Rais Magufuli Atoa Namba yake Ya Simu Kwa Wavuvi.....Awaahidi Mambo Matatu.

Rais John Magufuli leo ameungana na wananchi katika kufanya usafi ambapo akiwa katika eneo la Feri jijini Dar es Salaam, ameweza kuzungumza moja kwa moja na wavuvi wadogo.

Baada ya kusikiliza kwa makini kero zinazowakabili wavuvi hao wadogo akiwa amekaa ndani ya kifaa duni cha kufanyia uvuvi maarufu kama ‘mtumbwi’ usio na mashine, rais Magufuli aliwaahidi wavuvi hao kuzitatua kero hizo.

Kati ya mambo matatu aliyoahidi kuyafanyia kazi kwa haraka ni pamoja na kuondoa masharti kuwa kuwa na ‘Fire Extinguisher’ ambapo alieleza kuwa sharti hilo halina mashiko kwa wavuvi hao wadogo wasio na mashine.

“Kwanza maji yenyewe tu ni ‘fire extinguisher’, si moto ukianza unaingia ndani ya maji,” alisema Dk. Magufuli.

Kadhalika, rais aliahidi kuwasaidia wavuvi hao kwa masharti ya kuunda umoja wao ambao utakuwa na viongozi waadilifu wanaofanya kazi kwa maslahi ya wavuvi hao na sio maslahi ya ‘wakubwa’. Alieleza kuwa atalifanyia kazi suala la wavuvi hao kukopesheka na kuwasaidia kuwa na vifaa bora.

Aliongeza kuwa atahakikisha anafuta ushuru kwa wavuvi hao wadogo ili kuwaondolea kero na mzigo wa gharama.

Pia, alisema atahakikisha anaanza kuwasaidia kadiri awezavyo wavuvi wa eneo la Feri kwa kuwa ni majirani zake.
“Katika kudhihirisha ujirani mwema, hayo matatizo nitayabeba.”

Hata hivyo, rais aliwataka wavuvi hao kuhakikisha hawajihusishi na uvuvi haramu wa kutumia sumu na mabomu.

Katika hali ambayo wengi hawakuitegemea, rais Magufuli alimpa mmoja kati ya wawakilishi wa wavuvi hao namba yake ya simu na yeye akachukua namba ya watu wawili kati yao.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya zoezi hilo, Dk. Magufuli aliwashukuru watanzania wote kwa ujumla kwa kuitikia wito wake wa kufanya usafi huku akieleza kuwa hili linapaswa kuwa zoezi endelevu kwani uchafu hauwezi kuisha kwa kufanya usafi mara moja kwa mwaka.

Nafasi za Kazi
Bonyeza www.ajirayako.com

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwakweli huyu Magufuli ni rais wa pili wa Tanzania toka kwa nyelele na sio wa tano kama wanavosema wengine wengi.

    ReplyDelete
  2. safi sana magufuli
    Mungu azidi kukubariki
    tumekuelewa watanzania

    ReplyDelete
  3. Hongera WA kukaya
    Wasaidie watani wetu
    Futa futa uongozi wa soko la ferry

    ReplyDelete
  4. nenda ikulu utapewa

    ReplyDelete
  5. Mdau mwanzo hapo juu uliendika"NYELELE"Angekuwa bado yupo hai angekushtaki mahakamani kwa kulikosea kuliandika jina lake aliitwa"NYERERE"Is that clear to you now?

    ReplyDelete
  6. Kweli naamini ni jinsi gani elimu imeshuka hapa Tanzania kwa kiwango cha kusikitisha sana pindi pale nisomapo comments za wadau humu mitandaoni wengi wao hawajui/hawawezi kabisa kukiandika kiswahili fasaha wanababaisha tu ili mradi bora liende kwa mfano sehemu ya kuandika herufi"R"mtu anaandika"L"na makosa mengi sana ya kipuuzi rudini tena kwenye shule za ngumbaru(wengi wenu mlikuwa bado hamjazaliwa"ngumbaru zilikuwa ni shule za watu wazima kuwawezesha kujua kusoma na kuandika enzi za utawala wa Nyerere mpo hapo?)ili mkajifunze tena kiswahili fasaha

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa kweli kiswahili kimeharibiwa sana hadi inasikitisha, kwenye hakuna mtu anaandika "akuna", hela m tu anasema "ela" afadhali mtu anaandika "hafadhali" mi nashindwa kuelewa hivi waalimu ndio wanafundisha hivyo au nini jamani? Baraza la Kiswahili liko wapi kuokoa kizazi hiki?

      Delete
  7. Aah android hazijui kiswahili jamani hahaha

    Nyerere angekuwa hai Ile bakora ingempitia mdau hapo juu.

    Magufuli is our miracle president Mungu amsimamie sana. Amen

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad