Sijaridhika Wala Kukubaliana na Utumbuaji wa Majipu wa Huyu Mheshimiwa Magufuli Kutokana na Haya

Sijaridhika wala kukubaliana na utumbuaji wa majipu wa huyu Mheshimiwa Magufuli, ambaye ni Rais wa Jamhuri yetu ya Muungano. 

Jambo la kwanza alilonikosesha nisimwamini kwa asilimia kubwa niusanii namna alivyokwepesha kashfa ya watu binafsi waliojimilikisha UDA na kuikosesha serikali mapato kwa kukwepa kodi. Suala la UDA limefukiwafukiwa hadi sasa linaonekana kutopewa uzito stahiki.

Uteuzi wa baraza la mawaziri umedhihirisha hana jipya zaidi ya kuwanyanyapalia dagaa huku wahusika wakuu wa kashfa bandarini, Escrow na TRA waliokuwa mawaziri na makatibu wakuu wa serikali ya Kikwete akiwatunukia uwaziri tena na kuendelea Ukatibu Mkuu licha ya kashfa nzito zilizoibuliwa na bunge hadi kuachia ngazi.

Kushindwa kushughulikia mgogoro wa Uchaguzi Mkuu Zanzibar dalili tosha Rais Magufuli kadiri ya msimamo wa CCM hana ubavu kwa chama chake, bali kukipigia magoti tu. Hana nguvu alina nayo kikatiba ila kutii matakwa ya chama chake.

Dhahiri alichoanza Rais Magufuli ni nguvu za soda, hatimaye yatakayojilia ni kukata tamaa na kuendelea na mazoea bora liende muhula uishe.

Source:Jamii Forums

Nafasi za kazi
Bonyeza =>www.ajirayako.com

Post a Comment

17 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mfyuuuuu!!! Umetumwa???? Huyo alokutuma inaelekea bado hajakulipa, haya nenda kamwambie akulipe kwanza, pengine akili itakukaa sawa......hebu mwacheni JPJM afanye ATAKALO.......upo?? Kama ni nguvu ya soda, ya togwa, ya uji, utasubiri sana hiyo nguvu iishe, litakuchwea.....HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
  2. Ukubaliane nae ama usikubaliane nae, lakini ndani ya siku 7 ameliingizia taifa shilling BILION 10!!! Hilo la Zanzibar watalimaliza wazanzibari wenyewe, hebu usimchoshe mkuu wetu....

    ReplyDelete
  3. WEWE ENDELEA KUCHONGA MCHANA, USIKU KALALE....HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
  4. naunga mkono hoja,,... hakuna jipya..... kuna ambayo anayafumbia macho.

    ReplyDelete
    Replies
    1. mbona yeye alimfumbia macho Lowasa akataka kumpatia urais mkaona ni sawa tu.

      Delete
  5. Mtoa mada huna jipya kashfa ya uda na tra na bandari vp vya muhimu zaidi? Maana uda n kwa ajili ta dar pekee but tra na bandari ni issue ya tz nzima ,sasa aache kuanza vitu vya muhimu vya tz nzima aanze na kero ya dar pekee, idiot !

    ReplyDelete
  6. Inaonekana aliyekutuma haya maneno yako ameshakufa.sasa ni hivi hapa kazi tu.

    ReplyDelete
  7. Hapa kazi tu endeleeni na maneno yenu ya kwenye khanga.na. Mtaisoma no.

    ReplyDelete
  8. Roma haikujengwa kwa siku moja! Mtu mwerevu hutatua masuala kwa utaratibu unaoleta tija. Madudu ni mengi, uozo ni mkubwa.... Rais wetu (chaguo la Mungu) ameanza kuyashughulikia vizuri sana! Tumtakie heri ili aendelee kwa staili na kasi hiyo hiyo. Viva JPM

    ReplyDelete
  9. tena hakuna jipyyaa hata moja huezi kueka mawaziri waliokula nchi na wanafahamika kua n majambazi wa kula serikaeri maguu anapelekwaa hana mpyaa sasa asubiri kudharirika

    ReplyDelete
    Replies
    1. MCHAWI MPE MTOTO AKULELEE, HAPA KAZI TU.

      Delete
  10. ni kweli kabisa hatokuwa na nguvu zaidi ilivyotarajiwa kushindwa kuwathibiti watoto wa vigogo na mgogoro wa Zanzibar na Zanzibar imo kwenye muungano hivyo ana wajibu wa kulishughulikia ila hana ubavu, then kwa baraza la kina watukanifu ni mtihani mtupu!

    ReplyDelete
  11. mtihani mtupu serikali inaendeshwa zaidi kichama kwa wale wenye mtazamo wa mbali

    ReplyDelete
  12. hawezi kufanya chochote lazima kapigwa stop mabwana wastaafu hao

    ReplyDelete
  13. Rais ameanza kazi vrz sana,anayeleta maneno maneno kashazoea majungu,ila kwa sasa amechemsha hatuna mda wa kuyapa nafasi Majungu,HAPA NI KAZI TU.

    ReplyDelete
  14. Siamini kama ni kweli kama kila anachofanya magufuri kinahitaji kupongezwa, ni vizuri kumpongeza anapostahili na kumkosoa anapokosea. Wapo baadhi ya wadau kazi yao ndani ya miaka mitano itakuaa kusifia tuuuuu napata shida na uwezo wao wakufikili. Raisi anapokosolewa anapata nafasi ya kujirekebisha na kufanya vizuri zaidi. Mfano kwa upande wangu kwa kuwa TRA ambayo inasimamiwa na wizara ya fedha ilikuwa na shida sana ya kufuatilia ukwepaji wa kodi sikutegemea Mwigulu awepo katika baraza, Mawaziri wengine naona kama wako poa. hayo ni maoni yangu kama mtanzania mwenye nia njema na Taifa letu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad