Profesa Lipumba, Lissu wapinga uteuzi wa Muhongo na Mwakyembe

Saa chache baada ya rais Magufuli kutangaza baraza lake la Mawaziri ambalo limekuwa baraza dogo kama alivyoahidi, aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) na mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu wamekosoa uteuzi wa Profesa Sospeter Muhongo na Dk. Harison Mwakyembe.

Dk. Mwakyembe alikuwa waziri wa Uchukuzi katika serikali ya awamu ya nne na hivi sasa ameteuliwa kuwa waziri wa Katiba na Sheria. Profesa Muhongo ambaye alijiuzulu kwa kashfa ya Escrow katika serikali ya awamu ya nne, amerudishwa katika wizara ya Nishati na Madini.

Profesa Lipumba amekosoa uteuzi wa profesa Muhongo kwa madai kuwa uteuzi wake umelitia doa baraza hilo.

“Kwa kitendo kama hiki, Rais Magufuli amejiwekea dosari kutokana na uteuzi huu. Maana yake ni kuwa katika kashfa ile Profesa Muhongo hakuwa na hatia,” Profesa Lipumba aliliambia gazeti la Mwananchi.

Profesa Lipumba aliongeza kuwa wananchi watapata ugumu kumuelewa Rais kutokana na ahadi zake kuwa atapambana na rushwa na ufisadi.

Naye Tundu Lissu aliliambia gazeti hilo kuwa uteuzi wa Dk. Harison Mwakyembe hakuwa sahihi kwa kuwa ndiye aliyekuwa waziri wa Uchukuzi na punde baada ya rais Magufuli kuingia ikulu, Mamlaka ya Bandari ikabainika kukumbwa na kashfa ya upotevu wa makontena.

“Juzi Rais Magufuli aliufumua uongozi wa Bandari ya Dar es Salaam kutokana na kashfa, miongoni mwa waziri waliokuwa wakisimamia sekta hiyo ni Dk. Harrison Mwakyembe, eti leo amemrudhisha kundini?” Lissu ananukuliwa.

Lissu aliongeza kuwa Muhongo pia hakufaa kuwa miongoni mwa mawaziri kwa kuwa alifukuzwa na Bunge kutokana na sakata la Escrow.

Hata hivyo, Profesa Lipumba alimpongeza rais kwa kutekeleza ahadi yake ya kuunda baraza dogo kwa lengo la kubana matumizi.
Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ujio wa lowasa ukawa hawakupinga ujio wa masha hawakupinga ujio wa kingunge hawakupinga
    ebu mwacheni muhongo apige kazi hii wizara aliipatia sana alifanya bei ya umeme kushuka na umeme ulikuwa haukatiki hovyo kipind yupo waziri
    ishu ya escrow haimuhusu ni chuki tuu
    ebu fanya yako lissu kwenye jimbo lako watu wanataka mabadiliko ya kweli sio ya kuzungusha mikono

    ReplyDelete
  2. Hapa inaonyesha wazi mkuu aliyepita ka cheza. Baada ya kushindwa kumteua Membe na kumrithisha uraisi, amemweka kusudi kuzimisha katiba ya wananchi ili vigogo wakuu wasipelekwe jela. Ni Membe aliyesababisha hasara kubwa bandarini akiwa waziri wa uchukuzi.Akipitisha macontainer ya wakuu kwa mida tofauti. Muhongo pia karudishwa ili mikataba waliyopeana kindugu, kiurafiki,kifamilia isifumuliwe. Kinana karudishwa kwani meli zilizohusika kubeba meno ya tembo, madawa ya kule ya zisi hunguzwe. Hii yote ni kulindana kunakoendelea ndani ya CCM ambako kumetimisa nchi na uchaguzi. Kusita kwa Magufuli kutangaza baraza jipya ni hawa mawaziri. Na wasikubalije hata. Ni Membe na Lowassa tena vitani kupitia raisi ya awamu iyopita bado vita inaendelea.
    Hapa Watanzania wanakejeliwa na kupitia raisi wa awamu ya nne. Bado yupo kazini kuliteketeza Taifa

    ReplyDelete
  3. Udhaifu wa Magufuli ndio huu.mchaps kazi asiyekuwa huru. Kwa maana hii anaendeshwa na genge lilokaa kikaoni la CCM badala ya kumtegemea Mungu.

    ReplyDelete
  4. Wakahug transformer

    ReplyDelete
  5. Muhongo ni mtaalamu wa nishati na madini ndio fani yake

    ReplyDelete
  6. Mtakoma mwaka huu. Msiyempenda karudi. Daima msema kweli mpenzi wa Mungu

    ReplyDelete
  7. hata hao wanaotetea wanajishaua ila wanajua kuwa magufuli kachemka kurudia makombo ya jk. hasa yale mafisadi papa kayarudisha tena, akili za kuambiwa changanya na zako. poleni watz kwa ujinga.

    ReplyDelete
  8. Nyie akina Lissu hebu pigeni kimya, kwanza hamumtambui JPJM kama Rais, hata nyinyi mlimpitisha Lowasa ambaye mlimtangaza dunia nzima kwamba ni FISADI PAPA. Fanyeni yenu, mwacheni TINGATINGA 'atingishe dunia'........... HAPA KAZI TU

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad