Rais Magufuli Awahakikishia Watanzania Kutimiza Ahadi Yake Ya Elimu Bure.......Aipongeza TRA kukusanya Trilioni 1.3 Ndani Ya Mwezi Mmoja,Atoa ONYO kwa Wakuu Wa Mikoa

Rais Magufuli amempongeza Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Dkt. Philip Mpango kwa kazi nzuri ya ukusanyaji wa mapato inayofanywa na mamlaka hiyo ambayo imeongeza ukusanyaji wa Mapato na kwa mara ya kwanza mwezi huu ukusanyaji wa mapato hayo unatarajiwa kuwa zaidi ya shilingi Trilioni 1 na Bilioni 300

Kutokana na mafanikio hayo amewahakikishia watanzania kuwa fedha kwa ajili ya kutimiza ahadi ya kutoa elimu bure kwa shule za msingi na sekondari ambazo ni kiasi cha shilingi Bilioni 131 zitatengwa mwezi huu na kupelekwa moja kwa moja katika shule husika.

Amesema wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa watapatiwa nakala za taarifa za ugawaji wa fedha hizo na kuonya kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayethubutu kuzitumia vibaya.

Dkt. Magufuli ameongeza kuwa fedha hizo ambazo ni pamoja na fedha za maendeleo, fedha za mitihani na fedha vifaa vya kufundishia zitaanza kutumwa kila mwezi kuanzia mwezi huu wa kumi na mbili.

Nafasi za Kazi 

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Fukuza kwanza hawa wakuu wa mikoa Na wilaya waliopewa kwa hisani kwani uozo wote unaanzia kwao
    Kwani siku hizi wamegeuka mapolisi kutia watu ndani tena wana talaaluma
    Wanawavunja mioyo kabisa watendaji

    ReplyDelete
  2. Uozo Na ufisadi Upo mambo ya nje
    Watumishi wakimaliza mikataba wanarudi nyumbani
    Lakini nyumba zao zinaendelea kulipwa eti kisa hakuna pesa ya kusafirisha mizigo
    Lakini wageni au rafiki WA maofisa wa balozi hufikia nyumba hizi
    Nyumba zingine zimelipiwa hadi miaka 4
    Ukitaka ushahidi tunao tunakaa ughaibuni na tunawajuwa wafanya Dili hizi
    Fukuza wote hawa wengi wao ni watoto WA vigogo Kila balozi
    Wanahama nchi Kila nchi
    Wao ndo wafanya dili na vigogo wa serikali hufikia nyumba hizi hawafikii mahotelini

    ReplyDelete
    Replies
    1. Saaafi saaana fichua uozo.....

      Delete
  3. Na nyumba inalipiwa dola 3000
    Lakini wizara haina pesa kusafirisha mizigo kwa miaka 4
    Yale Yale ya TRA kutoa mashine kwa wauza bidhaaa
    Shame kikwete

    ReplyDelete
  4. Dola 3000 kwa mwezi

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad