Suluhisho la Foleni katika Jiji la Dar....Kuna Umuhimu Gani wa Wizara Zoote Kuwa Jijini Dar es Salaam?

Ili kupunguza foleni katika jiji la Dar es Salaam, nashauri Serikali itawanye makao makuu za Wizara katika mikoa mbalimbali nchi nzima! Mkoa wa Dar es Salaam kipekee kabisa umekaliwa na wizara zote, hivyo wafanyakazi na taasisi zake wapo Dar es Salaam! Mabenki, na makampuni mengine mengi yanaona ni rahisi na faida yakifunguliwa Dar es Salaam kulikoni yangefunguliwa mikoani ambapo purchasing power ya wananchi wa huko ipo chini!

Endapo Wizara zitatawanywa nchi nzima, at least wizara tatu kila mwaka itaondoa watumishi wengi Dar es Slaam na familia zao, hence kupunguza idadi ya magari barabarani! Pia itafanya mabenki na taasisi zingine kufungua matawi kwenye hiyo mikoa kama siyo kuhamia kabisa! Zoezi hili likifanikiwa, Dar es Salaam kutabakiwa na wizara na taasisi za umma chache zenye umuhimu wa kubakia Dar!

Dar es Salaam ina foleni kwakuwa, idadi ya wakaazi wake inazidi kuongezeka siku hata siku lakini miundo mbinu ni ileile, haiongezeki! Umiliki wa magari limekuwa ni jambo la kawaida sana kwa karibu kila mtu anayejishughulisha anamiliki gari kama siyo magari! Juu ya hilo ni kuwa, karibu wote tukiamka asbuhi tunaelekea uelekeo mmoja wa mjini, na woote tunatawanyika kutoka mjini ikifika jioni! Ijapo kumekuwa na jitihada nyingi kutengeneza barabara za michepuko, lakini taratibu kadri muda unavyoenda na zenyewe zinazidiwa! Kutoka Mbezi hadi mjini au mjini to mbezi ya Kimara inaweza ikuchukue hadi masaa matatu?. Muda wa Abood kutoka Dar hadi Morogoro!

Mtu wa mikoa mingine, akitaka jambo lake wizarani itamlazimu aende Dar, lakini mkaazi wa Dar ni daladala tu ya kumfikisha mjini, na ana uwezo wa kutembea wizara karibu zote kwa mguu na akazimaliza! Kwa hali hii, wakaazi wa mikoa mingine hawatendewi haki licha mzunguko wao mdogo wa hela wa mikoani itabidi achukue basi, treni au ndege na akodishe hoteli akiwa Dar hadi amalize mambo yake. Kuna wakaazi wengi wa Dar hawajawahi kufika Kigoma, Rukwa, Kagera, Ruvuma nk kwakuwa hamna jambo linalomfanya aende mikoa hiyo? Endapo mikoa hiyo ingepelekewa Wizara zikahamia huko, basi kama hajaenda kusalimia basi kuna jambo atalifuata katika wizara ilio katika hiyo mikoa!

Ushauri ni kuwa, katika kuhamisha huku kwa Wizara, zilenge ile mikoa yenye mwamko mdogo wa kimaendeleo ya kijamii na uchumi! Wizara ya Elimu, ihamie Kigoma , Mambo ya Ndani ihamie Dodoma, Maji Nishati ihamie Singida nk nk? Kwa hali hiii hata wakazi wa huko wataneemeka na mzunguko wa fedha kutoka kwa wahamiaji wapya!

Kuna umuhimu gani wa wizara zoote kuwa jijini Dar es Salaam?
Ofisi za Balozi mbalimbali, kuna ulazima wa wao wote kukaa hapa Dar?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad