Shamsa Ford: Sitaki Tena Kutoka Kimapenzi na Mastaa...Kisa na Mkasa?

Msanii wa filamu na mama wa mtoto mmoja, Shamsa Ford amesema amekoma kutoka kimapenzi na watu maarufu.

Muigizaji huyo ambaye miezi michache iliyopita alikiri kutoka kimapenzi na rapa Nay wa Mitego, ameiambia Bongo5 kuwa sasa hivi amepata mpenzi mpya ambaye atamweka wazi siku ya harusi yake.

“Mimi ni mwanamke mzuri nakosaje mwanaume? Nimetimia kila idara, nina mchumba ambaye tunapendana Mungu akijalia kiukweli natamani awe mume wangu,” amesema.
“Nimeshatangaza kabisa mastaa sitaki nimekoma, nimekoma kutoka kimapenzi na mastaa au kumtangaza mpenzi wangu kwenye mitandao. Mpenzi wangu watamjua siku ya harusi yangu. Unajua mastaa wana mambo mengi sana na kuendelea nao ni kupoteza muda tu” amesisitiza Shamsa Ford.

Hata hivyo Shamsa hakutaka kuzungumzia sababu ya kuachana na Nay.

Bongo5

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hata huyo uliyenaye sasa sijui ndo unamwita mchumba anakudanganya akimaliza kukumwagia matakataka yake anasepa zake nani aoe makombo ya nay mchafu aliyekuachia gonjwa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad