Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Latoa Kauli yake Kuhusu Shutuma za Kurusha Sherehe ya Harusi Laivu Kwa Masaa Mawili

Shirika la Utangazaji TANZANIA TBC limesema halijakiuka sheria za utangazaji kufuatia kipindi  maalumu cha chareko kilichorushwa na kituo hiki Desemba 19 siku ya jumamosi na kuwa kilichofanyika ni ubunifu wa vipindi.

Akizungumzia suala hilo Mkurugenzi Mkuu wa TBC, CLEMENT MSHANA amesema mteja wa kipindi hicho alitaka harusi yake irushwe moja kwa moja ambapo pia alipewa maelekezo ya kuzingatia wakati kipindi kitakapokuwa kikirushwa.

MSHANA amesema TBC ipo tayari kupokea maoni mbalimbali ya watazamaji wake ili kuboresha utendaji kazi wa chombo hicho, ambapo amewataka watazamaji kuendelea Kutazama TBC

Hii inakuja kufuatia hivi kitendo cha shirika hilo la umma kuamua kurusha ‘live’ harusi,kitu ambacho kililalamikiwa na wadau wengi hususani watazamaji wa kituo hicho,hali iliyompelekea Waziri wa Habari,sanaa na michezo Nnape Nnauye kumtaka Mkurugenzi huyo kujieleza ni kwa nini chombo hicho cha umma kinadiriki kufanya mambo hayo
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad