TFDA Yateketeza Shehena ya Vipodozi

Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Kanda ya Kati imetekeza shehena ya vipodozi vyenye viambata vya sumu vya thamani ya Sh49 milioni.

Vipodozi hivyo tani mbili na nusu, viliteketezwa mbele ya maofisa polisi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), usalama wa Taifa na wamiliki wake baada ya kukamatwa vikisafirishwa kwa njia za panya hivi karibuni.

Mkaguzi wa Chakula na Dawa wa TFDA, Dk Endrybet Mbekenga alisema jana kuwa kazi hiyo itakuwa mwendelezo wa uteketezaji wa bidhaa nyingine zenye kemikali ambazo zina madhara kwa binadamu.

Alisema shehena hiyo ilikutwa ikishushwa kutoka kwenye lori la mafuta.

Dk Mbekenga aliwataka wafanyabiashara kuacha kuendelea kuingiza bidhaa hizo nchini zilizopigwa marufuku na Serikali kwa sababu zina sumu.

Alisema vipodozi hivyo athari zake ni kubwa kwa matumizi ya binadamu, ikiwamo wanawake kuota ndevu, kupata saratani ya ngozi na kuathiri figo.

Alionya kuwa wafanyabiashara watakaokiuka kanuni za mamlaka hiyo, watachukuliwa za kisheria.

Ofisa wa Forodha wa TRA, Mohamed Mnonda alisema watashirikiana na polisi na TFDA kuzuia bidhaa zote zinazoingizwa nchini kinyemela kwa kukwepa kodi.

Kwa mujibu wa Sheria ya Kodi, ni makosa kwa gari linalosafirisha bidhaa kwenda nje ya nchi kurudi nchini na bidhaa nyingine kutoka nchi iliyopelekewa mzigo.

Nafasi za Ajira

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad