Taarifa: Ziara ya Edward Lowassa Kuwashukuru Watanzania kwa Kura Walizompigia

Taarifa inatolewa kwa vyombo vya habari na umma wa Watanzania kwa ujumla kuwa aliyekuwa Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Ndugu Edward Lowassa atazungumza na wananchi wa Tanga katika mkutano wa hadhara utakaofanyika mjini Tanga, siku ya Alhamis, Desemba 17, 2015.

Mkutano huo ni sehemu ya ziara ya viongozi waandamizi wa Chama na UKAWA kwa ujumla ambao watakwenda maeneo mbalimbali nchi nzima kuwashukuru wananchi kwa namna walivyounga mkono upinzani na agenda nzima ya MABADILIKO katika uchaguzi mkuu uliopita na wanavyoendelea kuweka matumaini yao kwa upinzani kuwa ndiyo nguzo imara wanayoweza kuitegemea kuwaletea mabadiliko ya kweli kwa ajili ya maendeleo yao na ustawi wa taifa kwa ujumla.

Itakumbukwa kuwa mbali ya Watanzania kupiga kura za ushindi katika nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu uliopita, wananchi waliwachagua wabunge wengi wa upinzani wanaotokana na UKAWA na kuongeza nguvu kubwa ndani ya bunge hususan kupitia Kambi ya Upinzani Bungeni ambayo itakuwa serikali yao mbadala huku wakiviamini vyama hivyo kusimamia na kuongoza halmashauri zipatazo 34 nchi nzima, ikiwa moja ya misingi imara katika kupigania mabadiliko ambayo Watanzania wanayataka.

Wananchi wanastahili shukrani kwa imani hiyo kubwa ambayo ni ishara ya wazi kuwa matumaini yao kwa miaka mingine mitano yatasimamiwa na kuongozwa na upinzani imara kupitia UKAWA.

Katika ziara hiyo ya Tanga, Ndugu Lowassa ataambatana na viongozi wengine waandamizi wa UKAWA ukiwa ni mwanzo tu wa ziara kubwa itakayokwenda nchi maeneo mbalimbali nchi nzima.

Imetolewa leo Jumanne, Desemba 15, 2015 na;

Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. agenda nzima ya mabadilikoo... lowasaaaa
    sawa sawaa

    ReplyDelete
  2. Kila la kheri katika ziara hiyo ndug.Lowassa

    ReplyDelete
  3. Acha kiloba kunywa bia utapata mabadiliko

    ReplyDelete
  4. Ulipo Tupo, HAIJALISHI.....!

    ReplyDelete
  5. Nice move! Wananchi tunashukuru sana kambi ya upinzani maana changamoto wanazoipa serikali kwa kiasi kikubwa zinasaidia sana maendeleo ya nchi hii! Tunaamini mtaendelea kuipa changamoto serikali na kuibua hoja za msingi kwa maendeleo ya taifa! Haipingiki kuwa nyinyi ndiyo vinara wa mabadiliko

    ReplyDelete
  6. Hahahaha kampeni zinaendelea

    ReplyDelete
  7. Ameshafunga choo lakini, hatutaki ya chato yajirudie tena

    ReplyDelete
  8. CCM Acheni ushamba mbona kinana anazunguka Kila kona
    Waacheni UKAWA msaidieni magufuli kufichuwa mafisadi ndani ya CCM

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad