Serikali imepoteza jumla ya Sh48.47bilioni baada ya makontena 11,884 na magari 2,019 kupitishwa badarini Dar es Salaam bila kulipiwa kodi.
Hata hivyo, jumla ya watu saba wanashikiliwa na wengine nane wanatafutwa na Jeshi la Polisi kwa kuhusishwa na ukwepaji kodi huo uliolikosesha taifa mapato.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawaamesema ufisadi huo umebainika baada ya serikali kuzifanyia ukaguzi bandari zote za nchi kavu (ICDs) jijini Dar es Salaam.
Akifafanua, Waziri Mbarawa amesema makontena hayo 11,884 yalikuwa na thamani ya Sh 47.4 bilioni wakati magari gari 2019 zenye thamani ya sh 1.07bilioni yalitolewa bandarini pasipo kulipiwa tozo.
Ufisadi Mwingine Wa Bilioni 48 Waibuliwa Bandarini .......7 Watiwa Mbaroni, 8 Wanasakwa na Jeshi la Polisi
4
December 29, 2015
Tags
Mh!! basi haya da.... dili dili diliii mtindo mmojs ds!!!
ReplyDeleteNdio tusiojua mchezo huu tulikuwa tunapata shida! duh jamani maana tulikuwa tunajiuliza mbona ukiagiza gari ushuru wake mkubwa hivi? kumbe kuna watu wanakwepa kulipa kodi hatimaye wanasababisha wachache wenye nia mbaya na nchi hii ....basi jamani inauma sana Mungu wape afya njema wale wote wanaosimama kwa niaba ya watanzania wengine
ReplyDeleteCCM haniingilii kichwani kuubuwa utawala wa awamu ya nne nje nje
ReplyDeleteKwani hamna vikao
Kwani rais alikuwa hashauriki, tusitake sifa nyote mlikuwa huko huko inawezekana mmeisha clean Mali zenu sasa mnaanza kubwata
Kama mliona hafai mbona mlibakia madarakani?
Waliochoshwa Na ufisadi walihama CCM
AnonymousDecember 30, 2015 at 3:18 AM
DeleteKashfa zingine
Mfungeni basi huyo aliyeleta yote haya
Lakini wema wake Na upole umemponza
Kwani aliwachaguwa nyote hamkumshauri
Ni aibu leo kutoa uozo wake