Sakata la TBC Kurusha Harusi Live: Mtaalam wa Habari na Aliyefanya Kazi Hapo Afanunua Kama ni Kosa!

Serikali imeliagiza shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kutoa maelezo ya kina baada ya kurusha matangazo ya moja kwa moja sherehe za harusi kwa zaidi ya saa mbili, jambo lilihojiwa na wananchi maeneo mbalimbali hasa katika mitandao ya jamii.

Serikali imechukua hatua hiyo baada ya kupata malalamiko mengi kwa kile kilichokuwa kinarushwa na Kituo cha Televisheni cha TBC1 cha shirika hilo linaloendeshwa kwa ruzuku kutoka Serikalini.

Agizo hilo limetolewa jana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ambaye alibainisha kuwa amepokea simu za watu wengi waliokuwa wanahoji juu ya kipindi hicho, hivyo kulazimika kuchukua hatua mara moja za kutaka maelezo kutoka kwa watendaji wa shirika hilo.

Chini ni maelezo ya mtaalam wa habari na aliyefanya kazi hapo:

Wadau, kwanza naomba ku declare interest, kuwa sikubahatika kuiona hiyo live ya harusi binafsi ya mtu!. Pili mimi ni mdau wa broadcast journalism, na niliwahi kufanya kazi TBC enzi zile ikiitwa TVT, ila hapa sichangii kama an authority by as an experienced broadcast journalist!

Naomba nitofautiane na wengi, kuwa TBC inaweza kuonyesha live ya kipindi chochote ambacho kinaonyeshwaga kikiwa recorded, hii ina maana kama TBC wanarusha kipindi cha Chereko, kikionyesha sherehe binafsi za watu, then mtu akifika bei, Chereko inaweza kwenda live kwenye event yoyote, iwe ni harusi, send off, kitchen party, ubarikio, au hata birthday ya mtu, provided ili live itatumia muda ule ule wa recored program, na kama itabidi ku extend time, isile muda wa more serious na relevant programs simply because mtu ana fedha za kulipia!

TBC nayo japo ni kituo cha TV kama vilivyo vituo vingine vyote vya TV, nayo inayo haki ya kufanya biashara, kama TV nyingine zote zinazovyofanya biashaa, na ina kipindi cha Chereko kinachoonyesha harusi za watu, then kama mtu ana pesa kulipia, then why TBC ikatae pesa?!, lakini suala la kurusha matangazo ya live, it is not about money on who can pay, but the contents and national interests, nadhani TBC wangeirusha hiyo live muda ule ule wa Chereko na baada ya hapo vipindi vingine vikaendelea kama kawaida, sidhani kama kungekuwa na any basis ya malalamiko, kwa sababu live social events za public figures, prominent people na super stars zinafanyika kwenye tv duniani kote japo not on public TV.

Dr. Buberwa nimefanya naye programs, hana tofauti sana na Renatus Mkinga, au Mchungaji Mtikila (RIP), kuhusiana na soundness of the state of their minds!, hivyo kitendo tuu cha mtu kulipia live ya harusi yake alone, kilitosha ku sound alarm kuhusu tuning a pivate function into a state function, mimi ndio ningekuwa producer, ningekuwa very careful to make sure live inahusisha kuonyesha events tuu na kamwe nisingithubutu kurusha live kitu chochote atakachoongea Buberwa.

Mwisho, hili la TV ya taifa kufanya biashara linahitaji mjadala wa kujitegemea, BBC World Service, haifanyi biashaa, na haipokei tangozo lolote la mtu yoyote zaidi ya public announcements, lakini iko funded 100% na public, mtu yoyote ukiisha kanyaga tuu ardhi ya UK, unailipia BBC utake usitake!, na sisi tufike mahali, TBC yetu iwe funded 100% ili isihitaji sentano ya mtu, na kugawa majukumu into diferent channels say TBC 1 iwe ni nationa interest, TBC 2 comercial, ifanya biashara, TBC 3, elimu, TBC 4, Afya, TBC 5 kilimo, uvuvi na ufugaji, TBC 6 watoto, TBC 7 michezo, TBC 8 miziki etc, etc.
Pasco
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jamaaani nakuombeni wadau muitizame kwa jicho la hurume ZBC maana imeoza kabisa, muda mwingi ukifungua utakutwa 'kasida za harusi hizo hizo kila siku zinajirudia au Mawaidha ya sheikh Mmoja huyo huyo kila siku anarudiwa yaaani ukweli inaendeshwa zaidi kisiasa.
    ZBC-2 nako ndio uozo kabisaaaa hakuna vipindi vipya wala mtazamo mpya kila siku vipindi vyake vinajirudia ni aibu haswa.

    Jambo la kushangaza katika siku za uchaguzi nilitegemea nikifungua ZBC nitapata habari za uchaguzi wa Zanzibar lakini kutwaa kasida za harusii basi alau zingekuwa mara moja kwa wiki lakini kila siku si chini ya mara 3 au nne kwa kasida moja waakimaliza taarifa ya habari kasida za kiIndonesia wakimaliza kasida Kiswahili.
    Nataka munielewe si kama nachukia kasida ila kitu chochote kikirudiwa rudiwa mwisho kinakinaisha.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni udini tu ndio unakusumbua, huna lolote

      Delete
  2. Wewe uliyeandika hii mada umezidi uhaya, yaani ina maana huwezi kuandika habari nzima kwa kiswahili mpaka uchanganye na kingereza??umenibore sana, na huyo mwenye harusi ni kabila hiyo hiyo mnapenda sanaa show off, hivi mtabadilika lini? ameona kwenye chereko haitoshi anahitaji kitu matawi ya juu.. kha hahahaaa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad