Ukimya wa Lowassa,Sumaye na Mbowe Kuhusu MAJIPU Yanayotumbuliwa na Magufuli Wazua Maswali

Ukimya wa wanasiasa walioongoza harakati za kupambana na ufisadi katika majukwaa ya kisiasa, wakati huu Serikali ikichukua hatua za wazi na haraka kukabiliana na ubadhirifu wa mali za umma, umeibua maswali kuhusu uzalendo kwa nchi yao.

Miongoni mwa wanasiasa waliohusishwa na maswali hayo ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu, Frederick Sumaye, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe na mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa.

Akizungumzia sakata hilo jana, Mhadhiri Mwandamizi wa Masuala ya Siasa na Utawala wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Benson Bana, alisema kama kweli ni wazalendo, ni vyema wale wote waliokuwa wakipinga ufisadi wajitokeze hadharani, kupongeza hatua zinazoendelea kuchukuliwa.

Profesa Bana alisema hali inavyoendelea nchini kwa sasa ni wazi kwamba Rais John Magufuli, anapaswa kuungwa mkono na wote waliokuwa wakipinga ufisadi na ubadhirifu serikalini. 
  
Ni wakati muafaka sasa wale wote waliokuwa wanapinga ufisadi wakiwemo wanasiasa, wajitokeze hadharani kumuunga mkono Rais wetu, kama kweli walisema hayo kwa uzalendo na uungwana,” alisisitiza Profesa Bana.

Alisema ni wakati sasa wa Sumaye, Lowasa, Mbowe na wengine waliokuwa mstari wa mbele kueleza umma ufisadi na ubadhirifu serikalini kwenye kampeni za kuwania urais mwaka 2015, wakajitokeza hadharani kupongeza kazi inayofanyika.

Pia aliwataka wote waliosema hawataunga mkono serikali iliyoko madarakani, kufuta mara moja kauli yao, kwani yanayoendelea kufanywa ni mambo mazuri kwa ajili ya ustawi wa Watanzania wote bila kujali itikadi zao.

Magufuli na Ilani ya Ukawa 
“Yapo maneno kwamba Rais Magufuli anatekeleza ilani za vyama vingine na si ya CCM, haya maneno yapuuzwe ni kukosa hoja, ilani za vyama vyote vya siasa vinavyojitambua, zinajibu maswali haya ya wananchi,” alisema Profesa Bana.

Akifafanua hilo, Profesa Bana alisema kuna maneno yanaendelea kuzunguka kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu au kwenye mitandao ya kijamii, kuwa Dk Magufuli anatekeleza ilani za vyama vingine vya siasa na kusisitiza hoja hiyo haina mashiko.

Alisema Dk Magufuli anatekeleza yale aliyoahidi kwenye kampeni alipokuwa akiwania nafasi hiyo, kwa kuwa yapo kwenye Ilani ya CCM, huku akisisitiza kuwa ilani za vyama vya siasa mwaka huu zilifanana kwa njia moja au nyingine.

“Sisi tulipata bahati ya kusoma na kuchambua ilani za vyama vitatu CCM, Chadema na ACT-Wazalendo, tulipopitia ilani za vyama hivyo na vingine vilivyoshiriki kwenye uchaguzi uliopita, tulibaini zote zinafanana,” alisema Profesa Bana.

Alisema kama kuna chama kinasema ilani inayotekelezwa ni yao, wangekuwa mstari wa kwanza kujitokeza hadharani kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kutekeleza hayo, lakini kukaa kimya kunazua maswali mengi. 
  
Wajuta kutompa kura 
Alisema ni vyema Rais apewe nafasi aendelee kutekeleza anayofanya kwa sababu anajibu maswali ya wananchi yaliyokuwa yakisubiriwa kwa muda mrefu na kwamba wapo baadhi ya wananchi wanajuta hivi leo kwa kutompigia kura.

Tunazungumza na watu mbalimbali wanatuambia wanajuta kumnyima kura Rais Magufuli, kwa sababu kama asingeshinda, nchi ingekosa kiongozi mzuri na mwenye kasi ya maendeleo kwa wote,” alisema Dk Bana.

Wapenda utajiri 
Mhadhiri mwingine wa chuo hicho, Profesa Kitila Mkumbo alitoa mwito kwa Watanzania wote kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kubadilisha mitazamo yao ya kupenda vya bure, bali wafanye kazi kwa bidii.
  
Profesa Mkumbo alisema juhudi zinazofanywa na Rais Magufuli, zitakuwa na tija zaidi iwapo Watanzania wote watamuunga mkono kwa kubadilisha mitazamo yao ya kupenda utajiri wa haraka haraka.

Jitihada za Rais Magufuli pekee hazitoshi, bali jamii yote ya Tanzania lazima ibadilike, tuache kufanya vitu kwa mazoea na kupenda vya bure na utajiri wa haraka haraka, bali tupende kufanya kazi kwa bidii,” alisema Profesa Mkumbo.

Alisema masuala ya ubadhirifu na ufisadi ni mambo sugu yanayosumbua nchi na hatua zilizoanzwa kuchukuliwa na Rais Magufuli ni nzuri kwani tofauti na serikali zilizopita, yeye anatekeleza kwa kasi zaidi.

Ubadhirifu ni tatizo sugu nchini, lilianza kufanyiwa kazi tangu enzi za Mwalimu Nyerere hadi Rais mstaafu Jakaya Kikwete, ila kwa awamu hii ya Rais Magufuli, yeye anatekeleza kwa kasi zaidi,” alisema Profesa Mkumbo.
Tags

Post a Comment

14 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ukimya wao sababu
    Kura wameeibiwa hata magufuli
    Afanye Tanzania iwe akhera
    Bado wanalaani kilichomuweka madarakani
    Hawana shida na magufuli Bali hutupendi style au mfumo uliyomuweka mafuguli madarakani
    WA wizi WA kura haaaaaaaangiiiiii akilini Upike supu ya kuku na nguruwe sufuria moja baadaye usume hii kuku halali , guruwe haram
    Magufuli hajasema lolote kuhusu uchaguzi wa Zanzibar Kwani yeye ni rais WA Tanganyika Au Tanzania
    Kila kukicha yupo kwenye tra , bandarini
    Kwani jk kakomba fedha zote
    Wamempa nchi masikini pole ndugu yangu magufuli

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pole sana ndugu.Nakushauri kuwa mpole.Magu ndio chaguo la wengi.Muombee tu.

      Delete
  2. unachokiongea ww,nahic hazikutoshi.ni ushaidi gani uliotumia kutudhihirishia kuwa wizi ulifanyika ili kumuingiza magufuri ikulu? piga picha ya idadi ya wabunge wa ukawa kisha tafakari lowasa angeshinda angetengeneza serikali ya namna gani! kulikuwa na mafuriko ya kwenye majukwaa na mafuriko ktk sanduku la kura.kwa kipind hiki watu walijitoa kwa muda wao kusikiliza sera za kila mgombea kisha wakafanya maamuz sahihi.any way nisongee sana,ila magufuri ndio chaguo la wa tz,hata kama wakikaa kimya cc tutaendelea kumuunga mkono rais wetu jpm.wewe unataka aanzie Zanzibar tu !? angefanya hivyo ndo ungesema kuwa aliingia ikulu kwa haki? jpm hawez kwenda na mambo yote at once.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Shoga wewe
      Kama mnauye na makonda

      Delete
    2. Kuna tofauti ya uchaguzi wa wabunge na urais
      Senge wewe
      Nampenda magufuli lakini CCM sipendi hadi akhera
      Na ndo maana naafanya yote kwa ilani za UKAWA
      Yupo CCM kichama lakini Rohan moyo wake Upo UKAWA

      Delete
    3. unaamini kabisa lowasa angeeza fanya haya anayofanya magufuli kuokoa trillion ndan ya mwezi mmoja kukemea ufisadi na vitu ka hvyo????

      Delete
    4. Mbona povu linakutoka lol! kubali tuu kuwa CDM iko ICU kwa sasa, Nimeshajuta kuchafua kidole changu kuchagua CDM nikiamini CCM ni walewale.. Lakini kwa uhakika ni kwamba CCM walishinda kwa kishindo kama ni wizi ni kidogo sana, Nimesharudi nyumbani CCM HOYEEE, JPM HOYEEE!

      Delete
  3. 12:01 unatafuta bwana bwabwa nini?tupe taarifa wanaume wakutafute.

    ReplyDelete
  4. Anatimiza ilani ya UKAWA

    ReplyDelete
  5. Magufuli anatumia ilani ya CCM,mnaodhani Magufuli anayoyafanya yanatokana na ilani ya UKAWA tafuteni ilani ya CCM,UKAWA na ATC muzisome muone tofauti yake.Uzuri wa Magu haya tunayoyaona anafanya yote alikuwa anakemea hata wakati wa kampeni.

    ReplyDelete
    Replies
    1. kweli kabisa hivyo vyama vingine havina ilani ccm inatumia ilani yake na ndiyo magufuli alikuwa anazunguka nayo wakati wa kampeni
      kama mtu hurudhiki na haya anayotenda magufuli basi wew utakuwa na matatizo

      Delete
  6. Kubali ukweli sasa tumepata mkunaji lazima majipu yote yatumbuliwe kaatayari kama wewe nimmojawapo. hapa Kazi Tu.

    ReplyDelete
  7. Wee unaesema mmeibiwa kura, mbona hamkuibiwa Arusha,Kilimanjaro na Manyara?wee nakufahamu dereva wa bodaboda ambae uwzo wako wa kufikiria unaishia hapo. Hata kujiongeeza uwezi? angalia wenzako watakulaghai na watakulia mkeo na wewe ukiwepo. Acha sababu za kijicho rais makini ni JPM TU. Huyo fisadi wenu asingeweza kutumbua hata kipele na nchi ingemshinda ndani ya mwaka mmoja. Sababu mojawapo angalia wote amabo waliokuwa wanakwepa kodi, wizi wa mapato ya nchi na bandari ndiyo waliokuwa wanawapa fdha Ukawa. unafikiri angewafanya nini baada ya kuingia madarakani?tumia akili na kupamabanua mambo, Lowasa alisma akishindwa anarejea Monduli kuchunga ng'ombe,kama nyinyi kweli ni waungwana muulizeni sasa hivi yupo wapi.?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad