Waziri Mkuu mstaafu ambaye juzi alichukua kadi ya uanachama wa Chadema, Frederick Sumaye ameukosoa uamuzi wa rais John Magufuli kuwasamehe watu waliorejesha kiasi cha fedha walichokwepa kulipa kodi.
Sumaye alitoa mtazamo wake huo juzi jijini Arusha baada ya kukabidhiwa kadi ya uachama wa Chadema ikiwa ni miezi takribani mitatu tangu alipojiunga na harakazi za Ukawa na kutangaza kuihama CCM.
“Unawezaje kutoa msamaha kwa wezi na wakepa kodi nchini kwa kuwapa siku saba eti wawe wamelipa madeni yao? Hili ni jambo la ajabu kabisa. Unawezaje kupitisha msamaha kwa wezi na wakwepa kodi? Sumaye alihoji.
“Haya tuliyaona wakati wa sakata la EPA na sasa tunayaona kwenye makontena, wezi wanasamehewa,” aliongeza.
Zaidi ya shilingi bilioni 10 zimekusanywa na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kutoka kwa wafanyabishara mbalimbali waliokwepa kodi kupitia makontena yaliyotoroshwa bandarini baada ya rais kutoa siku saba za ‘rehema’.
Baada ya siku hizo kupita (ijumaa), hivi sasa serikali inawasaka wafanyabiashara 15 ambao hawakujisalimisha katika kipindi kilichotolewa na rais Magufuli. TRA imeahidi kuchukua hatua kali za kisheria dhidi yao kama rais alivyoagiza.
Sumaye hebu piga kimya, hivi wewe ulifanya nini cha maana ulipokuwa waziri mkuu?? Ulimfunga nani?? Kama hukutaka wasamehewe, unaonaje JPM akianza na huyo 'shogako' Lowasa na sakata lake la Richmond?? 'MZIGO UPO KICHWANI, VIPI KWAPA UTOKE JASHO??????' Hebu mwacheni JPJM afanye yake, HAPA KAZI TU...
ReplyDeletethank you mdau, tena yeye ndio siongee kabisaaaaa, all this went down wao wakiwa madarakani miaka na miaka, so we don't want hear you bid mouth now period. Let the guy do his job. tena kazi mbayo takiribani miaka 40 ya ongoza went hamkuifanya, yeye ameweza kufanya kwa mwezi mona please give us break
DeleteKwani chadema mnamtambua JP kama ndio Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?? Tuanzie hapo kwanza.................
ReplyDeleteFunga domo lako Sumaye, wewe na huyo fisadi mwenzio Lowase mlistahili kuwa gerezani Segerea kama sio Ukonga, rudisha haraka lile 'shamba pori' kule Morogoro.......utasamehewa nawewe pia
ReplyDeleteKweli wewe ni Mr.00, hivi ulipokuwa waziri mkuu ulifanya nini kizuri tena chamaana, cha kukumbukwa ambacho kilileta faida kwa nchi, kikaliingizia taifa angalau sh. 100 kwa mwaka???? Mr. Ziro, hebu tulia kama unanyolewa, mwache 'MWANAUME JPJM' aka TINGATINGA aendelee KUTINGISHA..........
ReplyDeleteThank you mdau, hugo ni mr. 0000 kweli
DeleteACHA UPUMBAVU WEWE SUMAYE KAMA HUJUI NINI KINACHOENDELEA KAA KIMYA
ReplyDeletehio ndo ccm chama cha kulindana, kuna wezi, majangangili, majambazi, wachuna ngozi, wauaji wa albino, madalali. sasa hivi wamekuja na maigizo ya magufuli
ReplyDeleteSay what???????? Walipokuwa wanakwepa kodi SUMAYE alikuwa kwenye system mbona hakufanya chochote????????Acheni upuuzi wenu, sasa ndio mnajifanya kuwa mnawaona mafisadi ni wabaya? Mlikuwa wapi miaka yote? Mwacheni mzee wa hapa kazi afanye kazi yeke. MAGUFULI KIBOKO YA MAFISADI, MTAISOMA NUMBER MWAKA HUU!!!!!
ReplyDeleteactually you know what Sumaiye? you next, na wewe ueleze mali zako ulipataja, na kwanini mliuziana nyumba za serikali. Pumbavu sana were mr. zero
ReplyDeleteWatanzania lazima tuelewe wapinzani si maadui ni chachu ya maendeleo katika nchi zote duniani
ReplyDeleteTatizo la CCM hili halikubali lazima mjuwe bila UKAWA , Leo hii Magufuli asingekuwa Rais Kwani CCM ilikuwa na watu wao, lakini baada ya kuona kibano , mkamchagua
Lazima tuelewe magufuli si mungu ni binadamu Kama wengine na na naamini sana magufuli anasoma na kusikiliza ya wapinzani vile vile
CCM wengi wenu mnatabia ya kusema ndiyo sababu ni rais hapana ikifike wakati rais naye akosolewe na wana CCM si wapinzani pekee
ss ndo anaona gari lilikuwa bovu baada ya kushuka
ReplyDelete