Ufisadi:Kigogo Wa Ikulu Adaiwa Kutumia Fedha za Umma ( Laki 8 ) Kufanya Masaji

Harakati za kuwasaka wabadhirifu wa fedha za umma ili waingie kwenye msululu wa opareshini ya kutumbua majipu iliyoanzishwa na serikali ya awamu ya tano zimeibua tuhuma nyingine zinzomhusu moja kati ya vigogo anayeiwa kuwa mfanyakazi wa Ikulu.

Taarifa zilizochapishwa katika gazeti la MwanaHalisi zinaeleza kuwa uchunguzi uliofanywa na gazeti hilo umebaini nyaraka zinazoonesha kigogo huyo alitumia fedha za walipa kodi kiasi cha shilingi 821,997.24 kwa ajili ya kufanyiwa huduma ya kukandwa mwili (massage), katika hotel ya kifahari ya Four Seasons Safari Lodge iliyoko ndani ya mbuga za wanyama za serengeti, Arusha.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, stakabadhi waliyoipata katika hotel hiyo ilionesha kuwa kigogo huyo alifika hotelini hapo April 17 mwaka huu tarehe ambazo Rais mstaafu Jakaya Kikwete alikuwa na ziara jijini Arusha.

Imeelezwa kuwa kigogo huyo ambaye hotel hiyo haikutaka kumtaja jina alilala katika chumba namba 9017 na alikuwa na mrembo wake ambaye kwa pamoja walipata huduma zilizoingizwa kwenye stakabadhi iliyolipiwa na Ikulu.

Mbali na huduma ya Massage, huduma nyingine zilizoorodheshwa nakala ya ankara hiyo ni usafi wa nguo ambao uligharimu shilingi 676,000.

Katika kutafuta kujiridhisha, gazeti hilo lilimpigia simu afisa wa hotel ya Four Seasons Safari Lodge ambaye licha ya kukataa kutoa maelezo alikiri kuwapokea baadhi ya wafanyakazi wa Ikulu katika siku tajwa.
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Makubwa majipu yapasuliwe kwa wote tangu mzee ruhusa hadi jakaya

    ReplyDelete
  2. Dah!kweli siasa inalipa........

    ReplyDelete
  3. Sasa hiyo yote ili iweje?Hii ni sawa na kesi ya nyani kushtakiwa kwa wizi wa mahindi halafu hakimu ni ngedere ipate picha hapo mwenyewe hukumu yake itakuwaje

    ReplyDelete
  4. @anonymous 5;29 kinachoangaliwa ni wapi tulipoanguka ili tuweze kurekebisha sasa hayo mambo ya nyani,ngedere hayo yako watanzania wanasonga mbele,wakihukumiwa vizuri wasipohukumiwa basi mungu atawahukumu hapa duniani au akhera, cha muhimu wewe chapa kazi

    ReplyDelete
  5. Unaona hiyo hela kubwa sana si ndio?achen watu wale maisha bwana

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad