Rais John Magufuli, Majipu Yamekwisha? Ukimya wako Watia Shaka

Ulianza vizuri. Ulianza kwa mkwara imara hadi viongozi wakatamani wajiondoe wenyewe. Ukafanya ziara ya ghafla isiyo na hafla Wizara ya Fedha na Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Kama hiyo haitoshi,ukaunguruma Bungeni ukiahidi kutumbua majipu ya ufisadi kwa wale waliofaidi zaidi. Ukajielekeza TRA na Bandari. Pakatokea yaliyotokea. Baada ya hapo,ukimya umetawala.

Ukimya wako umetanguliwa na kikao cha Kamati Kuu ya CCM. Kulikoni? Au TeamLowassa imekwisha kule TRA na Bandarini na haipo kwingineko? Nauliza tu kiutaniutani!

By Mzee Tupatupa wa Lumumba(kwasasa Arusha)

Post a Comment

15 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nguvu ya soda hiyo
    Chezea kamati kuu ya CCM
    Ashambiwa asitumbuwe majipu
    Aanze na kuponya vidonda

    ReplyDelete
    Replies
    1. acha umbulula wako subili mwanamme afanye kazi

      Delete
    2. Ulikuwepo kwenye hiyo kamati kuu au MTABIRI??

      Delete
    3. Nilikuwepo team Lowassa iko kila kona

      Delete
  2. Hawajakukamata? We subiri, watakutia mkononi ndio utajua kama ni mkwara ama nene!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Miye nikamatwe kwani la magufuli allitoa Nani na Mimi ni Nani
      Uslite hapa
      Kila Leo ntaruka kwenda ninakokutaka mtakamatwa nyie pumba na vijidaaaaaaaaa
      Msoga na my team ngooooooooooo

      Delete
  3. Watu waache maneno ya kipuuzi, sasa kisa ameanza kufanya kazi kwa kasi mnataka kila siku iwe hivyo ama hamna vya kupost website mpaka muone tu matukio?
    Uraisi wake si miaka mitano ama?
    KWa hiyo kazi zote za miaka mitano azifanye ndani ya miezi miwili ama?
    Kikwete alikuwa ancheka tu, mwacheni Raisi wetu anajitambua, kwani aliyemuambia aanze kufatilia wakwepa kodi ni magazeti ama?

    ReplyDelete
  4. Ukiona kobe kainama ujuwe anatunga sheria au anatungiwa. .Ama hicho kikao cha CCM wamempa warning. .Kasi yake imekuwa hatari isije akatumbua majipu sugu Yaani (DONDA ndugu)..Hata mie hiyo nimeistukia..Tangu alivyorudisha mawaziri wa zamani alinivunja moyo ,nikajuwa huyu sio tena MagufulI aliye simama kama Magufuli..,mamlaka sasa yaanza kutoa mamlaka kwa wenye mamlaka. (Itakuwa rais jina tu si wakutoa mamlaka...wapo baadhi ya watu wameishikiria Tanzania mpaka kufa kwao..Rais Zidi kumuongoa Mungu wako usirubuniwe na waroho wa jasho la watanzania. .

    ReplyDelete
  5. SUBIRINI TU MOTO UTAWAKA HIVI KARIBUNI MAGUFULI SIO MCHEZO HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
  6. Lakini Magufuli bomba

    ReplyDelete
  7. Na kama unafikiri majipu yamekwisha acha kulipa kodi uone kama mkojo wako haukutokea matakoni, mbwa mkubwa wewe......

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huna adabu mitusi itakusaidia nini kwani magufuli mumeo

      Delete
    2. Mume wa mama ako na baba ako

      Delete
    3. Watanzania tunatisha, nadhani ni mapema mno kuona raising hatumbui majipu, tumpe nafasi na kumsupport.

      Delete
  8. TUMEKWISHA IONA.HII NDIYO STAILI YA UTAWALA[KIASHIRIA YA MHESHIMIWA MAGUFULI]AMEWARUDISHA MAWAZIRI WA KIKWETE 13.NI UAMUZI WAKE,SISI TUMESHUHUDIA.WALIOHARIBU VIBAYA KAWARUDISHA,TUSEME NINI?HATUONI DALILI AU MWELEKEO ILIYEPO KANDILI.TUSUBIRI.WANANCHI TULISHAWISHIKA NA KUMPIGIA KURA KUTOKANA NA AHADI ZAKE YEYE NA MGOMBEA MWENZA.NI NYINGI MNO,NYINGI SANA.TULIAHIDIWA CHA KWANZA KUSHUSHWA SANA BEI YA VIFAA VYA UJENZI YAANI CEMENT,MABATI,NONDO,MBAO,MISUMARI,VIGAE NK.[ORODHA YAKE YAPATA ITEMS 56]AMBAZO TUZIITE ESSENTIALS.TUNAANGALIA NA KUSUBIRI KWA HAMU.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad