Taasisi 1,200 Duniani Zampa Tuzo ya Amani Edward Lowassa

Taasisi 1,200 duniani zitampa aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa Tuzo ya Amani kutokana na utulivu aliouonyesha kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu.
Akizungumza kutoka Bukavu, DR Congo, mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa jamii, Mchungaji William Mwamalanga alisema Lowassa amechaguliwa jana mjini Bukavu na wajumbe 1,400 wa mkutano huo.

Mwamalanga alisema wajumbe wanaohudhuria kongamano la amani wanatoka mataifa ya Ulaya, Marekani, Asia na Afrika kwa kuwashindanisha wanasiasa 1,000 ili kumpata Kiongozi Bora wa Amani mwaka 2015, ambaye anajali na kuangalia maslahi ya jamii badala ya madaraka.
Hatua ya kumpatia tuzo Lowassa ni baada ya kuelezwa kuwa amedumisha amani hiyo hata baada ya kushindwa uchaguzi Mkuu wa Rais Oktoba 25.

Katika uchaguzi uliopita, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)ilimtangaza Dk John Magufuli kuwa mshindi kwa kupata kura 8,882,935 ikiwa ni asilimia 58.46 wakati Lowassa alipata kura 6,072,848 sawa na asilimia 39.97 ya kura zote.

Mchungaji Mwamalanga alisema katika kongamano hilo, wajumbe walijadili hali ya amani duniani na mchango wa wanasiasa katika kulinda amani hiyo.
Alisema kuwa wanasiasa barani Afrika wamekuwa vyanzo vya migogoro na mauaji ya raia wakati wa uchaguzi, kama ilivyo nchini Burundi. Hata hivyo, alisema kuwa wajumbe walipongeza ushindi wa Dk Magufuli, lakini wakasema umetiwa dosari na hali ya kisiasa Zanzibar baada ya matokeo kufutwa.

Alisema wajumbe wa kongamano hilo linaloshirikisha maaskofu, masheikh na vijana kutoka madhehebu mbalimbali ya dini barani Afrika, wamemuhimiza Rais Magufuli kumaliza utata wa uchaguzi wa Zanzibar.

Baada ya kupitishwa kugombea urais kwa tiketi ya Chadema, Lowassa alitangaza kuwa angefanya kampeni kistaarabu na kwa amani na baada ya matokeo aliwatuliza wafuasi wa chama hicho, akisema “hakuna anayeweza kuizuia bahati ya mtu” kwa hiyo kama amepangiwa kuwa rais, atakuwa.
Lowassa, ambaye ni Waziri Mkuu wa kwanza wa Serikali ya Awamu ya Nne, aliongeza upinzani kwenye uchaguzi wa mwaka huu baada ya kuihama CCM na kujiunga na Chadema iliyoukuwa na nguvu ya vyama vingine vitatu vya NLD, CUF na NCCR-Mageuzi.
Kama alivyoahidi, Lowassa hakutumia mikutano yake ya kampeni kushambulia mambo binafsi ya wagombea wengine, bali muda mfupi kuomba kura.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ni mtu wa amani anastahili tuzo,mbwa walibweka kila kona mchana na usiku huku wakimdhihaki, kwa matusi mengi sana lakini hakunyanyua mdomo wake kumjibu mbwa yeyote, na mpaka sasa bado anatukanwa na wala huwa aangaiki na mbwa, yeye ni mtu wa amani sana. Mungu mpe afya na maisha marefu.

    ReplyDelete
  2. hahahhahahahahahahah
    hana jipya mwizi huyo alikosa vya kujibu si ukweli unaumaa
    fisadiiiiiii papaaaaaa!

    ReplyDelete
  3. Amepewa tuzo amekuwa Diamond!? Duh!! hahahahahahaha aaaaaahhhhhhhh

    ReplyDelete
  4. Bado tunazifanyia utafiti hizo habari kutafuta uhalisia wake. Mabo ya mitandao watanzania lazima wwawe makini kutafuta uhalisia wa kile kilichoandikwa mitandaoni kabla ya kusherekea au kulaani.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad