Ufisadi Bandari na Mabehewa, Kamati Kuu ya CCM yawakingia Kifua Sitta na Mwakyembe

Katika hali inayoashiria kuwa CCM haijajifunza somo kuwa wananchi wamekerwa na ufisadi.
CCM inataka kuwafanya wananchi wakose matumaini kwa serikali yao, na hivyo kupelekea kuona kuwa juhudi za Raisi Magufuli ni hatua za kuwabana dagaa huku wakiyaachia mapapa yakitanua mtaani.

Hatua hiyo ya kamati kuu ni hatua ya hatari sana kwa sababu inaweka maslahi ya watu wachache mbele kuliko Taifa, Hili ni jambo la kutisha na kuogofya sana, kama chama kilichojinadi kurudi katika misingi kinawalinda watu ambao Kwa kutumia nyadhifa zao wameifikisha nchi katika hali mbaya,basi ni jambo la kuwakatisha tamaa na kuwanyong'onyesha wananchi walioanza kurejesha imani kwa serikali yao.


DKT Harrison Mwakyembe na Samwel Sitta ambao walikuwa mawaziri wandamizi kwenye Serikali ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ambao kwa sasa wanatuhumiwa kwenye Kashfa za ufisadi, imefichukua kuwa uwezekano wa kupandishwa mahakamani watu hao umeyeyuka. Mtandao umedokezwa,Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.


Sababu iliyotajwa ya kuwaokoa mawaziri hao imetokana na Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM,CC kilichoketi jana kimekuja na mipango mahususi ya kuwaokoa viongozi hao wanajiita na kuitwa ni waadilifu.

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya Kikao hicho ambazo zimevuja zinasema Kamati ya CC licha ya kujadili mambo mbali mbali ila jambo la ufisadi ambao uliibuliwa kwenye Bandari ya Dar es Salaam pamoja na Kashfa ya ununuzi wa mabehewa 250 ya mizigo pamoja na Mabehewa 50 ya kubebea mafuta ambayo yamebainika kwa sasa ni mabovu nalo lilizungumziwa.

Chanzo chetu hicho kilichokuwa ndani ya CC kimedai kuwa viongozi wa mkutano huo walitaka suala la kuwachukulia hatua mawaziri hao waliokushika nafasi ya wizara ya uchukuzi,litazamwe kwa umakini kwani linaweza kukiingiza chama hicho tena kwenye mgogoro.

Yaani CC wameona hawa wakina mwakyembe na Sitta wakipandisha Mahakamani kujibu tuhuma hizo,basi chama chetu kitaingia kwenye mgogoro ambao unaweza hata ukapelekea idara hata ya Ikulu ya kipindi kile kufika mahakamani maana ufisadi huu wa Mabehewa ni mkubwa sana na umefanywa na mtandao mkubwa ndani ya nchi kimesema Chanzo chetu hicho.

Hata hivyo Kamati hiyo ya CC licha ya kuwakingia kifua mawaziri hao kunakuja ni ikiwa ni siku moja kupita baada ya Rais John Magufuli kuvunja Bodi ya Bandari ambayo Samwel Sitta wakati yupo Uchukuzi aliiunda Bodi ambayo Magufuli ameivunja kutokana na kuhusika kwenye ufisadi,

Hatua nyingine kwa bandari hiyo ni Rais Magufuli kutengua uteuzi wa mkurugenzi mkuu wa Bandari Awadh Massawe baada ya kubainika pia ameshindwa kuisimamia Bandari hiyo kwa kupelekea Ufisadi wa kutisha ikiwemo upotevu wa Kontena zaidi ya 2000.

Sanjaria Bandarini hapo Rais Magufuli pia alimsimamisha kazi,Katibu mkuu Wizara ya Uchukuzi Shaaban Mwinjaka kutokana na kuitia hasara serikali ya bilioni 16 kwenye sherika la Reli ya Kati TRL.
Taarifa zilizopatikana wiki iliyopita zilisema Rais Magufuli alikuwa tayari amekabidhiwa ripoti ya Ufisadi wa Bandarini na TRL ambao unatajwa kuwa kwa namna yoyote uwezi ukawaacha mawaziri wenye dhamana ya Uchukuzi,


Hata ufanyaje ndugu,kwenye ufisadi wa huu wa kutisha lazima Sitta na Mwakyembe watawabwa Msalabani tu, maana wakati makontena hayo yanapoteka kati ya 2014 na 2015 mawaziri hawa walikuwepo uchukuzi hivi hawakuyaona haya au nao kuhusika katika kubariki wizi huu,harafu ukitoka kwenye Bandari unakuja kwenye TRL hapa ndio kuna madudu ambayo yanawaacha watupu,wanaojiita wapiganaji wa ufisadi amesema Mchambuzi wa Siasa kutoka chuo kikuu cha Dodoma ,John Shilima.

Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. NINAMUULIZA NAPE NNAUYE AMBAYE NDIYE KATBU MWENEZ WA CCM,JEE UHUJUMU UCHUMI TRA,PTA,TRL VILIZUNGUMZWAKWENYE CC YA CCM ?JEE ALIUNGWA MKONO RAIS MHE.MAGUFULI NA KUTAKIWA AWASHUGHULIKIE WALE WOTE WALIOKUA NA DHAMANA,WAKAICHEZEA DHAMANA ILE NA MATOKEO KULIINGIZA TAIFA KWENYE KASHFA NA WAHUSIKA KUIIBIA NCHI MABILLION KWA MABILLION.

    ReplyDelete
  2. CCM NI ILE ILE ; WIZI MTUPU LAKINI INAHITAJI UPEO WAKUFIKIRI ILI KUJUA HILO; KITU AMBACHO WATZ WENGI WAMEKOSA SABABU WAMEKOSESHWA ELIMU WASIJIELEWE

    ReplyDelete
  3. Wewe mwandishi wacha vijembe na visasi hata Nelson Mandela baada ya miaka 27 jela hakuelekeza nguvu zake kuwa adhibu waliomfunga alicho fanya ni maridhiano na nchi kusonga mbele kwa hiyo wewe maoni yako uchwara huridhiki na juhudi za Magufuli una taka aache kuziba mwanya ya mafisadi akae ashughulikie visasi ama kweli sisi wabongo hatuna shukurani

    ReplyDelete
  4. I knew it, a good leader must be surrounded by effective people, kazi Sana coz ccm are corrupted,but tutafika Tu na ili tufike lazima magufuli awape vyombo vya habari uhuru WA 100% ili WA tz na dunia nzima wawajue wahujumu WA nchi

    ReplyDelete
  5. kumbe hayo ndo mafisadi papa, mi nilidhaniaga luwasa wa maamuzi magumu. kumbe mwakiembe na mzee wa standard and speed ndo manyangumi magumegume yaliyoshindikana..... mwaka huu tutajua mengi sana. magufuli asante i think umeshuka kutoka juu.

    ReplyDelete
  6. akimkamata na kinana ntamuheshimu sana,sio anazunguka zunguka wakati anajua tatizo liko wapi

    ReplyDelete
  7. MHESHIMIWA MAGUFULI,ASALAAM ALEYKUM.TUPO PAMOJA NA WEWE.NI MSHIKAMANO.OMBI.HAPA TUMEGUNDUA BILA SHAKA YEYOTE KWAMBA WATU HAWA WAWILI SAMWELI SITTA NA HARISON MWAKYEMBE NI WEZI WAKUBWA,WAHUJUMU UCHUMI ZIMEPOTEA BILLION 600.TIMIZA WAJIBU WAKO HAWA WATU WAKAMATWE,WAFUNGULIWE MASHTAKA,KWA NINI UNAENDELEA YA KUWALEA?YUKO WAPI KWA SASA DANIEL YONA,YUKO WAPI KWA SASA BASIL MRAMBA?SI WAPO JELA WAMEFUNGWA KWA MAKOSA KAMA YA HAWA.WASIPOKAMATWA TUTAANZA KUWA NA MASHAKA MAKUBWA YA UTENDAJI KWAMBA WEZI WAKUBWA 'WANAOGOPEWA'

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad