Tajiri Anayemiliki Makontena Yaliyopotea Bandarini Ajitokeza......Amtupia Lawama Wakala Wake

Tajiri huyo anayetambulika kwa jina la Nassoro Ahmed bin Slum anayemiliki kampuni ya Bin-slum Tyres Ltd, amejitokeza na kukiri kumiliki baadhi ya makontena yaliyokumbwa na kashfa hiyo lakini  amekana kosa lenye sura ya kukwepa kodi  akidai kuwa limefanywa na wakala wake.

“Wafanyabiashara hatuna mamlaka ya kulipa kodi moja kwa moja serikalini. Tunalipa kodi kupitia kwa wakala aliyechaguliwa na serikali. Mimi nilimlipa kazi wakala wangu ambaye nimekuwa nikifanya naye kazi kwa miaka 10,” Bin Slum ameliambia gazeti la Raia Mwema.

Mara kwa mara huwa ananiletea nyaraka za malipo ya kodi lakini kwenye mzigo huu wa sasa  ambao kontena zangu zina matatizo ya kodi, alinitangulizia mzigo na mimi nikamdai nyaraka. Yeye aliniambia ananiandalia faili,” alieleza.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliagiza wote wanaohusika na kashfa hiyo kukamatwa na kuchukuliwa hatua na kodi iliyokwepwa ilipwe.

Tayari watu 12 wanashikiliwa na jeshi la polisi kufuatia sakata hilo.
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Safiiiiiiiiiiiiiiii!
    Imechukua muda gani tangu uambiwe na wakala wako unaandaliwa faili?kwa nini hukushtuka na kujiuliza vipi mizigo mingine ije na nyaraka bila faili huu ndio uje na faili?Na je hatua gani umechukua baada ya kuona unamiliki mzigo ambao bado hujui kama umelipiwa kodi au laa?Hakuna KANJANJA lipa kodi ya watanzania,HAPA KAZI TU.

    ReplyDelete
  2. Hawa wanaojitokeza sasa hivi wanataka kuilaghai serikali isiwachukulie hatua kali za kinidham kwa kukwepa kodi stahili iliyotakiwa kulipwa kabla ya mzigo kutolewa. kusema anamlaumu wakala wake ni dhahiri kwamba anafaham kilichotokea. kama ilikuwa ni utaratibu wa halali basi makontena hayo yasingetoroshwa usiku. Huyu ni lazima awe mfano kwa wengine waliyopitia hatua kama yake ili taifa lisonge mbele. Serikali ni lazima iwe imara ili kuifufua Taifa Kiuchumi.

    ReplyDelete
  3. Asante sana Rais Magufuli. Mungu akulinde, utimikie taifa na Watanzania.

    ReplyDelete
  4. Asante sana Rais Magufuli. Mungu akulinde, utimikie taifa na Watanzania.

    ReplyDelete
  5. Uongo tuu huu. Ameutunga yeye na wakala wake. Hizo ndio zao zilikuwa. Ila sasa wamepatikana.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad