Serikali Yawapiga STOP Akina Lowassa Na Wenzake Kufanya Mikutano ya Hadhara

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema wanasiasa walioshindwa kwenye Uchaguzi Mkuu hawaruhusiwi kuitisha mikutano ya hadhara kwa ajili ya kuwashukuru wananchi kwa kuwa wanaweza kuvuruga shughuli za maendeleo.

Waziri Mkuu alisema hayo wakati akilishukuru Jeshi la Polisi wilayani Ruangwa kwa kufanya kazi ya kusimamia Uchaguzi Mkuu uliomalizika Oktoba 25 kwa CCM kushinda kiti cha urais na kuzoa takriban viti 180 vya ubunge.

Naendelea kuwashukuru kwa mchango wenu mkubwa kiulinzi, lakini pia usimamizi wa zoezi zima la uchaguzi na hatimaye hivi sasa watu wameshapatikana,” alisema Waziri Majaliwa nje ya ofisi za jeshi hilo.

Na tumesema, siasa tumeshazimaliza. Sasa tunataka tufanye kazi za maendeleo. Hatuhitaji tena watu kuja kutuvuruga. Mikutano ya shukrani itafanywa na wale tu walioshinda kwenye maeneo yao. Wengine watulie.

Vyama sasa viache wale tu waliochaguliwa kwenye maeneo yao washukuru, wengine hawa watakuja kuleta maneno ambayo yatatuvuruga. Mimi naamini mko imara.”

Wakati Waziri Majaliwa akisema hayo, tayari Edward Lowassa, aliyekuwa mgombea urais wa Chadema na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), alishapanga kuanza ziara ya kuzunguka nchi nzima kwa lengo la kuwashukuru wananchi waliompigia kura.

Hata hivyo, ilipofika siku ya kuanza ziara hiyo, Chadema ilitangaza kuwa imeahirisha hadi itakapotangazwa tena, ikiweka bayana kuwa uamuzi huo hautokani na vitisho vya makamanda wa polisi wa mikoa.

Awali, amri ya kuzuia mikutano ya kisiasa ilikuwa ikitolewa kwenye mikoa na baadhi ya makamanda wa polisi, lakini tamko hilo la juzi la Waziri Majaliwa linatia msumari marufuku hiyo ya kuendesha shughuli za kisiasa kwa hoja ya kushukuru wananchi.

Lowassa, ambaye alihamia Chadema siku chache baada ya kukatwa jina lake na CCM mwezi Julai, aliweka rekodi ya kuwa mgombea wa upinzani aliyepata kura nyingi baada ya kupigiwa kura na watu milioni 6.07 ikiwa ni asilimia 39.9, huku mshindi akipata kura milioni 8.88 sawa na asilimia 58.46.

Tamko hilo la Waziri Majaliwa tayari limeanza kupingwa sehemu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kwenye mitandao ya jamii na vyama vya siasa kutoa matamko.

Hii ni kauli ya ajabu kutolewa na mtu anayesimamia utendaji wa shughuli za kila siku za Serikali inayotaka kuwaaminisha (wananchi) kuwa itakuwa tofauti na serikali nyingine zilizopita za CCM,” inasema Chadema katika tamko lake la jana jioni kujibu kauli ya Waziri Majaliwa.

Kama wao (CCM) ndiyo walioshinda kama ambavyo Waziri Mkuu Majaliwa amesema na kwamba wanaendelea kutekeleza wajibu waliokabidhiwa na wananchi, tunahoji hofu yao nini hasa wakiona au wakisikia Chadema wanapanga kwenda kuongea na wananchi? Wanaogopa nini?”

Taarifa hiyo iliyotolewa na Idara ya Mawasiliano, Chadema imesema kuwa waziri Majaliwa ametoa tamko hilo siku chache baada ya kufanya mkutano mjini Lindi uliowabagua wananchi kwa itikadi zao kwa kutoa nafasi kwa chama kimoja cha siasa ambacho ni CCM kuhutubia na kufanya siasa.

Matukio haya yanaanza kumdhihirisha Waziri Mkuu Majaliwa ni kiongozi mwenye uelekeo wa namna gani hivyo kuanza kuifunua Serikali ya Rais John Magufuli chini ya CCM kwa miaka mitano ijayo itawapeleka wapi Watanzania,” inaeleza taarifa hiyo.

Ni dalili za wazi za watu waliolewa madaraka na kuchoka kuwa viongozi na sasa wanataka kuwa watawala wenye kudhani kuwa fikra zao ndizo zinazongoza nchi badala ya misingi ya inayokubalika miongoni mwa jamii nzima kupitia Katiba, Sheria, Kanuni na taratibu mbalimbali.”

Naye makamu mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdallah Safari alisema uamuzi huo ni kinyume na Katiba na Sheria ya Vyama vya Siasa na kwamba Serikali inazuia wapinzani kufanya mikutano ya kushukuru wananchi kwa kuwa inajua watatoa ushahidi wa jinsi kura zilivyoibwa.

Wanatuzuia kwa sababu wanajua tutakwenda kutoa ushahidi wa jinsi CCM ilivyoiba kura za urais na ubunge,” alisema Profesa Safari.

Kiongozi anaweza kuzuia mkusanyiko iwapo tu nchi itakuwa katika hali ya hatari. Jambo hili hata Rais hawezi kulizua kienyejienyeji tu,” alisema Profesa Safari ambaye kitaaluma ni mwanasheria.

Alisema Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 imeeleza wazi majukumu ya vyama vya siasa, kuwa ni pamoja na kufanya mikutano na maandamano.

Pamoja na tamko la Waziri Mkuu kumruhusu kufanya mikutano kutokana na ukweli kuwa alishinda uchaguzi wa ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe alizungumzia marufuku hiyo kuwa ni kauli ya kisiasa isiyo na mantiki.

Mikutano inaratibiwa na Sheria ya Vyama vya Siasa. Hii kauli ya Majaliwa naona kama ilikuwa ya kisiasa zaidi. Jeshi la polisi ndilo lenye jukumu la kuzuia mikutano na litafanya hivyo kama kutakuwa na hali ya hatari na si vinginevyo,” alisema Zitto.

Mwanasheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia alimtaka Waziri Mkuu kujikita katika uwajibikaji badala ya kuingilia vyama vingine.

Sheria hairuhusu mtu yeyote kuzuia mikutano ya kisiasa isipokuwa kama kuna tishio la vita,” alisema Sungusia.

Kuruhusu baadhi ya watu kufanya mikutano na wengine kuwazuia ni kuwanyima haki watu.”  

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wewe kasim nenda salon kwanza katengeneze kichwa chako
    Waziri mkuu mzima unatia mkorogo kupaka rangi kichwani
    Unaficha nini wewe
    Mvi si ugonjwa

    ReplyDelete
  2. Waziri mkuu kasema wale walioshinda ndo waende kuwashukuru wananchi walio wachagua kwenye maeneo yao. Hivi walioshinda ni CCM tu? Mbona mnapenda kugeuza maneno jamani? Upinzani wameshinda wabunge na madiwani kibao, kuna mahali popote waziri mkuu kasema washindi wa CCM tu ndo waende kuwashukuru wananchi? Acheni siasa za chuki jamani. Hiyo hela ya kuzunguuka nchi nzima si mzipeleke kwenye kusaidia maendeleo ya wananchi sehemu mbalimbali nchini. Siasa za sifa zimepitwa na wakati tunataka maendeleo sasa

    ReplyDelete
  3. izo pesa za ukawa popote pale zinapotoka kutumika kuzunguka nchi nzima kwanini msizielekeze kwenye maendeleo majimboni kwenu acheni uboya siasa zishapita sasa ni muda wa kazi maswala ya kukusanyika bila mpango wowote eti shukrani kwann usiite press conference ushukuru watanzania iv hamchoki kuzunguka tanzania nzima? sasa ni muda wa mabadiiko ya vitendo sio mikono zungusha tena
    lowasa uko chadema amekuwa kama mungu mtu anaharibu chama kwa pesa zake mnaboa ukawa mfyuuuuuuuuuuuu safi sana majaliwa uzi ule ule lazima waheshimu maamuzi ya chama tawala sio kuleta dharau na hata wangekuwa hao ndo watawala lazima wangekuwa na misimao yao
    kuzunguka nchi nzima mtujazie foleni tuu na uchafu

    ReplyDelete
  4. Uhuruu uko wapi.. ccmini mtakuwa na usomi safi, sheria safi, na juacha ubabe. Hata mkitimiswa bado mnaonekana mna uduni miamili. Shida nini.ini mtatumia imu zenu na kuheshimu sheria za nchi ili nchi iwe na amani na ipige maendeo mbele.Tatizoenu nynyi viongozi ni nini?

    ReplyDelete
  5. Uhuruu uko wapi.. ccmini mtakuwa na usomi safi, sheria safi, na juacha ubabe. Hata mkitimiswa bado mnaonekana mna uduni miamili. Shida nini.ini mtatumia imu zenu na kuheshimu sheria za nchi ili nchi iwe na amani na ipige maendeo mbele.Tatizoenu nynyi viongozi ni nini?

    ReplyDelete
  6. Uhuruu uko wapi.. ccmini mtakuwa na usomi safi, sheria safi, na juacha ubabe. Hata mkitimiswa bado mnaonekana mna uduni miamili. Shida nini.ini mtatumia imu zenu na kuheshimu sheria za nchi ili nchi iwe na amani na ipige maendeo mbele.Tatizoenu nynyi viongozi ni nini?

    ReplyDelete
  7. Tunashukuru.Tangu Mheshimiwa Rais Magufuli kuapishwa mwishoni mwa mwezi Novemba 2015 mpaka leo hii jumamosi tarehe 26 december 2015 tumekwisha mpima na kumjua ni kiongozi wa aina ipi,anaijuaje siasa[alikwishasema mara kadhaa kwamba yeye ni mtendaji na si mwana siasa]ana mwelekeo upi kuhusu kuboresha maisha yetu sisi wananchi na anajipanga vipi kuhusu ahadi alizozitoa wakati wa mikutano yake ya kampeni yeye na mgombea mwenza wake,ahadi ambazo tuseme zitaweza kumvusha 2020 au sisi wananchi kuamua kumchagua kiongozi mwingine.HUO NDIO UKWELI.TUNAYAHITAJI MAISHA BORA YENYE UNAFUU NA MATUMAINI,FULL STOP.TUNATAKA MAENDELEO YA KUYAONA KAYA KWA KAYA,KITONGOJI KWA KITONGOJI,KIJIJI KWA KIJIJI,KATA KWA KATA,WILAYA KWA WILAYA,MKOA KWA MKOA NA TAIFA KAMA TANZANIA KWA MINGANISHO NA MATAIFA JIRANI HUSUSANI KENYA,UGANDA NA RWANDA.HIKI NDICHO KIPIMO CHETU.Lakini sasa kwa kauli-ashiria ya waziri mkuu kassim majaliwa[sina uhakika kama ni yake au katumwa]inaonyesha wazi kwamba hii miaka mitano ijayo itakua kisiasa ni ya ukandamizaji mkubwa kwa nia ya kuidhoofisha demokrasi na kujaribu kuuangamiza upinzani.chuki tumeshaziona,na majaliwa keshatupa ishara kwamba yeye ni nani kwa mujibu wa heshima ya siasa,demokrasi na kiashiria cha UDIKTETA MKUBWA UNAOPIGA HODI.TANZANIA HAINA DEMOKRASIA HATA KWA ASILIMIA 20.SUBIRI UJIONEE.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad