Rais Magufuli amempongeza Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Dkt. Philip Mpango kwa kazi nzuri ya ukusanyaji wa mapato inayofanywa na mamlaka hiyo ambayo imeongeza ukusanyaji wa Mapato na kwa mara ya kwanza mwezi huu ukusanyaji wa mapato hayo unatarajiwa kuwa zaidi ya shilingi Trilioni 1 na Bilioni 300
Kutokana na mafanikio hayo amewahakikishia watanzania kuwa fedha kwa ajili ya kutimiza ahadi ya kutoa elimu bure kwa shule za msingi na sekondari ambazo ni kiasi cha shilingi Bilioni 131 zitatengwa mwezi huu na kupelekwa moja kwa moja katika shule husika.
Amesema wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa watapatiwa nakala za taarifa za ugawaji wa fedha hizo na kuonya kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayethubutu kuzitumia vibaya.
Dkt. Magufuli ameongeza kuwa fedha hizo ambazo ni pamoja na fedha za maendeleo, fedha za mitihani na fedha vifaa vya kufundishia zitaanza kutumwa kila mwezi kuanzia mwezi huu wa kumi na mbili.
Nafasi za Kazi
Bofya www.ajirayako.com
Fukuza kwanza hawa wakuu wa mikoa Na wilaya waliopewa kwa hisani kwani uozo wote unaanzia kwao
ReplyDeleteKwani siku hizi wamegeuka mapolisi kutia watu ndani tena wana talaaluma
Wanawavunja mioyo kabisa watendaji
Uozo Na ufisadi Upo mambo ya nje
ReplyDeleteWatumishi wakimaliza mikataba wanarudi nyumbani
Lakini nyumba zao zinaendelea kulipwa eti kisa hakuna pesa ya kusafirisha mizigo
Lakini wageni au rafiki WA maofisa wa balozi hufikia nyumba hizi
Nyumba zingine zimelipiwa hadi miaka 4
Ukitaka ushahidi tunao tunakaa ughaibuni na tunawajuwa wafanya Dili hizi
Fukuza wote hawa wengi wao ni watoto WA vigogo Kila balozi
Wanahama nchi Kila nchi
Wao ndo wafanya dili na vigogo wa serikali hufikia nyumba hizi hawafikii mahotelini
Saaafi saaana fichua uozo.....
DeleteNa nyumba inalipiwa dola 3000
ReplyDeleteLakini wizara haina pesa kusafirisha mizigo kwa miaka 4
Yale Yale ya TRA kutoa mashine kwa wauza bidhaaa
Shame kikwete
Dola 3000 kwa mwezi
ReplyDelete