
    Hata Tibaijuka anajulikana UN
    Anamajisifu waziri unaanasiasa si taaluma bora angekuwa katibu mkuu nampa pole katibu mkuu wake eti Muhongo anatamba yeye mtalaam duniani fyuuuuuuuuuuuu
    Mbona ulaya hatujamsika
    Tanzania ni Nyerere tu hakuna
    Tapeli
    Asante Kafulila tunazo data zake huku ughaibuni tutakupa
    Tena bora ya Tibaijuka mama wa watu pamoja na pesa za mboga 10 mil
    CCM

    ReplyDelete
    Replies
    1. umepanick
      kubwa jinga wewe huna hata cha maana ulichoongea nyie watu wa lowasa mkoje mnafikiri kwa makalio sijui
      fyuuuuuuuuuuuu
      hovyoooo
      na mtaisoma number tuu

      Delete
  2. Mtoa comment wa hapo juu mbona haieleweki ni kitu gani umekiandika au unachojaribu kuwaelewesha wasomaji yaani picha yenyewe siipati kabisa kweli kiswahili ni lugha ngumu sana

    ReplyDelete
  3. tatizo shule anakurupuka tuu apo juu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad